Bunge la sasa limekuwa ni Bunge Uchwara limepoteza mwelekeo

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
103,039
2,000
Kinachoendelea ndani ya Bunge hili la MACCM ni upuuzi na uhuni MTUPU! Hakuna sababu ya kuendelea kuwa na Bunge la hovyo kama hili ambalo wabunge wamekosa heshima kabisa na kusahau wajibu wao Bungeni.

Hilo Bunge linaloongozwa na hao makada wa CCM huyo 'mchapa' bakora Ndugai na Naibu wake huyo mdada Tulia Ackson, namna wanavyoendesha huo mhimili wa Bunge, wamefanya vikao vya Bunge visiwe na tofauti yoyote na vikao vya NEC ya CCM!
 
nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,523
2,000
angalau bunge lililopita. bunge la sasa limekuwa muhuri kamili wa serikali. bajeti zote za serikali hata ziwe hovyo kiasi gani zinapitishwa tu. kiukweli wabunge wa ccm ni mizigo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
103,039
2,000
Halina maana ya kuendelea kuwepo ni uhuni tu na ubabe wa kuzuia hoja muhimu zenye tija kwa Watanzania. Futa paragraph hii ondoa page hii. Hapa ulipoandika hivi badilisha uandike hivi. Ali mradi ni unafiki wa hali ya juu! Ya nini kuwa na vyama vya upinzani nchini kama hawana uhuru wa kuongea kile wanachotaka wao.

Kunyanyaswa na kuonewa bungeni kila kukicha. Matusi ya Wabunge wa MACCM dhidi ya wapinzani RUKHSA lakini wapinzani wao huitwa kwenye kamati ya maadili uchwara kupewa vitisho vya kufukuzwa bungeni.

Bunge halina maana ya kuendelea kuwepo na vyama vingi nchini ni bora vifutwe tu badala ya kuendeleza huu unafiki uliokithiri.

Yaani ccm wamelifanya bunge kuwa kama bunge la Burundi
 
Inna

JF-Expert Member
Jan 13, 2017
11,040
2,000
Halina maana ya kuendelea kuwepo ni uhuni tu na ubabe wa kuzuia hoja muhimu zenye tija kwa Watanzania. Futa paragraph hii ondoa page hii. Hapa ulipoandika hivi badilisha uandike hivi. Ali mradi ni unafiki wa hali ya juu! Ya nini kuwa na vyama vya upinzani nchini kama hawana uhuru wa kuongea kile wanachotaka wao.

Kunyanyaswa na kuonewa bungeni kila kukicha. Matusi ya Wabunge wa MACCM dhidi ya wapinzani RUKHSA lakini wapinzani wao huitwa kwenye kamati ya maadili uchwara kupewa vitisho vya kufukuzwa bungeni.

Bunge halina maana ya kuendelea kuwepo na vyama vingi nchini ni bora vifutwe tu badala ya kuendeleza huu unafiki uliokithiri.
Daah umeongea kwa uchungu, sijui kama wanasomaga haya maoni yetu
Hapa,
Hapa hamna namna ni kumtoa tu 2020 huyo sizonje wao mana na wabunge wa ccm wanafanya hvo kumfurahisha hawataki challenge yoyote washakua kama huyo mtu wao
 
  • Thanks
Reactions: BAK

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
103,039
2,000
Wanaudhi sana hawa wahuni Inna. Nchi haina maendeleo yoyote yale ya kuridhisha halafu bungeni wanafanya uhuni tu na ubashite na wakqti huo huo Watanganyika tukiwa hatuna hata kitu kimoja cha kujivunia katika miaka 56 ya uhuru wa Tanganyika.

Daah umeongea kwa uchungu, sijui kama wanasomaga haya maoni yetu
Hapa,
Hapa hamna namna ni kumtoa tu 2020 huyo sizonje wao mana na wabunge wa ccm wanafanya hvo kumfurahisha hawataki challenge yoyote washakua kama huyo mtu wao
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,988
2,000
Tuchague wabunge wapinzani wengi idad yao ikizidi ya maccm basi hapo taifa litakuwa limekombolewa,na huu ndo mwarobaini wa matatizo mengi wananchi hawajui siri hii
Umeongea ukweli kabisa..
Ila kwa tume hii ya Uchaguzi..
Kazi ipo Mkuu.
Kumbuka na hawa wakurugenzi wapya wa halmashauri amewateuwa makada kabisa wa ccm ili wasaidie kwenye wizi.
 
tamuuuuu

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
14,252
2,000
Tanzania kuna bunge?
Ni upuuzi tu,sasa wabunge gani hao wao hawajielewi hasa wale kijani.
Yani wapo pale ushabiki tu,kiranja wao akisema nataka watanzania mtembee uchi kuanzia Leo,wapinzani wakigoma wao wanaunga mkono na kupambana kweli,MAJUHA CCM.

Tume huru idaiwe mapema ccm itoke vinginevyo watanzania mtapata tabu sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom