Bunge Live! J KIKWETE Tutakukumbuka

Bunge Live! J KIKWETE Tutakukumbuka

Kikwete anapitia phase ambayo Mkapa alipitia

Mkapa hata kutajwa hakutwa wakati wa uzinduzi wa uwanja wa Taifa
na Kikwete juzi hata kutajwa hatajwi uzinduzi wa daraja la kigamboni
Mimi naona ni bora JK hakutajwa wala hakuwepo kwenye uzinduzi, maana kwa nyota ya JK,angeifunika shughuli nzima.
 
Nadhani ni jambo jema tu kupata yaliyozungumzwa in summary kuliko kuangalia kitu kizima, kwa jamii zetu ambazo bado hatujakua na uwezo wa kumanage matumizi hata ya simu zetu sio vibaya serikali ikitusaidia katika hili, ili tuweke akili zetu katika kuzalisha na tuache wale tuliowachagua wafanye kazi ya kutuwakilishs vyema huko bungeni. Kungangania kutazama bunge live inamaana sisi wananchi hatuna hata imani na wale tuliowachagua kama wanafanya vyema kazi zao, sasa na tuwekeze katika kuchagua wawakilishi sahihi.
Post kama hizi zinaweza kusababisha mtu ukajikuta uko kizimbani maana zinatia hasira isiyo kifani.
 
kama opposition (UKAWA, etc) itakuwa so weak kiasi cha kushindwa kupata immediate solution ya changamoto ya kitoto kama hii, then I think they are very weak and sooner than later the electorate (myself included) will start losing confidence in them.

we are watching!
 
Ni bora magufuli dikteta kuliko JK mpanda ndege
Nchi ilipofika inahitaji uongozi wa Magufuli mixed grilled.hapo patamu, kina msigwa hawajitambui as a reader you can not issue such a low statement.kwani tunaishi kwa hisani, ndiyo maana nchi haitasonga kwa viongozi wa waina hii. Magufuli lazima aonyeshe kama nchi ipo na inasonga
 
Post kama hizi zinaweza kusababisha mtu ukajikuta uko kizimbani maana zinatia hasira isiyo kifani.
Na kweli mtaenda mahakamani wengi sana maana mnadhani nchi inaendeshwa kwa porojo na mihemko..
 
kama opposition (UKAWA, etc) itakuwa so weak kiasi cha kushindwa kupata immediate solution ya changamoto ya kitoto kama hii, then I think they are very weak and sooner than later the electorate (myself included) will start losing confidence in them.

we are watching!
In fact they are on test at the moment, they should prove to us that they are there for politicAl battle. Lamenting, lamenting as an opposition leader does not show that you are taking your bit.ETi bora mstaafu, purely this is kidding
 
Haya, serikali haina fedha. Wapo wenye fedha, Azam TV, StarTV nk basi waruhusuni hao waoneshe! Hamtaki! Kumbe mnachotaka kuficha nini?

Kikao cha bunge ni kikao cha kikazi sio mkutano na waandishi wa habari (press conference).Tofautisha kikao cha kikazi na press conference!

Wabunge wakishakaa na kumaliza kazi ya siku ndio taarifa za yale muhimu ya kazi na matokeo waliyofikia yanawekwa hadharani.

Taarifa hizo haziwi na vitu vya kipuuzi kama vile vya mbunge gani amtukana waziri au mbunge fulani kwa kumwita Kibaka nk.Zinakuwa na zile taarifa muhimu tu za kazi waliyofanya kazini kwenye vikao.Vikao vya kamati za bunge huwa havirushwi Live sababu ni vikao vya kikazi.Na kikao cha bunge ni kikao cha kikazi kile.Sasa hivi wabunge watafanya kazi barabara kuliko zamani kila mmoja anaomba kuchangia ili auze sura kwenye TV tu.Wachangiaji unakuta wako msururu!!!

Poleni waandishi kwa kukosa posho za kushinda Dodoma miezi mkiandika porojo za ndani ya bunge mara mpige picha sijui mbunge asinzia bungeni na upuuzi mwingine.
 
In fact they are on test at the moment, they should prove to us that they are there for politicAl battle. Lamenting, lamenting as an opposition leader does not show that you are taking your bit.ETi bora mstaafu, purely this is kidding

yaani, for once, wananifanya nimkumbuke the ever-omni-daring Rev Mtikila (rip).
 
Serikali za kifashisti ndizo zenye tabia za kuminya uhuru wa habari.
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli japo KJ MLISHO kuna mambo aliboronga lakini IPO siku tutamuelewa maana angekuwa huyu jamaa 95%wana jf tungeishia magereeezaa
 
Rais JPM ndio kwanza ana miezi sita IKULU...

- Suala la kutokuonesha bunge lilikuwepo tokea awamu iliyopita
- Cyber Crime Law ilikuwepo awamu iliyopita

Muacheni Rais Magufuli afanye yake ya awamu ya TANO, Watanzania tuwe na shukrani.
 
Katika jambo linalonikera ni kutoonyeshwa kwa bunge live,kwa hili tumerudi nyuma badala ya kwenda mbele.
 
Wahamisha magoli hamjui mnataka nini,vululu vululu tu mara kikwete dhaifu mara mnamkumbuka kikwete,achaneni na mambo ya live fanyeni kazi
 
Binafsi aheri kulala njaa niwe na freedom of expression kuliko kupewa chakula na nyumba alafu nifungwe kifikra kama punda,heri Jk kuliko awamu hii,upuuzi wa ubabe ndio ulicreate ombwe la uongozi kwenye nchi za Libya,Misri,etc so ziko kwenye kipindi kigumu cha mpito wa demokrasia
 
S
dah sijui nisemeje, kutokurushwa kwa bunge kumeniuma lakini, ukiangalia kwa maono ya mbali, uhuru wa habari na demokrasia kwa Africa una hasara pengine kuliko faida, ukiangalia nchi zenye matabaka makubwa yanayopingana ili kuweza kuyatawala yale makundi ni bora ukatawala kwa nguvu na kibabe kuliko kuruhusu demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari
vyombo hivi hutumika kutoa au kufichua taarifa ambazo zinaleta mgongano na kuchochea chuki zaidi katika jamii ambayo ilikuwa haipo stable na yenye watu ambao wanaweza kuwa influenced sana na wanasiasa
tukichukulia mfano wa nchi ambazo hazina demokrasia wala uhuru wa vyombo vya habari lakini kutokuwa na vitu hivi kumesaidia ni kama Rwanda

Rwanda hakuna demokrasia hakuna uhuru wa vyombo vya habari na kuna mtawala mmoja ambaye amebadilisha katiba ili atawale miaka mingine 7 na pia kumekuwa na shutuma nyingi za Kagame kutesa wapinzani wake na wengine kutokomezwa ki mafia,
ukiangalia hapa ni ukiukwaji mkubwa wa demokrasia na lakini ia Rwanda ni nchi ambayo ilikuwa na makabia mawili hasimu ambayo kama uhuru huo wa kujielezea, demokrasia ungekuwepo ungeweza kuamsha tena zile hisia na hata kusababisha machafuko mengine, lakini Rwanda ipo stable na inafanya vizuri

nchi nyingine ni Libya , nchi hii ilikuwa inatawaliwa na Ghadaffi kwa ubabe, alitawala kwa miaka zaidi ya 40 ukiukwaji mkubwa wa demokasia, uhuru wa habari wakosoaji wa serikali pia walikuwa wanateswa kufukuzwa na na kuuwawa
akaondolewa kwa mapinduzi, sasa hivi libya hakuna mtu strong wa kuitawala kibabe tena , bali vikundi vya watu na makabila mbalimbali vikipigana endlessly

Mfano mwingine ni Misri, nchi ya Misri ilikuwa ikitawaliwa na Hosni Mubarak, utawala wake ulikuwa hakuna demokrasia , na upinzani ulikandamizwa sana lakini nchi ilikuwa stable kuliko ilivyo baada ya yeye kuondoka na demokrasia kupanuka

kuna mifano mingi lakini hii inaweza kukuonyesha tu namna uhuru wa habari na demokrasia unavyoweza kuleta hasara kuliko faida kwa nchi za Afrika

Muda hautoshi kufafanua lakini upo totally wrong. Kuzuia uhuru hakuleti stability, kinyume chake ndiyo sahihi. Hizo nchi ulizozitaja Misri na Libya zimeparanganyika kutokana na udikteta wa hao viongozi wa mwanzo, siyo kutokana na uwepo wa demokrasia. Hata Rwanda, leo hii ikitokea ghafla Kagame hayupo, kama hakuna taasisi za kiuongozi na za demokrasia zilizoundwa, nchi inaparanganyika.

Madikteta huwa hawapendi kutengeneza taasisi wanataka kazi za kitaasisi wazitende wenyewe ili kulinda sifa binafsi na mamlaka. Kwa hiyo mambo mengi yanafanywa na mtu binafsi. Yeye huwa ndiye mtawala, sera na katiba.
 
Binadamu hupenda zaidi uhuru kuliko mali. Awamu hata wakifanya mazuri koasi gani, wakizuia uhuru wa watu, watachukiwa sana, tena kwa muda mfupi. Kumnyima mtu uhuru ni kumfanya hana akili, saikolojia ya binadamu ni kukataa kudharaulika.
 
Back
Top Bottom