Bunge la Marekani lapitisha sheria kumbana Trump kupigana vita na Iran bila ridhaa yake

Congress wanaujua mziki wa Iran vyema wanajua ni jinsi gani washngton maslahi yake yatakavyo guswa pia
 
Congress wanaujua mziki wa Iran vyema wanajua ni jinsi gani washngton maslahi yake yatakavyo guswa pia
Waliopitisha huo upuuzi ni Baraza la Wawakilishi/Hous of Representatives ambalo lina democratic wengi ambao ndio waliingia ule makataba wa kipuuzi na Iran chini ya Obama. Congress lipo chini ya Republicans ambao ndio watabe waliovunja huo makataba wa kindezi.
 
Leo hii unaita mabos wako wapuuzi ww
Waliopitisha huo upuuzi ni Baraza la Wawakilishi/Hous of Representatives ambalo lina democratic wengi ambao ndio waliingia ule makataba wa kipuuzi na Iran chini ya Obama. Congress lipo chini ya Republicans ambao ndio watabe waliovunja huo makataba wa kindezi.
 
Tukiachana na hilo bunge la Us kupitisha sheria hio ukweli mchungu Iran wako sawa haswaaa, na wamejipanga kabisa, alaf kitu kinachowaogopesha zaidi hao wabunge wa Us ni kuwa hawajui Iran itajibu kivipi, maana vitisho vya maneno tu vya Iran vimeshusha petrol dollars thamani, kiukweli Dunia ya sasa ukiwa na silaha hatari, alaf anga lako ukijua kulifunga hautoguswa na nchi yyte mpaka Dunia itamaliza, kubwa utakachofanyiwa ni vikwazo, na vikwazo ukijua kucheza navyo ndio unawamaliza kabisa aaa, Hongera sana Iran
UK nao wanatafuta sababu ya kuachia meli kuficha aibu ya mkwara waliopigwa na Iran. Waziri mambo ya nchi za nje wa UK kalazimika kumpigia Mh.Zarif wa Iran akimuomba muahakikishie ile tanker ya mafuta haiendi Syria ili aweze kuachia meli hiyo. Wale mabaharia wa hiyo hiyo meli waliokamatwa wameachiwa...
 
Nimeona hio Habari mkuu, Inaonyeshea wanamuogopa sana sasaivi, meli za Uk hazitembei tena Mashariki ya kati, wanaona bora warejeshe mpira kwa kipa
UK nao wanatafuta sababu ya kuachia meli kuficha aibu ya mkwara waliopigwa na Iran. Waziri mambo ya nchi za nje wa UK kalazimika kumpigia Mh.Zarif wa Iran akimuomba muahakikishie ile tanker ya mafuta haiendi Syria ili aweze kuachia meli hiyo. Wale mabaharia wa hiyo hiyo meli waliokamatwa wameachiwa...
 
Haha haha haha haha

Ina maana hizi ndege F35 na F22 zime kuwa kwerea au kunguru weusi...
Mkuu kwani ulikuwa hujuwi kwa nini Recep-Tayyip-Erdoğan Aliposema lazima ni nunuwe S-400 kwa pesa ndefu na kuivunja katiba ya Nato inayo mlazimisha kununuwa mifumo hio kwa washirika wa NATO!
Alisha juwa S-400 ikifu'nga Anga hao Kware F-35 na F-22 wana nasa kwenye ulimbo + Kunguru Weusi F-16 !
Ukisikia Russia waliposema wanauwezo wa kufunga anga wana uwezo kweli na kuzifanya GPS ziwe Bluetooth!!
 
Kuna Watu humu naona wamekuwa mashabiki, kama vile tu tunavyoishi kule uswahilini kwetu.

Kwanza tukumbuke Iran na UK/ USA ni jamii mbili tofauti, ni kama mfano wa Binaadamu na mdudu Mbu au Nyoka..Binaadamu tunamugopa sana Nyoka si kwa sababu Nyoka ni kiumbe mkubwa sana au mwenye akili sana kuliko Binaadamu bali ni tofauti ya utashi uliopo kati yetu na wao, wakati Binaadamu wewe una matarajio yako, mipango, future yako n.k..Nyoka yeye hana chochote anachowaza zaidi ya wakati ule uliopo mbele yake...wakati wewe unahofia maisha yako, famillia, kazi n.k kabla ujakabiliana naye, yeye Nyoka hana cha kupoteza, kwa hiyo ni rahisi wewe kuamua kumkimbia kuliko kukabiliana nae...ingawa kwa uzito wako na umbo lako ni zaidi ya mara l000 kwake, na ungeweza hata kumshika na kumminya mpaka afe, tena hata kwa mkono mmoja tu.

Ni kweli UK/USA wanaiogopa Iran, na si wao tu bali yeyote asiyependa uharibifu usio na sababu anaiogopa Iran.

Kwa Marekani wanamjua Trump wao, ndio maana wenye nafasi ya kumdhibiti wanaingilia kati...maana Trump si Mtu wa kujali sana matokeo...naye ni kama Nyoka au Mbu.

Kijiografia Iran na UK/USA sio majirani, hivyo ni wazi kuwa Iran atataka kushambulia 'maslahi' ya USA/UK yaliyokaribu au hata popote pale atakapofikia, na hata raia wa mataifa hayo, ili hali kuna raia wa Iran kule UK/USA ambao wao watabaki salama salmini kwani UK/USA hawawezi kufanya chochote kwa hao raia wasiohusika...kumbuka Iran anafadhili makundi mbalimbali, kwa hiyo usishangae hata huku Tanzania raia wa UK/USA wakawa kwenye risk.....ref mfano wangu wa Nyoka na Binaadamu.

Kwa vyovyote Iran atataka kujibu kwa kushambulia Israel, kwa hivyo vita itakayoanzishwa na UK/USA itasababisha kero kwa Israel, na hata Saud Arabia na majirani wengine wasiohusika...ndio maana kuna sababu kubwa ya wao kujiuliza mara mbili kabla ya kuingia vitani.

Pia Iran akishambuliwa lazima Urusi atavutiwa kuingilia, sasa je sababu zinatosha kuiingiza Dunia kwenye yote hayo?.

Hivi wale mnaoishabikia Iran, ni kwa sababu tu wametoa vitisho vya mdomo? siku zote zilongwa mbali zitendwa mbali.... Iraq tu iliwatoa jasho wakasumbuana kwa miaka 8, mpaka UN wakaingilia kati na kufanikiwa kuwaamua.
 
Congress wanajua madhara ya kuivamia Iran. Good warning to Trump.
Kama nimesoma vizuri kuna sehemu wanasema hawako tayari kuruhusu serikali yao inaingiza taifa lao ktk "long decade war" bila idhini ya congress.

Ina maana wanajua Iran sio nyanya, wakianza vita itachukua zaidi ya muongo mmoja na kulitia taifa lao hasara kubwa.
 
Kama nimesoma vizuri kuna sehemu wanasema hawako tayari kuruhusu serikali yao inaingiza taifa lao ktk "long decade war" bila idhini ya congress.

Ina maana wanajua Iran sio nyanya, wakianza vita itachukua zaidi ya muongo mmoja na kulitia taifa lao hasara kubwa.
Kwani Afghanistan ni strong,mbona Vita ioo zaidi ya muongo mmoja?
 
Hawa binadamu wanaojiita Wamarekani wana akili za ajabu sana sijapata kuona. Kinachochekesha ni kwamba hiyo sheria ni ya njia moja tu (One way operation) na wala haiwezi kumzuia Iran asishambuliwe.

Mchezo uko hivi: Hiyo sheria inamzuia Marekani asifanye shambulio dhidi ya Iran (Offensive Warfare) lakini haimnyang'anyi Marekani haki yake ya kujilindi kipindi atakposhambuliwa na Iran au atakapohisi kwamba anashambuliwa na Iran (Right to self-defense) ambayo iko kwenye Ibara ya 51 ya Hati Idhini ya Umoja wa Mataifa (United Nations).

Upande mwingine hii sheria imemgusa Marekani tu lakini haijawagusa washirika wake wa kimkakati (Strategic Partners) ambao wanaweza kusababisha songombingo na Iran na kumlazimisha Marekani aingie kwenye mgogoro.

Hivi leo unadhani Israel au Saudi Arabia wakianzisha songombingo na Iran, unadhani Marekani ataacha kuingilia kweli ?? Lazima ataingilia na akiingilia lazima ile kwake, vivyo hivyo asipoingilia lazima ile kwake. Democrats na Republicans wote ni maswahiba wakubwa wa Israel.........

Naomba nikupe mfano hai kabisa: Mwaka 1914 kuelekea 1916 Wamarekani walikataa katakata kujihusisha na vita ya kwanza ya dunia na walifanya hivihivi. Lakini waliingia kwenye ile vita chini ya mgongo wa kujilinda dhidi ya Uvamizi wa Mexico na Ujerumani. Soma kuhusu The Zimmerman Telegram.

Mfano mwingine ni kwamba Security Commitments ambazo zimejengwa kupitia mifumo ya kujihami inalifanya bunge la Marekani lisiwe na maana yoyote ile. Mfano Ibara ya 5 ya NATO inasema kwamba akivamiwa mwanachama moja basi wote wanaingia vitani. Hapa bunge halihusiki kabisa.

Sasa mkataba wa Marekani na Israel sijui unasemaje kuhusu ulinzi lakini kama Bunge linautambua basi kama Israel atalianzisha na Iran moja kwa moja Marekani lazima ataingia vitani tu.....

NB: Yote tisa, hii sheria bado haijapita, na sidhani kama itapita kwasababu kumbana Raisi wa Marekani siyo rahisi maana ana VETO Power ya kuipinga. Iran asifanye makosa ya kuwaamini wazungu, itakula kwake. Hawa binadamu wenye macho ya bluu a nywele za khaki siyo wema kabisa.
 
Back
Top Bottom