Bunge letu lioneshe uzalendo na wateule wote kubana matumizi tujitegemee

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,610
13,160
Kufuatia ushindi wa kishindo na mtazamo wadau wa maendeleo, natarajia Wabunge wetu na wateule wa Rais kuonesha uzalendo kwa kukubali kupokea robo mshahara na akiba iende kusaidia pengo kufuatia vitisho wadau wa maendeleo.

Angalizo kwa Mpango mtaani kugumu sana asifikirie kutuongezea kodi.

Maendeleo hayana chama.
 
Wala hakuna cha uzalendo. Wakibanwa vizuri hata hiyo robo hawataiona.
Kupanga ni kuchagua, tumechagua sifa ya kishindo dhidi ya kuharibu democrasia umoja na ustawi wa taifa letu wacha tusugue vichwa...." we Mupango sikuerewi nataka hera zipatikane..."
 
Naunga mkono wabunge waondolewe posho na maslai , walale hostel, wale bungeni ili kuokoa pesa zikatumike kujenga nchi maana mabeberu wamedhamiria kukata kufuta misaada. Wabunge 375 laki 3 kwa siku mara wiki ni zaidi ya milioni 400 hizi zinapotea bure, nao wabane matumizi Hadi tukiwa dona kantri ndo wapewe nyingi
 
Soon watumishi wataanza kukopwa mishahara nawashauri wajifunze kujiajiri hata kulima mchicha tuendako sipo. Mabeberu yamedhamiria kumpiga Mpenda ligi kotekote. TIN namba kikokotoo kianze na mapolisi na wakurugenzi wa tume
 
Siasa ni ajira kwa Tanzania.

magufuli ametuharibia sana ustawi wa Taifa Tunu za taifa zinazikwa kwa nguvu zote.

MKAPA ALILETA MTU WA HOVYO SANA.
 
Hahaha waongeze wabunge wa viti maalum kwanza.

Halafu wapikiwe ugali bungeni wawe wanakula hapo hapo badala ya kwenda kula migahawani.

Breakfast wapewe uji na miogo
 
Naunga mkono wabunge waondolewe posho na maslai , walale hostel, wale bungeni ili kuokoa pesa zikatumike kujenga nchi maana mabeberu wamedhamiria kukata kufuta misaada. Wabunge 375 laki 3 kwa siku mara wiki ni zaidi ya milioni 400 hizi zinapotea bure, nao wabane matumizi Hadi tukiwa dona kantri ndo wapewe nyingi
Mkuu akifufua bunge aliwaambia" wabunge ni wakat wao kuwa mabilionea "natamani nao wavae ndala na meno yao yachakae kwa kukosa hela za posho "
 
Naunga mkono wabunge waondolewe posho na maslai , walale hostel, wale bungeni ili kuokoa pesa zikatumike kujenga nchi maana mabeberu wamedhamiria kukata kufuta misaada. Wabunge 375 laki 3 kwa siku mara wiki ni zaidi ya milioni 400 hizi zinapotea bure, nao wabane matumizi Hadi tukiwa dona kantri ndo wapewe nyingi
Pia mishahara punguza mpaka ml 5 gross salary, tunaijenga nchi kwanza wote tuumie..
 
Back
Top Bottom