Bunge letu lisipoangalia litapoteza heshima yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge letu lisipoangalia litapoteza heshima yake

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Anold, Feb 9, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Jana niliweza kufuatilia mjadala uliokuwa unaendelea bungeni, kimsingi Nidhamu iliyokuwa ikionyeshwa na baadhi ya wabunge na lugha ambazo walikuwa wanazitoa kwangu mimi zimenivunja moyo sana kutokana na heshima niliyoiweka kwa bunge letu na wabunge kwa ujumla. Bila kuficha mheshimiwa spika kama atakuwa anaruhusu mijadala ya bunge itawaliwe na lugha na mazingira kama ya jana basi sitashangaa kuona bunge letu likigeuka ukumbi wa masumbwi na hivyo kuondoa kabisa ile sifa inayosemwa kuwa tanzania ni kisiwa cha amani. Sikutegemea hata siku moja kuona lugha za mtaani zinatolewa na wabunge kwa uhuru kiasi kile, kiti cha spika sidhani kuwa kiliruhusu kupewa heshima yake kitu ambacho nimeona ni dosari kubwa na kipekee sitaki kuamini kuwa ile ni dharau kutokana na ukweli kuwa watanzania tuna ustaarabu wetu ambao ni tofauti kabisa na mabunge mengine. Niliochokiona jana ni uhasama na chuki za wazi kati ya wabunge na wabunge pia kati ya vyama vya upinzani hii ni dalili mbaya sana kwani kama mambo yataendelea vile basi watanzania tumekwisha. Nina imani kubwa na uwezo wa mheshimi spika ni wakati wake kuwadhihirishia watanzania kuwa anaweza!!! Watanzania hatutaki kusikia lugha za kejeli na dharau, tunachotaka ni lugha yenye suluhisho la matatizo yanayotukabili watanzania sio kejeli, vijembe na lugha za mipasho!!
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mimi naombea katiba mpya ije mapema ili 2015 tuwatoe hao wabunge wote HASA wa CCM hakuna lolote wanalofanya unafiki mtupu
   
 3. Gudlucky

  Gudlucky Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bunge si sehemu ya kwenda kuonesha umahili katika kuongea lugha za mitaani, na si sehemu pia ya kuonesha chuki baida ya wabunge na wabunge au chama cha siasa hiki na kile! Ni sehemu ya kupigania haki ya watanzania kwa lengo la kuwaunganisha watanzania wawe wamoja katika mstakabari mzima wa taifa lao, ikiwa ni pamoja na suala zima la amani na maendeleo yao! Hawakwenda kutuonesha umahili katika kulumbana! Napenda wajue kabisa watanzania HATUPENDI!
   
 4. ANKOJEI

  ANKOJEI JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  wapingane wasipingane, sisi tunataka amani na maendeleo.
  tunawaangalia tu,
  2015 wakumwagwa lazima wamwagwe tu!

  wa2 wanataka sifa bungeni eti ndio watoke 2015, ballot box will tell!
   
 5. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Bunge lilishapoteza heshima siku nyingi tu. By the way, are you really serious unaposema una imani kubwa na uwezo wa mheshimiwa spika? Cha jani kilikuwa kikao pili tu toka awe spika hali ndiyo hiyo. huyu mama hafai kabisa uwezo wake ni mdogo kupita kiasi. aliwekwa hapo kwa manufaa ya mafisadi ili wamtumie kama alivyofanya jana. kwa uwezo mdogo aliouonyesha jana nadhani hata kwenye mazingira ya bunge hastahili kuwepo.
   
 6. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sioni hata sababu ya kuendelea kuwaita wahuni hawa eti 'waheshimiwa.' wameshapoteza heshima hawa na hawapo bungeni kwa maslahi ya wananchi, bali maslahi binafsi.
   
 7. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,934
  Trophy Points: 280
  Mkuu nasikitika sana mie sasa nimechoshwa na kinywaji aina ya AMANI. Walau ulevi unaisha kichwani na sasa ni uwajibikaji na maendeleo kwa hali yoyote ile. Amani inatulaza gizani, njaa n.k.
   
 8. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hakuna amani kwenye umasikini....................
   
 9. Engager

  Engager JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  "TANZANIA" kuna umhim wa kutawaliwa tena.
   
 10. Gudlucky

  Gudlucky Member

  #10
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amani Haiji kwa kutafuta njia za kuhalalisha ufisadi katika mali za watanzania wala kuchakachua mali ya watanzania, Amani inakuja kwa kutenda Haki inayoambatana na uwajibikaji katika kuwatumikia watanzania katika hali ya uadilifu na uaminifu! SASA watanzania tunataka HAKI, UKWELI na UWAZI, UAMINIFU na UADILIFU ikiwa ni mapoja Na UWAJIBIKAJI unaozaa MATUNDA si kwa wabunge bali matunda kwa WATANZANIA na TAIFA lao kwa ujumla! Unajua inavyoonekana sasa kaili mbiu ya kikwete inatupa upofu, Ukweli ni kwamba Maisha bora kwa kila mtanzania yamekuwa ni MAISHA BORA KWA WABUNGE WA CCM na UMASIKINI kwa WATANZANIA! ACHENI KUTUFANYA sisi VIPOFU!!!!
   
Loading...