Bunge la Marekani linamwajibisha Trump

Bunge la Marekani linamwajibisha Trump

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,896
Bunge la Marekani (Congress) limepiga kura ya kihistoria kutokuwa na Imani na Rais wa nchi hiyo Donald Trump kura ambayo imefungua milango ya mashtaka dhidi yake.
.
Kura hii inamaanisha kuwa Bunge dogo la nchi hiyo (Senate) litaanza utaratibu wa kumuondoa Rais Donald Trump madarakani mwezi Januari.
.
Trump anakabiliwa na tuhuma za kukiuka kiapo cha urais, kukosa uadilifu na matumizi mabaya ya madaraka kwa kuiagiza Ukraine kumchunguza makamu wa rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, ambaye yuko katika kinyang'anyiro cha kuwania urais kupitia Democratic.
.
Trump atafika mbele ya Seneti mwezi Januari lakini Bunge hilo lina wanachama wengi wa chama chake (Republicans) hivyo wengi wanadhani Trump atavuka kikwazo hicho na atasalia kuwa Rais wa Marekani. Yeye mwenyewe (Trump) amenukuliwa akisema kuwa Wabunge wa upande wa Democratic wamepangwa na kulazimisha kupiga kura ya kumuondoa hata kwa wale wasiotaka lakini ameeleza anaamini kuwa watakwenda kwenye Seneti na watashinda.
.
Bunge la Marekani (Congress) lina wajumbe wengi wa Democratic kuliko wa chama tawala Republican lakini Bunge dogo (Senate) lina wajumbe wengi wa chama tawala kuliko wapinzani wa Democratic.

#CloudsDigitalUpdates
 
Hakika Marekani wameonyesha njia.......

Kwamba ni wajibu wa Rais aliyeko madarakani kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi aliyoapa kuitii kabla hajaingia madarakani

Kuisigina Katiba ya nchi waziwazi kama afanyavyo Jiwe, hakika ni lazima impeachment imuhusu
 
Huwa nashanga mtu anayetakiwa kumdhibiti jiwe wamekuwa maswahiba kila sehemu yupo, kama kale ka msemo ka uliko tupo!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao ni wenzake wa ndani ya system! Wamegawana mihimili tu!

System ya kuitafuna nchi! Kule kashika ndugai, kule Ibrahim, kule John. Keki iko mezani.

Kwa chini kule wameweka jeshi ambalo ni watoto wa wanyonge wanaolipwa mishahara minono ya kuwahadaa waendelee kudanganyika kuwa na wao ni sehemu ya dola ili wawashughulikie watanganyika wanaotaka kuleta kidomo domo!

Kwa juu juu kule kuna undercover officers wa kuangaliaa nani analeta fyoko miongoni mwa watanganyika wanyonge!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika Marekani wameonyesha njia.......

Kwamba ni wajibu wa Rais aliyeko madarakani kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi aliyoapa kuitii kabla hajaingia madarakani

Kuisigina Katiba ya nchi waziwazi kama afanyavyo Jiwe, hakika ni lazima impeachment imuhusu
Hiyo mtasubiri sana trump hataondoka white house ingekuwa afrika hapo sawa.
 
USA wamenifundisha jambo fulani muhimu - mwanzo nilitaka kumlaumu Obama kwa nini hakuleta misaada mingi East Africa hususani Kenya wakati wa utawala wake.

Kumbe kila hatua ya Rais inapimwa na kujadiliwa. Najiuliza hivi Marais wetu, Mabunge yetu, na Mabaraza ya kimahakama wana jambo la kujifunza toka nchi zilizoendelea?

Kwa nchi kama Tanzania siku akitokea rais mnyimifu na mbinafsi atahamisha rasilimali za nchi kuwa zake, za mkoa wake na hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi yake
 
Hakika Marekani wameonyesha njia.......

Kwamba ni wajibu wa Rais aliyeko madarakani kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi aliyoapa kuitii kabla hajaingia madarakani

Kuisigina Katiba ya nchi waziwazi kama afanyavyo Jiwe, hakika ni lazima impeachment imuhusu

Umetumia akili kuandika hapa au umefyatuka tu? Hilo bunge lililompinga trump wengi ni upinzani, na litakalombakiza wengi ni chama chake, sasa hapo tofauti na hapa kwetu ipo wapi? Kwani hapa kwetu upinzani ulishawahi kupiga kula ya ndiyo kwa serikari? Msiwe mnashabikia vitu abavyo havipo,
 
Unafananisha mlima na kichuguu
Domokrasia America ilianza karne ya 18
Wana marais 45 waliopita
Ss tumeanza 92 alafu unataka tuwe sawa
Marekani wamekufa wanaharakati mamilioni kuitafuta hiyo domokiasi
Ss kwetu wanaharakati wapo kwenye keyboad
Ni tofauti kubwa sana..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom