Bunge la Tanzania ni mafichoni kwa mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la Tanzania ni mafichoni kwa mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 13, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  Spika azima hoja binafsi

  na Charles Mullinda, Dodoma
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu​

  SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, jana alizuia kuwasilishwa bungeni kwa hoja binafsi tatu zilizokuwa zimewasilishwa kwake na wabunge.

  Spika Sitta alitangaza uamuzi wake wa kuzuia kuwasilishwa kwa hoja hizo wakati akitoa matangazo bungeni baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.

  Aidha, Spika Sitta pia alizuia kusomwa kwa taarifa ya serikali kuhusu mgodi wa Kiwira kwa kile alichoeleza kuwa yapo masuala yaliyowasilishwa na Kamati ya Nishati na Madini ambayo serikali inahitaji muda wa kuyajibu kabla ya kuileta hoja hiyo bungeni kujadiliwa.


  Hoja binafsi zilizozuiliwa ni pamoja na iliyowasilishwa na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF) akitaka kuwepo kwa mabadiliko ya vifungu katika katiba, vitakavyoweka ukomo wa ukubwa wa serikali.

  Akitoa sababu za kuizuia hoja hiyo, Sitta alisema haiwezi kujadiliwa kwa vile inaingiliana na marekebisho ya Katiba.

  Alisema Ibara 98 ya Katiba inaeleza kuwa jambo kama hilo, linahitaji kushughulikiwa kwa kuwasilisha muswada bungeni na si kuwasilishwa na mbunge mmoja kama hoja binafsi.

  Hoja nyingine ni ile iliyowasilishwa kwake na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa, iliyokuwa ikitaka maelezo ya serikali kuhusu madai ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha, kuingilia mchakato wa utengenezaji wa vitambulisho vya taifa kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Serikali.

  Alisema baada ya kuipeleka hoja katika Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ambako ilijadiliwa na yeye kupewa ushauri, amekubaliana na ushauri wa kamati hiyo kuwa litakuwa jambo la busara mchakato wa zabuni hiyo kuendelea, kwani umekwisha kuchelewa.


  Alisema baada ya mchakato huo kukamilika na kama kutakuwa na malalamiko kuhusu zabuni hiyo ilivyoendeshwa, jambo hilo linaweza kurejeshwa bungeni na kujadiliwa ili kuona ni nani alikosea.

  Hoja ya tatu iliyozuiliwa na Spika Sitta ni ile iliyowasilishwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee (CHADEMA) iliyohusu mgogoro katika eneo la Chasimba, mkoani Dar es Salaam.

  Spika Sita alieleza kuwa ameridhika kuwa shauri hilo liko mahakamani hivyo haliwezi kujadiliwa bungeni.

  Kabla ya kutangaza kuzuiwa kwa hoja hizo, Spika alisema Mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi (CCM), aliondoa mwenyewe hoja yake iliyohusu uwajibikaji wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika halmashauri, baada ya kushauriana na kukubalika kuwa huu si wakati muafaka wa kuiwasilisha.

  Wakati huo huo, Spika Sitta alieleza kuwa kutojadiliwa kwa taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya Bunge iliyowasilishwa jana, kumetokana na taarifa hizo kuendelea kufanyiwa kazi.

  Taarifa hizo ni ya zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development ya Houston, Marekani, uendeshaji usioridhisha wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) unaofanywa na Kampuni ya Rites ya India.

  Nyingine ni kuhusu utendajii wa kazi usioridhisha wa Kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services (TICTS) na taarifa kuhusu uendeshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).


  Chini ya kanuni 37 kifungu cha 9 cha Bunge, Spika alisema aliziangalia taarifa hizo na kuona kuwa kuzijadili ni kupoteza muda na hivyo akaamua yachukuliwe maelezo ya kamati za Bunge, yawakilishe maoni yao.

  Hata hivyo aliwaambia wabunge kuwa uamuzi huo hauzuii katika mkutano ujao, mbunge kuleta hoja ili ijadiliwe kwa kina.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  Kamati ya madini ilikabidhi ripoti kwa Kikwete tangu mwezi April, 2008 zaidi ya miezi 10 iliyopita. Je, serikali inahitaji muda gani wa kuyajibu hayo maswali yaliyowasilishwa katika ripoti hiyo. Je, ripoti hiyo ilikuwa na jumla ya maswali mangapi ambayo serikali ilitakiwa kuyajibu? Na mangapi ambayo yameshajibiwa hadi hii leo!? Duh!!!! Spika na Bunge letu ni usanii mtupu!!! Kazi kweli kweli!!! Bado tuna safari ndefu sana ya kupambana na mafisadi na watetezi wao waliojaa ndani ya serikali, bunge na CCM :(
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,547
  Trophy Points: 280
  Kuna wabunge wa aina 3. Wananchi, walanchi na wenye nchi.
  1. Ni wale wenye uwezo wa uongozi na wito wa uongozi kwa kuwatumikia wananchi. Hawa wataweka maslahi ya taifa mbele na ndio tunawata viongozi wa watu waliochaguliwa na watu kwa manufaa ya watu.
  2. Ni wale wasio na wito wala uwezo bali wameingia bungeni kama moja ya njia sahihi za kujipatia neema. Hawa wako tayari kukopa ili akishaupata ubunge, atalipa deni taratibu. Hawa ni viongozi ambao hutanguliza maslahi yao kwanza na kushibisha matumbo yao hata kama waliowachagua watakufa kwa njaa. Hawa ndio walio wengi bungeni kwetu. Hawa ni viongozi wala nchi.

  3. Hawa ni wale ambao wako vizuri kiuchumi, haautegemei mshahara wala marupurupu ya ubunge. Hawa wanaingia bungeni kutafuta power za kuimarisha himaya zao. Hawa huwa hawachangii mijadala ya bungeni, wala hawana maswali, ila kwa sababu wana nguvu kubwa kiuchumi na jeuri ya pesa, wanalolitaka liwe, ndilo linakuwa. Hawa ndio viongozi wenye nchi.
  msharara
   
Loading...