BUNGE LIJALO LITAKUWA CHUNGU SANA KWA SERIKALI

Nchi imefikia pabaya.. Bora tuongozwe na jeshi tu kuliko kuona nchi inaaibika hivi. Hii sio aibu ya bashite na Rais ni aibu ya watanzania wote. Wabunge naamini watafanya kazi inayotakiwa kikao kijacho, nadhani serikali haijatambua nguvu ya mhimili wa bunge bado.

Jana tu tulikuwa tumeweka imani yetu kwa rais kuwa atafanya maamuzi ya busara kwa taifa...haikutokea, leo tunaweka imani kwa bunge...bunge lipi? Hili la ze-komedi (according to Jairo)?
 
Siku zote naombea bunge lijitambue lakini bado limekuwa mhuri wa serikali.

Hivyo likiamuaka nitampongeza Magufuli kwa kuwazibua masikio.
 
Kwa dalili zilizopo bunge lijalo litakuwa na umoja usiopata kuonekana!Nasikia waheshimiwa hawa wanaazimia kuikwamisha bajeti ya serikali bila kujali itikadi zao.

Ni suala la mda.Yetu macho.
Hata ikwamishwa, iliyopo inazingatiwa?
 
...bungeni hamna kitu.... wanafiki wa ccm hawawezi kukata mti waliokalia na matumbo yao.........

...sehemu pekee iliyobaki ya kudai haki kwa watanzania ni mahakama tu...ndio maana tumeomba sana watu kama Lissu wawe na uongozi kwa wanasheria ili angalau kusukuma agenda ya utawala wa sheria na haki.....ni mahakama tu imebaki....
 
Haa! Bunge kibogoyo wanasubiri kukaushwa mate 'one man show of leadership' Nitafurahi kuliona bunge liki ishauri serikali ipasavyo bila kuyumbishwa na mtu
 
Back
Top Bottom