BUNGE lililojaa MAHARAMIA

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
1,488
908
Labda tujenge hoja kwa kusema HIVII

HAZINA ni kama Roho ya kitu kinachojiita serikali. Ili serikali zote Duniani ziendeshwe lazima ziwe na mkoba wa vijisenti na masenti yao. Viongozi wenye dhamana kuziongoza serikali hizo hukodolea macho yao yote kwenye mkoba huo kuhakikisha kila senti inayotoka inatumika kwenye kusudio stahiki. Senti zote zinazokusanywa kutoka kwenye mapato ya ndani, kodi pamoja na wahisani hurundikwa kwenye Mkoba huu.. kutindikiwa kwa mkoba ni hatari kwa nchi na uongozi kwa ujumla.

Wizara ya fedha ndani ya nchi yetu ndiyo iliyokasmiwa kuratibu gawio la senti zitokazo kwenye mkoba huu na kutawanya kwenye wizara mbalimbali zenye mamlaka ya kutumia mapesa haya kihalali kwa mujibu wa sheria mbalimbali ambazo tumejitungia ikiwamo sheria za manunuzi (PPRA), sheria za matumizi na nyinginezo.

Wizara hizi Chini ya makatibu wakuu pamoja na mahasibu wao ndio wenye dhamana kuhakikisha mishiko hiyo wanayoipokea inatawanywa sawia kwenye umati wa Idara, wakala na kurugenzi zake ndani ya serikali kuu au serikali za mitaaa kutokana na mapendekezo ya idara hizo yaliyoainishwa kwenye dodoso la bajeti zao kwa vipindi vya robo mwaka au mwezi, Chini ya Waziri mwenye dhamana na wizara hiyo.

Idara hizi kwa umakini na kutegemea wataalam ilionao hutengeneza majarida mbalimbali kama procurement planning ambazo huchambua bajeti zao na matumizi yao kwa vipindi na vipindi. Umati wa wakala, idara au kurugenzi hizi zina wakaguzi wa ndani (internal Ouditors) ambao hukagua kuhakikisha kwamba senti hizi zilizotoka mkobani zimetumika kwenye lengo lililokusudiwa ili kuleta tija na maendeleo kwa mwananchi ..yaani wewe hapo..
BAADA ya mpito wa Muda katika mwaka husika wa fedha, mpekenyuzi mkuu wa hela hizi (CAG), nae huunda timu yake ambayo huzungukia Wizara na idara zake kupekenyua na kuchunguza bin kukagua mtitiriko wa pesa yote iliyotoka kwenye mkoba mkuu hazina na jinsi ilivyotumika kwa nani na wapi. Hata kama ulipanda baiskeli kwa kutumia fedha ya serikali lazima risiti ya nauli yako ionekane..
Baada ya Timu hizi kukagua matumizi ya fedha za kinachojiita serikali, hukusanya mapungufu, yaani fedha zote ambazo hazikutumika kihalali, zilizoyeyuka na walizokwiba viongozi wetu. Na mrundikano wa masent haya waliyokwiba ni mabilioni mengi sitaki hata kuyataja manake yamesomwa na wewe umesikia kama hujasikia shauli lako..
Pamoja na wizi na Ubadhirifu mkuu namna hii, bado serikali hiyo IPO, mawaziri ambao Uozo huu umefanyika kwenye mamlaka zao WAPO, wakuu wa wizara, wahasibu na watumishi wengine ambao wamehusika moja kwa moja na kukwiba huku WAPO na wanaendelea kula bata na nchi IPO tu inaendelea kuitwa Tanzania a.k.a Kituo cha amani(mapoyoyo)..
WANANCHI kupitia Bunge letu la ZOTOTO, tumeonekana kuanza kuamka sasa, kwamba kadhia hii, dharau hii, uonevu huu sasa lazima tuchukue hatua. Maskini ya Mungu wabunge wetu wachache wametutumka na kujivika jukumu la kutoangalia sura wala makunyanzi ya mtu bali haki ichukue mkondo wake.. wamethubutu kuiadabisha serikali kwa maslahi ya wananchi. Kwa kuanza hatua ya kuchora majina kama 70 na kisha kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na kiranja mkuu wa mawaziri na hatimae mawaziri wote na serikali hii. Hii ni hatua ya kusifia na itayofanya mawaziri hawa kujua kwamba Ofisi wanazopewa si kwa ajili ya kuchapa usingizi na kufanyia ufuska bali zina maadili na miiko ambayo wananchi wanayahitaji.
Cha ajabu na Cha Kushangaza sana, tena cha kusikitisha kwamba rundo kubwa la wabunge hawajasaini karatasi Hilo. Kha! hii inatisha sana..jambo hili nadhani si kwa maslahi ya chama Fulani bali ni kwa mtazamo wa kizalendo na kila mpenda haki. Na lazima wabunge hata mawazili akiwemo kaka yetu Pinda lazima waanguke saini zao kwa maslahi ya kuwajibika, hakuna mchawi hapo..
Kitendo cha baadhi ya wabunge kutokusaini karatasi hilo wananchi hatuzuiliki moja kwa moja kuwatafsiri ifuatavyo;
1. Wabunge hao ni maharamia, wezi na katili kwa wananchi wao
2. Wameridhia na kubariki wizi huo
3. Nao ni majambazi wamehusika na kukwiba

4. Lazima wananchi kwenye majimbo yetu hatusubiri 2015, tunaanza sasa kuwashinikiza wajiuzulu ubunge kwenye majimbo yetu tuwatafute tunaodhani watatufikisha 2015, mwizi ukimgundua husubiri kumpa muda aondoke mwenyewe ni kumtimua hapo hapo
5. Hawana utu, ni wauaji na wako kwa ajili ya matumbo yao, na tutaanza kuwapekua na kujua mali zao na zile walizozificha na kwa umoja wa wananchi tutawapokonya mali hizi na kuzirudisha serikalini.

KARATASI LA WABUNGE WALIOSAINI LICHAPISHWE VIZURI, WANANCHI TUWE NA NAKALA YA WATETEZI WETU WA KWELI, TUANZE KULITENDEA HAKI..
 
Natoa Tamko; wabunge ambao hamjasaini karatasi hiyo ni wasaliti.. na tunaanza kuwashughulikia kabla ya 2012 lazima mng'oke. tunatengeneza mtandao wa Kuwang'oa..
 
Mbunge wetu keshajipa tenda ya kujenga uwanja wa ndege.. Asee .. Kila tenda anajizungushia kwa makumi ya makampuni ambayo yeye mwenyewe anayaongoza kimugongomugongo.. Kitaeleweka muda si mrefu...
 
mawazo uliyonayo ni sahihi sana,mwizi hatakiwi kupewa muda wa kujiandaa laa! Bali ni kumvurumisha tu kabla ya kujiandaa,kwani wametuchosha,wametudharau,wametubeza sana sana,,,
 
Wakuu towachongee wote ambao hawasaini hata Kama ni mbunge wako Kama inawezekana CDM watengeneze vipeperushi vya kuwachongea kwa wananchi
 
Nina hasira!
Joseph Selasini (Mb.) anayewakilisha Rombo ametia sahihi yake kuunga mkono hii hoja? Majibu tafadhali kabla sijafanya maamuzi ya tofauti...
 
Cha ajabu na Cha Kushangaza sana, tena cha kusikitisha kwamba rundo kubwa la wabunge hawajasaini karatasi Hilo. . Wabunge hao ni maharamia, wezi na katili kwa wananchi wao.
2;Wameridhia na kubariki wizi 3.Nao ni majambazi wamehusika na kukwiba

Wanasema maana nyingine ya neno Parliament ni kundi la mabundi(source;etv africa). Nadhan hii ndio haswa inayofaa kwa bunge letu mana asilimia kubwa mule ni mabundi ukiondoa makamanda na wale wachache mfano wa kina Deo.
 
Wanasema maana ingine ya neno Parliament ni kundi la mabundi(source;etv-africa). Nadhan hii ndio maana inayofaa kwa bunge letu mana limejaa mabundi ukiondoa makamanda na wachache mfano wa Deo.
 
imagejpeg
 
Back
Top Bottom