Bunge laelekea kumuelemea Spika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge laelekea kumuelemea Spika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Feedback, Jun 21, 2011.

 1. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  • Asema mwenendo wa wabunge si mzuri
  • Umepotezea Bunge mvuto kutokana na vituko
  Katika kile kinachoonekana kuwa Spika wa Bunge, Anne Makinda, ama kazidiwa au kuchoshwa na mwenendo wa wabunge katika kuliongoza Bunge, ameendelea kutoa kauli za kuwaonya kwamba wanaidhalilisha taasisi hiyo kiasi kwamba imepoteza mvuto kwa wananchi. Kauli ya Makinda aliyoitoa jana, inafanana na ile aliyotoa Jumatano iliyopita akilalamikia jambo hilo, kiasi cha kujikuta akiingia katika mgogoro wa wakazi wa Kariakoo baada ya kuwafananisha wabunge na watu wa Kariakoo. Jana, alieleza kukerwa kwake na mwenendo wa wabunge akisema kitendo cha baadhi yao kuongea bila utaratibu pindi mmoja wao anapokuwa anachangia hoja katika mjadala kuhusu bajeti ya serikali, kimeharibu taswira nzuri ya Bunge kwa watu wanaofuatilia shughuli zake.

  Makinda alisema hayo wakati akimkaribisha Mbunge wa Dole (CCM), Sylvester Mabumba, kuongoza mjadala wa wabunge kuhusu bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, baada ya yeye (Spika Makinda) kubanwa na shughuli nje ya ukumbi wa Bunge. Alisema hivi sasa taswira ya Bunge imekuwa si nzuri kwa watu wanaofuatilia shughuli zake kutokana na baadhi ya wabunge kuongea bungeni bila kufuata utaratibu. Spika Makinda alisema kitendo hicho kimekuwa kikisababisha kero kwa watu na hivyo kushindwa kufuatilia shughuli za Bunge.

  “Napigiwa simu nyingi na kuandikiwa ujumbe, image (taswira) yetu mbele ya jamii siyo nzuri. Kuongea bila utaratibu tunatumia muda, ambao wachangiaji wangekuwa wengi,” alisema Spika Makinda. Aliongeza: “Jamani tuendelee kukua, tusiendelee kuwa kero kwa watu. Walikuwa wanapenda sana kuangalia sana kipindi hiki, lakini sasa wengine wanakereka sana kwa tabia zetu. Kwa hiyo tubadilike, muwe watu waheshimiwa kama tunavyoheshimiwa na watu waliotuchagua.”

  Kauli ya Jumatano iliyopita aliyoitoa wakati akitoa matangazo na ufafanuzi wa masuala mbalimbali bungeni akieleza kusikitishwa kwake na mwenendo wa wabunge ndani ya Bunge kwa kufanya mambo kinyume cha kanuni zinazokubalika, alifananisha hali hiyo na kama watu wako Kariakoo. Awali Makinda alisema kuwa alichokuwa amefanya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Rasmi Bungeni, Freeman Mbowe, kwa kutaka mwongozo wa Spika baada ya kupata majibu yasiyoridhisha kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, alikuwa sahihi na si kama wanavyofanya wabunge wengine wanaopiga tu kelele za kuomba mwongozo wa Spika wakati mzungumzaji akiwa bado anaendelea kuzungumza kama wako Kariakoo. Makinda alisema kimsingi, mwongozo wa Spika unaomwa mara tu baada ya tukio husika kumalizika ndani ya Bunge, kama ambavyo alikuwa amefanya Mbowe.

  Ni katika muktadha huo, Spika aliwataka wabunge kuacha kufanya mambo ya ovyo wanapokuwa katika vikao vya Bunge kwani wanatia aibu kwa watu wanaowatazama na wameligeuza Bunge kama Kariakoo. Vile vile, aliwaasa wasome vizuri bajeti ili watakapochangia wachangie vitu vya msingi badala ya kuzungumza mambo yasiyohusu bajeti. Alisema alisikitishwa na hali iliyotokea Jumanne wiki iliyopita katika kikao cha jioni kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge, George Simbachawene. Alisema katika kikao hicho wabunge walifanya vituko vya ajabu kiasi cha yeye (Makinda), kushindwa kuendelea kuangalia mwenendo wa kikao hicho.

  “Hii ni aibu kubwa na sijui kwa nini mnajidharaulisha kwa wananchi, mnajua watu huko nje wanawaheshimu sana, sasa mkifanya mambo ya ovyo wanawadharau na mjue haya yote yanayofanyika humu yanaonekana, mimi mwenyewe nilikuwa naangalia, lakini nikashindwa kuendelea kwani nilikuwa naona vitu vya ajabu ajabu,” alisema Makinda na kuongeza kuwa:
  “Hapa bungeni kuna utaratibu wa kuzungumza, mtu akiwa anazungumza wengine mnapaswa kumsikiliza, lakini jana (Juzi) mtu mmoja anachangia na wengine wanazungumza utadhani mko Kariakoo.”

  Katika kikao kilichoongozwa na Simbachawene, wabunge walikuwa wakiwasha vipaza sauti vyao na kutoa maneno ya vijembe kwa wenzao na wengine wakizomea wachangiaji. Hali hiyo ilimpa wakati mgumu Simbachawene, ambaye alikuwa akilazimika kuwakatisha wabunge waliokuwa wakiomba mwongozo ili kuwabana wazungumzaji walioonekana kuwakejeli wengine.

  “ Waheshimiwa wabunge tutumie muda wetu kujadili huu mpango ulio mbele yetu, nikiruhusu kila mtu asimame atoe mwongozo muda wote tutakuwa tumeupoteza bure, naomba tuwe makini,” alisema Spika Makinda. Baada ya kurusha kombora kwa watu wa Kariakoo, mchana Makinda alilazimika kuomba radhi kutokana na tafsiri iliyoonekana kuwakera baadhi yao. Kauli kwamba wabunge wasizungumze kama wako Kariakoo ilionekana kuwakera baadhi ya watu waliomtumia ujumbe wakimweleza kuwa amewadhalilisha na kwa kuonyesha kuwa eneo hilo halina maana.

  “Nawaomba radhi waliokwazika na kauli yangu, lakini sikumaanisha kuwadharau watu wa Kariakoo, nilichokuwa na sema ni kwamba watu watofautishe kati ya kuzungumza bungeni na mitaani, hapa bungeni kuna taratibu zake za kuzungumza, mtu mmoja akizungumza wengine mnapaswa kumsikiliza tofauti na sehemu kama sokoni Kariakoo ambapo mtu mmoja anaweza kuwa anazungumza na wengine wanazungumza wakati huo huo.

  Ijumaa iliyopita, wakati wa kuchangia bajeti, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), alijikuta katika wakati mgumu kwa kukatishwa kuzungumza na Mwenyekiti, Jenista Mhagama. Kwanza alimtaka kufuta kauli yake kuwa serikali inaua watu akitolea mfano mauaji ya watu watano katika mgodi wa North Mara na ya watu watatu waliouawa mjini Arusha wakati wa maandamano ya Chadema Januari 5, mwaka huu. Safari ya pili alimkatiza akimwekekeza kuwa kanuni za Bunge zinakataza kuwataja wabunge wengine kwa majina na badala yake azungumze na kiti. Alisisitiza kwamba utamaduni na kanuni za Bunge zinataka mzungumzaji yeyote kuzungumza na kiti na si kujibishana na mbunge mwingine au waziri.

  Baada ya maelekezo hayo Msigwa aliendelea kuchangia hoja bajeti, na alipomaliza alisimama Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher ole Sendeka, akitaka Mwenyekiti asaidia kuwasilishwa kwa maelekezo kwa wabunge juu ya maadili ya kuzungumza bungeni kwa kuwa Msigwa alikuwa ameongea maneno ya kuudhi kwa kuifananisha serikali ya Tanzania tangu uhuru sawa na mtoto wa miaka miwili anayelialia tu.
  Sendeka alisema kuwa Tanzania imekuwa na wasomi bora na mabingwa, wako katika nchi mbalimbali duniani, wanaongoza taasisi kubwa duniani kama Umoja wa Mataifa na kwingineko; imekuwa na marais watatu, akiwamo Mwalimu Nyerere ambaye anahesimiwa duniani; Rais Ali Hassan Mwinyi. Rais Benjamin Mkapa na sasa Rais Jakaya Kikwete. Alisema serikali zote hizo zimefanya kazi vizuri, zinaaminika na kuheshimiwa na mataifa yote duniani.

  Kwa maana hiyo, alisema hata kuwako kwa Msigwa ndani ya Bunge ni mafanikio ya serikali hizo, kwa maana hiyo kuifananisha na mtoto wa miaka miwili ni maneno ya kuudhi. Alimtaka Mwenyekiti Mhagama kutoa mwongozo ama kwa kumshauri spika atoe mwongozo kwa wabunge jinsi ya kuzungumza kwa wabunge bungeni na jinsi ya kuhesimu serikali yao. Mhagama alikubaliana na Sendeka na kusema kuwa atawasiliana na Spka ili aone kama anaweza kufanya nini ikiwa ni pamoja na uwezekano kurekebisha kanuni za Bunge.

  Kabla suala hilo halijapo, aliibika Waziri wa Nchi, Ofisi Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi, kumwomba mwenyekiti wa bunge amtake mbunge huyo athibitishe kauli yake juu ya Waziri Mkuu kwenda na ndege mbili Iringa na magari 50. Kabla ya kutoa uamuzi, Mhagama alimweleza Msigwa athibitishe madai yake au ayafute. Katika mtafaruku huo ndani ya Bunge, Kambi ya Upinzani Rasmi Bungeni kupitia kwa Mnadhimu Mkuu, Tundu Lissu, Ijumaa iliyopita ilitangaza kwamba itamshitaki Makinda katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanunu za Bunge, kwa madai kuwa anapindisha kanuni kwa kuwapendelea mawaziri na wabunge wa CCM na kuwakandamiza wapinzani.

  Kambi ya Upinzani Rasmi inaundwa na wabunge wa Chadema. Jana NIPASHE ilifuatilia malalamiko ya Upinzani kama yamefikia wapi, lakini John Joel, Kaimu Katibu wa Bunge, alisema kuwa Upinzani haujawasilisha malalamiko yao dhidi ya Spika. Wakati hayo yanajiri, leo wabunge wanatarajiwa kupitisha bajeti ya serikali iliyowasilishwa Juni 8, mwaka huu na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo. Kulingana na mwenendo wa uchangiaji wa mjadala wa bajeti, huenda wabunge wa upinzani wataibana serikali kuhusiana na mambo kadhaa, kubwa likiwa ni suala la kutaka posho za wabunge kuhudhuria vikao zifutwe.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Makinda anatakiwa akiri kitu kimoja tu - kwamba KANUNI za bunge sio 'holy grail' kwamba hakuna mtu yoyote anayejuwa au kuelewa ni nini kilichoandikwa kwenye kanuni za bunge na hivyo mapungufu yanayotekea wakati wa vikao ni kwa sababu ya kutojua kanuni.

  Kwa waliopata bahati ya kusoma hizo kanuni - ni very simple list ya dos and donts. very simple. Shida Mama Makinda aliyekulia bungeni amekuwa anasoma hizo kanuni (a) in isolation kwamba kila kifungu kinajitegemea wakati vifungu (kisheria) vinasomwa multiple kwa pamoja to give full meaning, na (b) Mama Makinda amekuwa pia anasoma kanuni bila kuowanisha (disregard) na sheria mama -yaani katiba ya nchi.

  Na hapa ndipo ccm na Mama Makinda wote kwa pamoja inabidi wavune walichopanda. CCM waliamua ku-mpa uspika bila kuangalia ni matatizo gani wanatakiwa kutatua au niseme ni challenges gani zilikuwa zinawanyemelea. Similarly, Mama Makinda alikubali kubeba mzigo wa kiti cha u-spika bila kujua ndani ya mzigo huo kuna misumari au unga au nini hasa.

  Hivi both CCM na Makinda, hawakujuwa kuwa CHADEMA ina wabunge wengi wanasheria wanaojuwa kusoma sheria -the way it should be read? Hivi hawakujuwa wabunge wengi wa CHADEMA ni wanaharakati na kwenda kwao bungeni walikuwa wamechoshwa na ubabaishaji kwenye chombo cha kutunga sheria? Hivi hawakujua zama hizi za science & technology ni vigumu kwa kiongozi kuficha au kupindisha mambo na wananchi wakakaa kimya? Matokeo yake Mama Makinda anaanza kujificha chini ya kivuli cha u-pya wa baadhi ya wabunge, na kejeli kuwa watu hawaelewi kanuni. Na wabunge wa ccm nao wamekuwa kama mateka -aibu tupu kwa ccm.
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Duh..............
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,164
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Kuyumba kwa chombo kunatokana na udhaifu wa Dereva. Hivyo yeye ndiye anayelipotezea taswira nzuri bunge kwani hajui anachokifanya. Anadhani kazi yake ni kukingia kifua serikali, asisiangizie wabunge, yeye ameshajiangalia.
   
 5. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Kinanishangaza kitu kimoja juu ya wabunge wa CCM, hawatoi michango ya maana na wenzao wa vyama pinzani wakitoa michango wao wanaibuka na taarifa au mwongozo (wamefanywa mbumbumbu na serikali yetu).

  Hivi wako wapi wale wapambanaji wa CCM wa Bunge lililopita? Watu kama Mwakyembe, Ole Sendeka, Selelii, Injinia Stella, Anna Killango, Shelukindo etc.
   
 6. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  wabunge wavivu wa kusoma watachangia nini bungeni! wanapewa bajeti hawaisomi matokeo yake kila mbunge wa ccm akisimama anaanza kumpongeza JK, Bilali, Pinda na Makinda! Kwani nani hajui kwamba Jk ni raisi au makinda ni spika? hawachanii hoja za msingi kazi ni kusema serikali ya ccm! serikali ya ccm! Tunajua ni serikali ya ccm hatuitaji kukumbushwa, changieni hoja zilizopo mbele yenu hatuitaji pongezi sisi
   
 7. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ole Sendeka, Stella Manyanya na Anna Killango, hawakuwa wapambanaji ila waganga njaa tu. Acha kuwapandisha chati hao.
   
 8. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni ukilaza. na yeye anafanya kazi kama remote control. Mkulu hayupo ndo maana hawezi kufamy maamuzi kama spika!!
   
 9. Mpenda Kwao

  Mpenda Kwao Senior Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 29, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi kwanini tusiwe na speaker kivuli kutoka kambi ya upinzani ambaye atakuwa anatathmini utendaji wa Speaker wa CCM?


   
 10. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,428
  Trophy Points: 280
  akitaka kulimudu hilo genge asahau matakwa ya waliyomuweka hapo awatumikie watanzania.. its that simple!
   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  Na bado ataona rangi zote za upinde wa mvua katika bunge la miaka hii mitano.
   
 12. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Mama Makinda amepatwa na ugonjwa wa JK (Kikweteism) wa kulalamika alamika ovyo. Wewe umepewa kuongoza bunge na kanuni ziko wazi kwa nini uanze tena kulalamika kila wakati. Kama mambo unaona ni magumu achia ngazi tu, kila mtu atakusifu, kuliko kung'ang'ania kiti kinachokuzidi uzito. Malalamiko ya JK yanatosha, sasa tukiongeza na ya kwako Doh!!!!!!! Tutafika kweli?
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,133
  Trophy Points: 280
  Bora ameliona hilo, bunge limekuwa ni mzigo mzito sana kwake.
   
 14. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  yeye hatimizi ule msemo 'mix with yours'!! amewekwa kutetea mafisadi na kukandamiza wanaharakati so hachanganyi na za kwake na kugundua mziki wa CDM ni mnene!!!
   
 15. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  yeye pia anajidhalilisha kutwa nzima kuzunguka na vivulana vidogo kona zote za dodoma
   
 16. G

  Galula Jr Member

  #16
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sidhani kama linaelekea ila limemshinda
   
 17. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Mbaya zaidi naibu wake naye bomu....inabidi wawepo manaibu wawili wa upinzani na magamba
   
 18. W

  We know next JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana kabisa na thread hii, lakini sikubaliani na mtazamo wa spika kuwa wabunge wenyewe ndio wanafanya mambo ya kulidhalilisha Bunge.

  Mytake:

  1. Ukiwa kama Kiranja, mahali popote pale, awe ni monitor darasani, koplo jeshini au hata Mwalimu Darasani, ukiona watu unaowasimamia wanafanya mambo hovyohovyo, basi ujue kuwa tatizo si watu ni wewe kiongozi;

  2. Mimi nadhani, Bunge linaboa si kwa ajili ya makelele bali ni kwa watu kupoteza muda mwingi kuongea vitu ambavyo havina mvuto kwa wananchi, au kuongea vitu kama vijembe wa kambi nyingine. Wananchi wanataka mjadala mkali wa mambo na si kupoteza mda kuwashukuru wapiga kura wako, kumshukuru Rais kwa Dira ya maendeleo, kumshukuru Waziri wa fedha kwa Budget, kuwashukuru wabunge wenzako, kuwashukuru familia yako, kuwashukuru na wapambe wako...hii yote ni nonsense. Nadhani wa kumshukuru ni Mwenyezi Mungu tu kwa uhai aliokupa kuwa pale Bungeni, then anza kuwawakilisha wanachi kwa hoja zenye mantiki. Bungeni ni mahala pa kuwawakilisha wananchi wote kwa ujumla wao, na si kukiwakilisha chama au kundi fulani. Ikiwa kama kweli wabunge watajadili mambo kwa faida ya watanzania wote..nadhani Serikali itakuwa na kazi ya ziada kufanya kazi kwa manufaa ya Watanzania wote.

  3. Ikiwa kama hilo la pili halitaangaliwa vyema, basi Bunge linaishia kubaya.. na muda si mrefu tutaachana nalo!
   
 19. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  unapoingia kwenye taasisi nyeti na ngumu kama bunge kwa minthari ya kutetea kambi fulani, tena ambayo haina maslahi ya taifa, lazima utagota ukutani. hizi ni dalili za kuanza kuishiwa stamina manake amekuwa anapambana kwa nguvu mkubwa kuliko uwezo wake. pole pole stamina itamwisha na atazidi kupayuka na kuropoka mpaka sasa atakuwa kituko na kichekesho kwa jamii nzima. tusubiri katuni zitakavyoanza kumchora! Bahati mbaya sana ni mwanamke, manake kwa wengine tutajitahidi kumheshimu kwa vile tu ni mmoja wa mama zetu. kama angekuwa mwanaume, naamini tayari angeshakuwa kikaragosi kwenye jamii hii! lakini ka'kawa lakuvunda halisikii ubani...engine itachemsha sasa hivi. nakuhurumia sana mama makinda. umeecha choo cha....
   
 20. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Laelekea kumuelemea au Tayari limeshamuelemea. Akiacha itakadi ya kachama ataliongoza bunge.
   
Loading...