Prof_Adventure_guide
JF-Expert Member
- Dec 21, 2023
- 519
- 1,463
Ndugu zangu Watanzania, huu si wakati wa kimya. Tumevumilia kwa muda mrefu. Sasa ni wakati wa unfiltered truth. Tuko katika kipindi ambapo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepoteza kabisa legitimacy yake ya kikatiba. Limegeuka kuwa a ceremonial rubber-stamp institution, linalotumika kuhalalisha uozo wa mfumo wa utawala, badala ya kusimamia maslahi ya wananchi. Hili ni Bunge la aina ya fedheha – dhaifu, lisilo na backbone, na linalogeuza sheria kuwa mzaha wa kisiasa.
Mwaka wa fedha 2020/2021, serikali iliwasilisha bajeti ya Shilingi Trilioni 34.88. Kati ya hizo, Trilioni 22.10 zilitengwa kwa matumizi ya kawaida na Trilioni 12.78 kwa maendeleo. Kwa macho ya juu juu, unaweza kudhani ilikuwa bajeti ya matumaini, lakini kwa waliochambua kwa undani, bajeti ile ilikuwa institutionalised economic fraud. Ilikuwa ya kisanii, iliyofichwa kwenye maneno ya kiufundi na namba nzuri zisizo na uhalisia. Ilikuwa financial deception ya kiwango cha juu.
Bunge lilikubali kupitisha bajeti hii licha ya ukiukwaji mkubwa wa Katiba na sheria za nchi. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Ibara ya 63(3)(c), inaeleza kuwa “Bunge ndilo lenye mamlaka ya kuidhinisha matumizi ya fedha za Serikali.” Lakini matumizi yalifanyika kabla ya kuidhinishwa rasmi na Bunge. Hii ni blatant constitutional breach. Aidha, Ibara ya 135(4) ya Katiba hiyo hiyo inasema kuwa “Hakuna fedha yoyote itakayotolewa kwenye Hazina ya Serikali isipokuwa kwa idhini ya Bunge.” Kwa hiyo matumizi yaliyofanyika bila idhini ni outright illegality – siyo makosa ya kiutawala, bali ni jinai ya kifedha.
Lakini haikuishia hapo. Serikali ilikiuka pia The Public Audit Act (Cap. 418), hasa Kifungu cha 10(1), kinachoitaka kutoa taarifa kamili kwa CAG juu ya matumizi ya fedha za umma. Katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2021, kuna ushahidi kuwa serikali ilificha baadhi ya taarifa au kuchelewa kuzitoa – huo ni administrative obstruction, unaolenga kuzuia uwajibikaji.
Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 (The Budget Act, 2015) pia ilivunjwa. Kifungu cha 18(1) kinasema wazi kuwa “No expenditure shall be incurred unless it has been approved in the Appropriation Act.” Lakini matumizi yalifanyika kiholela. Ni kama sheria haipo. Na bunge? Liliendelea kupiga makofi na kupongeza badala ya kuhoji. Huu ni uzembe wa kikatiba na institutional incompetence.
Wabunge wa kuteuliwa na hayati Dkt. John Magufuli, je, mnajua mandate yenu? Au mmekuwa spectators tu ndani ya chombo ambacho kinatakiwa kuwa custodian of democratic accountability? Kwa nini mnashindwa kabisa kuibana serikali? Mnajua kuwa mnachangia kwa namna ya moja kwa moja kuangamiza taifa? Hivi kweli, wakati watu wanalia na bei ya vyakula, kukosekana kwa huduma za afya, na ukosefu wa ajira, nyinyi mnaleta mijadala ya upuuzi bungeni kuhusu mavazi, udaku, na vijembe vya kipuuzi? Huu ni cognitive bankruptcy, ni aibu kwa taifa.
Watanzania hawajawachagua nyinyi mje kufanya political comedy. Tumewapa dhamana ya kulinda maslahi ya wananchi, siyo kuwa court jesters. Taifa linazama. Hali ya maisha ni mbaya. Umaskini unazidi kuongezeka. Lakini bunge, ambalo kwa mujibu wa Katiba ndilo the sovereign watchdog, limegeuka kuwa sehemu ya tatizo badala ya suluhisho. Sasa kama bunge halisimami, nani atasimama?
Hatutakubali tena kuwa watumwa wa mfumo unaolinda wachache na kuumiza wengi. Kama wabunge wameshindwa kazi yao, wakae pembeni. Kama hawawezi kuisimamia serikali, basi waondoke. This country deserves better. This republic demands integrity. Hatuwezi kuruhusu taifa liendelee kuongozwa na watu wasiojali wala kuwajibika.
Enough is enough. Time to rise. Time to speak truth to power.