Bunge laahirishwa ili wabunge warekebishe mambo yao ikiwemo makazi. Rais Magufuli kulihutubia Ijumaa Novemba 13, 2020

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Spika wa Bunge kahairisha Bunge sababu wabunge wengi wanataka kuongea na wapiga kura wao , wengine wanataka kununua nguo lakini wengine hawajapata bado sehemu za kulala...hivyo Bunge limeahirishwa mpaka kesho saa tatu asubuhi.
===

NDUGAI: Waheshimiwa wabunge najua mmewasili kwenye siku kadhaa sasa lakini baada ya kuapa tu hapa, sasa mambo yote tutarekebisha yanayohusiana na utaratibu. Pia natambua kuwa waheshimiwa wabunge mnao wageni wengi, mnayo mambo mengi ya kurekebisha hapa mjini.

Wengine bado mambo ya makazi hayajakaa sawasawa, wengine simu za wajumbe bado nyingi sana...... Wajumbe bado wanafatilia, lazima upate muda wa kuwasiliana na wajumbe. Wabunge ni watu wenye shughuli nyingi sana kwa hiyo tumeona mchana wa leo tuwaachie muwe huru mrekebishe mambo yenu ili tuweze kukutana kesho saa tatu kwa shughuli za kesho kwa maana hiyo naahirisha shughuli za bunge mpaka kesho saa tatu.

Pia mapema Ndugai aliwakumbusha wabunge desturi ya bunge linapoanza baada ya kutoka kwenye uchaguzi, hotuba ya Rais kuhutubia bunge. Amewataka kuwahi mapema Ijumaa asubuhi kwa ajili ya kumsikiliza.
 
Hakuna KAZI bora na inayolipa Kama UBUNGE.....

Hizi kazi Nyingine za SERIKALI...
Unapopangiwa kituo cha KAZI ni lazima URIPOTI haraka iwezekanavyo(wabunge wameripoti pia).

Hizi kazi zetu za SERIKALI unaporipoti na kuanza KAZI basi jua ya kuwa NYUMBA ni juu yako(kwa baadhi). Pia Wabunge wetu, suala la nyumba ni juu yao ila sijajua tu kama POSHO YA SIKU wanapewa baada ya wiki ama MWEZI tokea waanze KAZI.....

Hakika UBUNGE ni Raha humu AFRIKA....

Nami inshaalah kabla sijafikisha 40yrs nitajitahidi kuwaomba WAJUMBE wanipitishe huko JIMBONI kwangu ili nimtoe MBUNGE WA SASA na nikae mimi KUFAIDI hizo PRIVILEGES lulu..😂😂
 
Hakuna KAZI bora na inayolipa Kama UBUNGE.....

Hizi kazi Nyingine za SERIKALI...
Unapopangiwa kituo cha KAZI ni lazima URIPOTI haraka iwezekanavyo(wabunge wameripoti pia).

Hizi kazi zetu za SERIKALI unaporipoti na kuanza KAZI basi jua ya kuwa NYUMBA ni juu yako(kwa baadhi).Pia Wabunge wetu,suala la nyumba ni juu yao ila sijajua tu kama POSHO YA SIKU wanapewa baada ya wiki ama MWEZI tokea waanze KAZI.....

Hakika UBUNGE ni Raha humu AFRIKA....

Nami inshaalah kabla sijafikisha 40yrs nitajitahidi kuwaomba WAJUMBE wanipitishe huko JIMBONI kwangu ili nimtoe MBUNGE WA SASA na nikae mimi KUFAIDI hizo PRIVILEGES lulu..😂😂
Tamaa mbele mauti nyuma!
 
Tamaa mbele mauti nyuma !
Tamaa ndio ASILI YA BINADAMU....

Nilitamani kuwa msomi, nikasoma..
Nilitamani kuoa, nikaoa....

Na leo asubuhi nimetamani kunywa SUPU ya KUKU ila bahati mbaya mfukoni nimeamka majalala, nimemuachia mwenzangu BUKU 2 Kama mkubwa wa MEZA....

Kwa tamaa yangu halali, ninaamini nitaweza kuinywa KESHOKUTWA ama MTONDOGOO baada ya hawa wapangaji wa hiki KIBANDA kunilipa...
 
Rais wa Tanzania, John Magufuli atalihutubia Bunge la 12 Ijumaa Novemba 13, 2020 huku wabunge ambao wapo nje ya Dodoma wakitakiwa kurejea jijini humo.

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameeleza hayo bungeni leo Jumatano Novemba 11, 2020 wakati akitoa taarifa kwa wabunge kabla kuanza kwa shughuli za kikao cha pili.

Ndugai amesema kila mkutano wa kwanza wa Bunge jipya rais anahutubia ili kuweka dira ya Serikali kwa miaka mitano inayokuja na utekelezaji wa ilani kadiri anavyoona inafaa.

Amesema kwa kuwa hutuba hiyo ni muhimu amewataka wabunge ambao wana mpango wa kusafiri nje ya Dodoma kuahirisha safari zao.

“Hata wale ambao wapo nje ya Dodoma wanatakiwa kurejea ili kusikiliza hutuba hiyo. Sisi wabunge saa tatu kamili tuwe ndani ya ukumbi huu, tunaomba sana kuwahi kufika nikisema saa tatu kamili uwe kwenye kitu ni kwamba uwasili saa mbili. Siku hiyo tutakuwa na wageni wengi, kutakuwa na gwaride hapo nje,” amesema Ndugai.

Chanzo: Mwananchi
 
Kina Lema wakiona hivi wanatamani kulia na kuamua kukimbilia tu Kenya
 
Back
Top Bottom