Bunge letu ni aibu tupu!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,039
Uzembe huu aibu kwa Bunge
Tanzania Daima

OFISI ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imekiri uzembe katika utendaji wake wa kila siku.
Hili limethibitishwa na Spika mwenyewe, Samuel Sitta, katika moja ya habari za gazeti hili leo.

Uzembe huo umefanywa na sekretarieti ya Bunge hilo kwa kushindwa kumpa barua rasmi ya kumsimamisha kuhudhuria vikao vya Bunge, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA) kwa miezi mitano mfululizo.

Zitto, anatumikia adhabu hiyo tangu Agosti 14, mwaka huu, baada ya kudaiwa na wabunge wenzake kuwa alilidanganya Bunge kuhusu utiaji saini wa mkataba wa Buzwagi uliofanywa na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, jijini London Uingereza.

Kabla ya kufikiwa kwa uamuzi wa kumsimamisha, Zitto alilitaka Bunge kuunda kamati teule ya kuchunguza suala hilo huku akisisitiza kuwa mkataba huo ulisainiwa kinyume cha maagizo ya Rais Jakaya Kikwete kusitisha utiaji saini wa mikataba mipya.

Wakati Rais Kikwete anaagiza hilo, pia alitangaza kwamba kwa sasa serikali inadurusu mikataba ya madini iliyoingiwa awali.

Sote tunafahamu kuwa, adhabu iliyomkumba Zitto, ilitikisa nchi baada ya kambi ya upinzani kulifikisha hili mbele ya wananchi, wakiamini wao ndio wenye mamlaka ya kuchagua mchele na chuya.

Kwa maana hiyo basi, Sitta anakiri kuwa ndani ya Bunge tukufu kuna uzembe ambao kwa namna moja ama nyingine ameshindwa kuutafutia tiba.

Tunasema ameshindwa kwa kuwa alikiri hadharani kwamba uzembe wa sekretarieti umesababisha Zitto kutopewa barua rasmi kwa wakati, kinyume cha taratibu za kiofisi.

Ikumbukwe kuwa ni zaidi ya miezi miwili sasa tangu kusimamishwa kwa mbunge huyo.

Ni wazi kuwa adhabu hiyo inawanyima uwakilishi mzuri wapiga kura na wananchi wa Kigoma Kaskazini, tofauti na matarajio yao.

Lakini, msingi wa maoni yetu ni namna ambavyo Bunge linavyoshindwa kuwajibika kwa masuala ya msingi kama haya.

Inakuwaje ofisi nzito na moja ya mhimili wa utawala kushindwa kuandika barua ya kikazi isiyozidi dakika 45, bila sababu za msingi kuelezwa.

Kwa vipi tuuamini utendaji wa watumishi hao ilhali barua ya kumjulisha mhusika kuwa amesimamishwa kutokana na sababu ya kulidanganya Bunge inashindikana kuandikwa kwa zaidi ya miezi miwili sasa?

Tunaamini kuwa Spika ana uwezo wa kumwajibisha yeyote anayeshindwa kutimiza wajibu wake na kusababisha aibu ndani ya chombo hicho muhimu cha kutunga, kurekebisha na kupitisha sheria za nchi.

Nini maana ya uzembe huu? Nani wa kuwajibika iwapo Spika anakiri uzembe ndani ya Bunge huku akishindwa kubainisha hatua madhubuti atakazochukua kuhusu hili?

Tunalazimika kutilia shaka utendaji wa Sekretarieti ya Bunge letu na wote wanaohusika ndani yake.

Iwapo inashindikana kuandika barua, ni vipi katika masuala makubwa yenye masilahi kwa taifa yanayoamuliwa na wabunge?

Katika hili tunashawishika kuamini kwamba, uzembe unaofanywa na chombo kikubwa zaidi ndani ya Bunge unatokana na kufanya kazi kidugu, kulindana, kujuana au pengine kuogopana.

Tunasema chombo kikubwa kwa sababu, baada ya wabunge kufanya maamuzi ya jambo Fulani, kazi inabaki kwa sekretarieti kuliweka jambo lile katika maandishi na kulifikisha linapohusika.

Maana ya uzembe huu ni kwamba, yapo mambo mengine ambayo hayajatekelezwa kwa sababu za uzembe kama huu.

Tunafahamu uzembe kazini ni jambo linalorudisha nyuma maendeleo na wakati mwingine husababisha rushwa na wanyonge kunyimwa haki zao.

Huu ni urasimu unaopigwa vita kila kukicha. Hivyo basi, tunamtaka Spika kuliweka hili bayana, ili kuondoa ukakasi wa uzembe huu.

Udhaifu katika utendaji huondoa imani ya wananchi kwa viongozi wao na kushusha heshima ya Bunge.
 
Sidhani kama kutompa rasmi barua Mh Zitto ya kumsimamisha ubunge kwamba inatokana na uzembe!, kwamtazamo wangu sababu zilizo sababisha ni akti ya hizi zifuatazo:

-Kuchanganyikiwa baada ya wakata issues wakiwepo watu walio bobea kuonyesha wazi kwamba hiyo adhabu si sawa!

-Butwaa iliyo wapiga kutokana na muitikio wa wananchi kwa sakata lenyewe!

-Hofu ya kwamba wataweka vigezo gani ndani ya barua hiyo kuonyesha sababu za msingi/rasmi ya kumsimamisha, kwani kwa kufanya hivyo kwa sababu za juujuu ambazo tayali wanasheria na wanaharakati walisha onyesha udahifu wake watakuwa wanajifunga na kutoa kidhibiti muhimu kwa Zitto kuwapeleka mbele ya mahakama!

-Labda wamegundua walivo chemsha na pengine wanajipanga ili kuomba radhi kwa muhusika! (least likely)
 
Rwabugiri na wana JF kwa ujumla, naomba ufafanuzi kidogo katika hoja yako hapo juu.
Ina maana kutokana na suala hili la Zitto kutopewa barua rasmi ya kusimamishwa kuhudhuria vikao, ataendelea kuhudhuria vikao vya bunge hadi hapo atakapopewa barua rasmi?
 
Mtu Pori hapo hata mie natumbua yangu macho tu! Kinachoweza kuwaokoa na pengine kurudisha hadhi ya bunge ni ile sababu ya mwisho ambayo pia nina wasi wasi wa uwezekano wake kuwa mdogo kwa hali halisi ya viongozi wetu wasio kosea na wasio tayali kuomba msamaha ( nukuu Mkijiji)
 
Rwabugiri na wana JF kwa ujumla, naomba ufafanuzi kidogo katika hoja yako hapo juu.
Ina maana kutokana na suala hili la Zitto kutopewa barua rasmi ya kusimamishwa kuhudhuria vikao, ataendelea kuhudhuria vikao vya bunge hadi hapo atakapopewa barua rasmi?

Mwenyewe si uliona vile walijichanganya kujibu swali la kwa nini Zito kafukuzwa bungeni? Wamekosa cha kuandika kwenye barua!
 
hilo changa la macho tu!

utawala wa bunge haujaandika barua kwa kuwa wanashindwa na sababu za kuandika za kutoa adhabu hiyo, kwa vile wanajua watanzania hawajalala kuna siku wataitumia barua hiyo kuonyesha 'uhalifu' wa bunge hilo
 
Back
Top Bottom