Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,498
- 51,090
- Thread starter
- #41
Hawa binadamu wanaojiita Wamarekani wana akili za ajabu sana sijapata kuona. Kinachochekesha ni kwamba hiyo sheria ni ya njia moja tu (One way operation) na wala haiwezi kumzuia Iran asishambuliwe.
Mchezo uko hivi: Hiyo sheria inamzuia Marekani asifanye shambulio dhidi ya Iran (Offensive Warfare) lakini haimnyang'anyi Marekani haki yake ya kujilindi kipindi atakposhambuliwa na Iran au atakapohisi kwamba anashambuliwa na Iran (Right to self-defense) ambayo iko kwenye Ibara ya 51 ya Hati Idhini ya Umoja wa Mataifa (United Nations).
Upande mwingine hii sheria imemgusa Marekani tu lakini haijawagusa washirika wake wa kimkakati (Strategic Partners) ambao wanaweza kusababisha songombingo na Iran na kumlazimisha Marekani aingie kwenye mgogoro.
Hivi leo unadhani Israel au Saudi Arabia wakianzisha songombingo na Iran, unadhani Marekani ataacha kuingilia kweli ?? Lazima ataingilia na akiingilia lazima ile kwake, vivyo hivyo asipoingilia lazima ile kwake. Democrats na Republicans wote ni maswahiba wakubwa wa Israel.........
Naomba nikupe mfano hai kabisa: Mwaka 1914 kuelekea 1916 Wamarekani walikataa katakata kujihusisha na vita ya kwanza ya dunia na walifanya hivihivi. Lakini waliingia kwenye ile vita chini ya mgongo wa kujilinda dhidi ya Uvamizi wa Mexico na Ujerumani. Soma kuhusu The Zimmerman Telegram.
Mfano mwingine ni kwamba Security Commitments ambazo zimejengwa kupitia mifumo ya kujihami inalifanya bunge la Marekani lisiwe na maana yoyote ile. Mfano Ibara ya 5 ya NATO inasema kwamba akivamiwa mwanachama moja basi wote wanaingia vitani. Hapa bunge halihusiki kabisa.
Sasa mkataba wa Marekani na Israel sijui unasemaje kuhusu ulinzi lakini kama Bunge linautambua basi kama Israel atalianzisha na Iran moja kwa moja Marekani lazima ataingia vitani tu.....
Hakuna ambiguity wala cha ajabu hapo, Congress hata siku moja haiwezi kuweka zuio dhidi ya Self Defense!
Hata Sisi Tanzania na ubovu wa katiba yetu lakini bado inamnyima haki hata raisi wa nchi kuwazuia wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupambana na adui aliyeikalia nchi yetu kimabavu,na inamnyima mtu yeyeote kusaini mkataba wa kukubali nchi hii kushindwa vita au kuitoa Jamhuri ya Muungano kwa adui SEMBUSE CONGRESS?
Walichokifanya ni cha kawaida tu lakini chenye manufaa kwa nchi yao, mambo ambayo allies watafanya wakafanye wao, kama Marekani akitaka kuingia basi itabidi arudi kwa congress waidhinishe