Hoja nzuri lakini presenter anakosa focus. Issue ni kuwa hawana sifa au ni wakatoliki. Maana siamini kama wote waliochukuliwa ni wakatoliki kwani St. Augustine inachukua watu wa dini zote. Pia siamini kama watu wenye sifa wapo St. Augustine tu.
Inawezekana pale wakubwa walikuwa na mtu wao wakaona wachukue watu wote wa chuo kimoja ili kupoteza ushahidi lakini pia macho ya kifisadi hayaoni. Ushahidi unaonesha mafisadi mara nyingi hawajui kusoma alama za nyakati.
Ninaamini kuwa kama ofisi ya umma ilitakiwa kuchukua watu wa vyuo vingi zaidi ili kuweka diversity ya watumishi wake. Ukiweka watu wote wanatoka chuo kimoja kwa mtazamo wangu naona si sahihi.
Hoja ya kandanda kuhusu wakatoliki sikubaliani nayo hata kidogo.Kwanza mimi ni mluteri lakini sijawahi kugundua kuwa tunaonewa. Malalamiko haya nimeyasikia mara ya kwanza pale Lowassa alipojiuzuru akapokelewa kwao Monduli kwa shangwe na mmoja wa watu maarufu alikuwa Askofu Laizer wa Arusha. Baada ya hapo Lowassa alisafiri kwenda Israel kwa ziara ya kidini na mhubiri maarufu Mr Mwakasege ambaye by default nae ni mluteri. Baada ya hapo ikaonekana kuwa waluteri wanamuunga mkono Lowassa na pia wanahisi kuwa wanaonewa.
Lakini hizi ni hisia tu,sidhani kama kuna ukweli wowote. Ukiangalia kwenye nchi yetu,wakristo wa kikatoliki ndiyo wengi zaidi kuliko wakristo wengine. Kielimu pia hawako nyuma sana kwani maeneo ambayo wamisionari wa kikatoliki walifika hapo zamani walijenga mashule.
Suala la Malecela linajulikana,kama hujui leta maswali watu watakujibu. Nadhani hujui sababu kwanini Mwalimu alitishia kurudisha kadi ya CCM. Tatizo halikuwa dini(uanglikana). Kuthibitisha hilo kabla ya hapo Mwalimu alipong'atuka alimuachia madaraka Mzee Mwinyi ambaye ni muislam wakati walikuwepo wakatoliki wengi sana kipindi hicho ambao walikuwa na uwezo kama/zaidi ya mzee mwinyi.
Mwisho, naomba nitoe wito kwa watanzania,tunaposhindwa mambo tusilete chokochoko za udini kwani ukweli tunaujua. nchini kwetu waislam na wakristo wanaishi nyumba moja wanalala pamoja, wanafanya kazi ofisi bila kutengana. Utajua huyu muislam au mkristo inapofika wakati kila mtu anaenda kwenye ibada.
Asante