Bunge la bajeti, Mawaziri wataleta mrejesho gani, watashawishije wabunge kupitisha bajeti ijayo?

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/17 inaisha baada ya mwezi mmoja kuanzia sasa.Zile trions of money watu wanataka waone mrejesho wake kama zilivyoahidiwa, maana hata wabunge wana hali ngumu sana.Fedha imeenda kidogo sana majimboni,wanaishi kwa kujificha ficha, na wengine wamekimbia vijijini sasa wanakaa mijini.

Mawaziri mna wakati mgumu kwanza wa kuleta mrejesho wa bajeti iliyopita,lakini pia kuwashawishi wabunge wengine wawaunge mkono.Hali majimboni n mbaya sana.

Ikumbukwe sasaiv, kuna mijadala na upepo mingi sana inayovuma kila siku. Mara vyeti feki, mara njaa , mara ajira, mara sukari, nk nk.

Kaeni chini vzr,tumieni wataalamu wenu mshibe nondo za kuwajibu wabunge na kuwashawishi bajeti ijayo ipite.Kuna sura zimeshachafukwa bungeni.
 
Wabunge si watetezi wetu kiasi hicho kama unavyodhania. Wakikaa tu mjengoni account zao zinasoma. Hawana uchungu nasi hata kidogo.
 
Tangu nimeanza kuelewa habari za uchumi,fedha na biashara sijawahi kuona ama kusikia budget iliyofeli km ya mwaka 2016/17. Duuuuuuh,34% tu ya miradi ya maendeleo ndiyo imetoka!!!!!!! Sasa hayo maendeleo tunayoyapigia kelele sijui tutayapataje.......?
 
Hivi tunapoambiwa na serikali kwamba "tunabana matumizi" wakati huo huo pesa zilizoidhinishwa na Bunge zinashindwa kuwafikia wananchi, tafsiri yake ni nini, au ndo pesa zote zinaelekezwa kwenye ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato?
 
Kwa wabunge wa Ccm usitegemee jipya. Wao wamekwenda bungeni kusema ndioooo
Walipitisha sheria ya madini kwa hati ya dharura na kishabiki kwa wingi wao leo wanaunda tume kuchunguza mchanga kwenda nje ya nchi. Wamesha sahau wao ndio walipitisha sheria na wanacho hitaji wao ni mrahaba tuu. Dhahabu ni ya mwekezaji. Nchi ya ajabu sana hii. Hapa tulipo ni kwa neema za wingi wa wabunge wa Ccm
 
Wabunge gani hao watakaothubutu kuipinga bajeti ya mkulu? Walishapigwa mkwala walishalainika kama mrenda wamebaki ni ndioooooo!! hoja imepita!
 
Back
Top Bottom