Mrejesho kuhusu Uwakilishi Wangu katika Mkutano wa pili wa Bunge

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Wakati wa kuomba kura nilikuja kwenu katika ukumbi huu kuwaomba mniunge mkono, kati ya ahadi nilizotoa wakati huo ni kuchukua maoni yenu na kuyawasilisha bungeni. Naomba kwa leo niwape mrejesho kuhusu uwakilishi wangu katika mkutano wa pili wa bunge kwa ajili ya kupata maoni ya kuzingatia katika mikutano ijayo.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 63 (2) Bunge ndicho chombo kikuu chenye madaraka kwa niaba ya wananchi ya kuishauri na kuisimamia serikali. Katika kutimiza wajibu huu kwa nafasi yangu ya ubunge wa Jimbo la Ubungo niliwawakilisha wananchi wenzangu kwenye Mkutano wa Pili wa Bunge la Kumi ulioanza tarehe 8 Februari na kuahirishwa tarehe 18 Februari 2011. Naomba nitoe mrejesho kwa muktasari kuhusu ushiriki wangu katika vikao vya mkutano husika wa bunge.

Katika kikao cha kwanza tarehe 8 Februari wakati wa mjadala juu ya Azimio la kufanya Mabadiliko katika Kanuni za Bunge toleo la 2007 niliomba muongozo wa Spika kwa kurejea kanuni 68 (7) kuhusu haja ya kiongozi wa kampi rasmi ya upinzani kupewa nafasi ya kuzungumza na nikatoa hoja kwa mujibu wa kanuni 55 (3) (b) kwamba mjadala uahirishwe mpaka kwanza kiongozi wa upinzani apewe nafasi ya kuzungumza kama zilivyo mila na desturi za uendeshaji wa Bunge. Spika alilazimika kumpa kiongozi wa upinzani nafasi ya kuzungumza pamoja na kuwa tayari alikuwa amefunga orodha ya wachangiaji hapo awali bila kumpa nafasi. Baada ya hotuba ya kiongozi wa upinzani nilishiriki kutoka bungeni ili kutoshiriki maamuzi ambayo yalilenga kuminya demokrasia ya kambi rasmi ya upinzani bungeni na pia kutoa fursa kwa wabunge wa chama tawala kuchagua wenyeviti wanaowataka kuwakilisha kambi rasmi ya upinzani kwenye kamati za muhimu za usimamizi wa fedha za umma kinyume na misingi ya utawala bora.

Katika kikao cha tatu tarehe 10 Februari mara baada ya maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu niliomba muongozo wa Spika kwa kurejea kanuni ya 68 (7) kutokana na kauli ya Spika ya kumtaka Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuthibitisha papo kwa papo bungeni juu ya uongo wa Waziri Mkuu kwa mujibu wa kanuni 63 (3) (4) na 68 (1). Nilimueleza Spika kwamba Lema hakutumia kanuni 68 (1) ya ‘kuhusu utaratibu' kama Spika alivyodai bali alitumia kanuni 68 (7) ya kuomba muongozo wa Spika wa hatua gani za kuchukua iwapo kiongozi mkubwa kama Waziri Mkuu analidanganya bunge. Aidha nilimkumbusha Spika kuwa alishatoa muongozo kuwa alete taarifa hivyo hakupaswa kutoa ushahidi wa papo kwa papo. Kauli yangu ilimfanya Spika atoe mwongozo mwingine wa kumtaka Lema awasilishe maelezo yake tarehe 14 Februari katika kikao cha asubuhi.

Katika kikao cha nne tarehe 11 Februari nilitoa mchango wangu wa papo kwa papo bungeni wakati wa hoja ya kujadili Hotuba ya Rais Kikwete ya kufungua bunge jipya. Katika hotuba hiyo niliwashukuru wananchi na kuzungumzia suala la viongozi kuepuka kupandikiza mbegu ya udini, haja ya kukabaliana na mfumuko wa bei unaosababisha kupanda kwa gharama za maisha, suala la kufufua viwanda na jitihada za kukabiliana na matatizo ya maji katika jimbo la Ubungo. Nilianza hotuba hiyo kwa kuweka katika kumbukumbu za historia namna tulivyoshinda Ubungo kwa nguvu ya umma ya wazee, wanawake na vijana pamoja na vikwazo vya kikatiba na kisheria. Katika hotuba hiyo nimetaka vyombo vya ulinzi na usalama vimshauri Rais na viongozi wengine kuacha kutoa kauli za mara kwa mara ambazo kimsingi ndizo zinazopandikiza udini. Aidha nimeitaka serikali kuwasilisha taarifa ya hali halisi kuhusu mfumuko wa bei na hatua ambazo inapendekeza zichukuliwe ili kudhibiti kupanda kwa gharama za maisha ambapo kunaweza kuleta migogoro katika taifa. Nilidokeza kuhusu mwelekeo wa kufa kwa kiwanda cha Urafiki Ubungo na kueleza kusudio la kuwasilisha maelezo binafsi kuhusu suala husika. Nilieleza Bunge kuhusu Kongamano la Maji Ubungo na kueleza dhamira yangu ya kuendelea kushirikiana na Wizara katika kutatua kero husika. Sikuendelea zaidi kwa kutokana na muda wa dakika kumi kuisha hata hivyo niliwasilisha mchango wa ziada wa maandishi kuhusu ufisadi hususani kuhusu Dowans na Kagoda na michezo ikiwemo suala la kurudishwa kwa viwanja vya umma ambavyo vimehodhiwa na chama kimoja baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi ( Bonyeza hapa kusoma hotuba husika: http://mnyika.blogspot.com/2011/02/hotuba-yangu-bungeni-katika-mkutano-wa.html )

Katika kikao cha tano tarehe 14 Februari mara baada ya kipindi cha maswali na kauli za mawaziri Spika aliruhusu moja kwa moja Hoja ya Kujadili Hotuba ya Rais ya kufungua bunge kuendelea. Nilitaka muongozo wa Spika kwa mujibu wa kanuni 68 (7) na 63 (6) ambayo inatoa fursa ya mbunge kutoa uthibitisho wa ukweli bungeni ili Lema apewe nafasi ya kuwasilisha maelezo yake bungeni katika kipindi hicho cha asubuhi kama alivyoelekeza Spika mwenyewe katika kikao cha tatu. Hata hivyo, Spika alitoa muongozo mpya kuwa Lema awasilishe maelezo na ushahidi wake kwa maandishi ofisini kwake. Katika kikao hicho pia niliuliza swali la nyongeza baada ya majibu ya Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Swali namba 65 ambapo nilihoji kwa kuwa waraka wa kutengua utaratibu wa wahitimu wenye stashahada wenye kupaswa kurudia mitihani michache kufanya hivyo wakiwa kazini ulisambazwa ukiwa umechelewa huku wakitakiwa kulipia ada ya mitihani na kujiandaa je serikali iko tayari kutoa muda wa nyongeza zaidi ya uliotangazwa wa mwezi Aprili? Katika majibu yake naibu waziri alieleza kwamba serikali itatoa muda mwingine wa walimu hao kufanya mitihani yao ikiwa wakishindwa kufanya mwezi Aprili hata hivyo serikali iliwahimiza wafanye hivyo wakati huu ili kuepuka ushindani wa nafasi za ajira utakaokuwepo kipindi kijacho.

Katika kikao cha sita tarehe 15 Februari mara baada ya kauli za Mawaziri ambapo Waziri wa Nishati na Madini alitoa kauli ya serikali kuhusu hali ya umeme nchini na utekelezaji wa miradi ya umeme katika kipindi kifupi na cha kati nilitoa hoja ya dharura kwa mujibu wa kanuni 55 (3) (e) na kanuni ya 47 ili bunge lijadili jambo la dharura la mgawo wa umeme unaolikumba taifa. Nilitaka jambo hilo lijadiliwe kwa kutoa maelezo ya namna linavyowathiri maisha ya wananchi waliowengi na pia kuathiri uchumi wa taifa. Pia, nilieleza kwamba katika kauli yake Waziri ameeleza hatua za dharura zinazotaka kuchukuliwa na serikali ambazo nyingine kimsingi sio za dharura na pia zinahusisha matumizi makubwa ya fedha za wananchi ambazo nilizikadiria kuwa ni zaidi ya bilioni 300 nje ya bajeti ya serikali hivyo ni muhimu bunge likajadili. Spika wa Bunge akaikataa hoja hiyo pamoja na kuwa iliungwa mkono na idadi ya wabunge inayohitajika badala yake akanitaka kama Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nikazungumzie mambo hayo kwenye kikao cha kamati husika hapo baadaye. Kimsingi nilitaka suala hilo lijadiliwe kwa sababu katika maelezo yake Waziri alitaja kuwa serikali inakusudia kukodi mitambo ya dharura ya MW 260 (hii ni mitambo ambayo gharama yake ni kubwa sana, na inaweza kuchelewa isije wakati wa dharura kama ilivyokuwa kwenye sakata la Richmond), pia Waziri hakuzungumzia kabisa kuhusu mitambo ya Dowans ambayo asubuhi ya siku hiyo nilizungumza LIVE na TBC1 na kutaka serikali iitaifishe mitambo husika kwa kutumia sheria ya uhujumu uchumi na sheria nyinginezo ili iiwashe kwa dharura na kupunguza pengo la MW 120 wakati taifa likiendelea kufanya maamuzi ya namna ya kufidia kiwango kitachobaki. Aidha mjadala huo ungewezesha pia kutaka waziri awajibike kwa kutochukua hatua za mapema za kukabiliana na kinachoitwa dharura ambacho kilishafahamika toka mwaka 2006, 2008 na 2009 na maamuzi ya kuondokana na hali hiyo yakafanyika lakini hayakutekelezwa kwa wakati ( Bonyeza hapa kwa kauli ya awali kuhusu Dowans na mgawo wa umeme: http://mnyika.blogspot.com/2011/02/mitambo-ya-dowans-itaifishwe-waziri.html)

Katika kikao cha saba tarehe 18 Februari niliuliza Swali la Nyongeza kutokana na majibu ya Swali namba 85 kwa Wizara ya Maji. Kwenye swali langu la Nyongeza kwanza nilimkosoa Naibu Waziri kwa kutaja majina ya miradi ya maji ambayo iko Kigamboni na kueleza kwamba ni ya Ukonga na kumweleza Naibu Waziri kuwa pamoja na uwekezaji wa fedha za miradi ya maji za Benki ya Dunia na Wadau wengine wa maendeleo kwenye Ruvu Juu na Ruvu chini ikiwemo kuweka mtandao mpya wa mabomba ya maji maarufu kama mabomba ya wachina; bado maji kwenye kata za Kwembe, Kibamba, Msigani, Mbezi, Saranga, Kimara nk maji hayatoki kwa pamoja na mambo mengine upotevu wa maji na wafanyabiashara wanauza maji bei juu kujiunganishia kinyemela; je Naibu Waziri yuko tayari kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya maji ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa? Naibu Waziri alijibu kwa kunipongeza kwa kuweka kipaumbele cha kwanza suala la maji katika kazi zangu na kuahidi kutembelea miundombinu husika kwa kushirikiana nami. Pia, niliuza Swali namba 91 kwa niaba ya Mbunge wa Mpanda Mjini Said Amour Arfi kwa Wizara ya Fedha kuhusu kero za upatikanaji wa mafao ya wastaafu na mirathi kwa watumishi waliokufa kazini. Baada ya majibu ya Waziri kueleza kwamba sababu ni matatizo ya mawasiliano ukiwemo udhaifu katika mfumo wa kumbukumbu kwa upande wa watumishi wanaohudumiwa na mifuko; niliuliza maswali mawili ya nyongeza, moja kuhusu namna ambavyo serikali imepanga kuondokana na matatizo hayo ya mawasiliano na kumbukumbu hasa kwa kuwa wapo wastaafu na marehemu ambao kumbukumbu zao zote zimekamilika lakini bado kuna kero nyingi katika kupata mafao na mirathi. Pili, niliuliza swali la kutaka tamko la serikali kuhusu wastaafu wengine ambao hawahudumiwi na mifuko kama wale wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki ambao mpaka sasa wanahangaika kuhusu mafao yao. Serikali ilijibu kuwa haina tamko la kutoa kwa sasa kwa kuwa inasubiri kwamba suala la Wastaafu wa Afrika Mashariki lipangiwe jaji mwingine katika mahakama ya rufaa kama walivyoomba.

Kwa muktasari huo ni mrejesho kuhusu ushiriki wangu ndani ya vikao vya mkutano wa pili wa bunge la kumi. Hata hivyo, kuna masuala mengine yanayohusu ushiriki wangu katika shughuli nyingine za kibunge nje ya vikao kwa nafasi zangu zingine kama Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CHADEMA, Katibu wa Wabunge wa Mkoa wa Dar es salaam, Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, Mjumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo, Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani-Nishati na Madini na nafasi nyinginezo ambayo sijayaeleza katika taarifa hii. Nawashukuru sana wote walitoa maoni kwenye Mikutano ya Mbunge kuwasikiliza na kuzungumza na Wananchi tuliyoifanya Mbezi mwisho na Manzese Bakhresa siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano wa pili wa bunge, sehemu ya masuala mliyonituma nimeyawasilisha. Hata hivyo yako mengine kutokana na ufinyu wa muda na kubanwa na kanuni sikupata wasaa wa kuyawasilisha ikiwemo suala la hoja ya mchakato wa katiba mpya ambalo nililitolea kauli ya tahadhari baada ya serikali kukubaliana nami mchakato husika kuanzia bungeni kwa kutungwa kwa sheria (Rejea kauli yangu ifuatayo: JOHN MNYIKA: Tahadhari kuhusu serikali kupeleka muswada wa katiba mpya bungeni). Nawashukuru kwa kuniunga mkono.

Tuendelee kuwasiliana, kushauriana na kushirikiana.

Wenu katika utumishi wa umma,

John Mnyika (MB)
 
Mh. Mnyika tunashukuru kwa kuonyesha waziwazi ni nini ulikifanya uko bungeni ASAP baada ya kikao cha bunge kwisha. Suala la Umeme ni utata mtupu na ningependa kama utakuwa careful na huyo Mwenyekiti wa kamati ambaye ana act kana kwamba kamati ndio inaongoza wizara ya Nishati. Kamati jukumu lake ni kuisimamia serikali na kutoa mapendekezo, lakini jukumu bado linabaki Serikalini kwenye maamuzi.

Hakuna dharura kwenye umeme, na suala la mgao ni suala la kujitakia tu sisi watanzania. Kama waziri kivuli naomba sana upate advise kutoka kwa wataalamu wa umeme ili Emergency Power Purchase isiwepo kabisa kama option Tanzania. Suala muhimu ni kununua tu mitambo ya Gas kutosa GE au Wartisila ya 200MW kila mwaka for the next 3 yrs mfululizo ili by 2015 at least Tanesco iweze kujiendesha kibiashara.
 
Naomba na mimi nikupe pongezi kwa kazi kubwa unayofanya Mh Mnyika, lakini pia nikupe na pole kwa majukumu mengi uliyopewa katika kutumikia wananchi wa jimbo lako na taifa kwa ujumla. Mungu akuzidishie hekima, maarifa, afya na juhudi ya kutenda. Unatupa matumaini sisi wananchi wa kawaida tunaohangaika na maisha, lakini tunafuatilia kwa karibu kuona nani anatupigania kutuondoshea shida zetu. Asante.
 
What an increadible MP, This is a very passionate and touching feedback! Keep it up John.

Nilipata wasaa wa kusikiliza baadhi ya michango yako bungeni, nafarijika kukuarifu kuwa unapanga vizuri hoja zako. Nakuomb Mh John washirikishe wabunge wengine wa CDM, namna ya kujenga hoja zenye mvuto kwa wananchi, muwe wamoja pamoja na uwakilishi ulio tofauti bungeni na mahitaji tofauti, lakini kuna kujengeka ktk uongozi, na hi inahitaji kutiana moyo. Incourage others to speak and share their strategies fo people to enrich them!

Big up Mh. John
 
Mh. Mnyika tunashukuru kwa kuonyesha waziwazi ni nini ulikifanya uko bungeni ASAP baada ya kikao cha bunge kwisha. Suala la Umeme ni utata mtupu na ningependa kama utakuwa careful na huyo Mwenyekiti wa kamati ambaye ana act kana kwamba kamati ndio inaongoza wizara ya Nishati. Kamati jukumu lake ni kuisimamia serikali na kutoa mapendekezo, lakini jukumu bado linabaki Serikalini kwenye maamuzi.

Hakuna dharura kwenye umeme, na suala la mgao ni suala la kujitakia tu sisi watanzania. Kama waziri kivuli naomba sana upate advise kutoka kwa wataalamu wa umeme ili Emergency Power Purchase isiwepo kabisa kama option Tanzania. Suala muhimu ni kununua tu mitambo ya Gas kutosa GE au Wartisila ya 200MW kila mwaka for the next 3 yrs mfululizo ili by 2015 at least Tanesco iweze kujiendesha kibiashara.

Moelex23 .... nashukuru kwa ufafanuzi huu mzuri na wenye busara .... kinachotakiwa kuzingatia sasa hivi ni jinsi gani ya kujikwamua na tatizo hili sugu la mapungufu ya umeme unaozalishwa hapa nchini kwa ujumla... hivyo tuangalie namna ya kupata uzalishaji wenye uhakika kama suluhisho la tatizo la umeme tanzania na hii iendane na ushauri wa kitaalam zaidi bila kuzingatia shinikizo kutoka upande wowote ule ... emergency power purchase izingatie faida na hasara zinazokabili zoezi hilo na sio uharaka kwani hata huu mgao tulishauzoea .... miezi mitatu inaweza ikavumilika kutafuta ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi na siyo mobile turbines kama za DOWANS kwani hata hizo zisingewashwa muda wote kutokana na dhumuni halali la mitambo kuwa ni kwa ajili ya emergency
 
Kijana tupo nyuma yako.Nakutakia maisha mema katika kuiendereza chadema.Ushauri wangu kuweni pamoja wabunge wa CHADEMA hili pengo la Dr.W. S, lisionekane.alikuwa mstali wa mbele kuuliza maswali,kuchangia hoja na kuibua changamoto mbunge.Ndg wajua kuwa hata darasani vichwa vinaonekana tu na bongo lala hivyo hivyo.MAKUTAKIA KAZI NJEMA,MUNGU AKUBALIKI,MUNGU ISIMAMIE CHADEMA,AMINA
 
mh hongera sana. nadhani ni mbunge wa kwanza tz kufanya hivyo. tengeneza kitabu chako uweze kuweka kumbukumbu za mambo makubwa hayo unayofanya who knows baadae tunaweza kukupa urais!
 
Binafsi naku admire what you are doing at that age. Nilishawahi kukuandikia ktk FB that you've everything to inspire new generation. Ukifanikiwa maji kwa Ubungo hili jimbo utaliacha mwenyewe. Songa mbele, unaungawa na watu wengi sana na kamwe hutaanguka!
 
Nafarijika, mbunge amenipa habari za kule tulikomtuma. Excellent Mh Keep it up!
Wale wabunge mliokuwa mumesinzia, ni busara na uungwana pia kama mtawaambia wapiga kura wenu '' samahani kikao hiki kilichokwisha nilikuwa napitiwa na usingizi mara kwa mara'' at least uungwana utatufariji. Kulala si kosa!
 
Mheshimiwa Mnyika,

Tunakila sababu ya kujivunia uwepo wako Bungeni. Endapo anagalau wabunge Mia moja kati ya Mia tatu na hamsini waliopo wangejitoa kwa kadri unavyojitoa hii nchi ingepiga hatua kubwa.

Ila hata kwa kujitoa kwako tunashukuru na wengi unawagusa katika maisha yao ya kila siku. Uongozi ndio unachokionyesha na kukifanya.

Kila kheri brother na Mungu akulinde na hatari zote za dunia.
 
Wakati wa kuomba kura nilikuja kwenu katika ukumbi huu kuwaomba mniunge mkono, kati ya ahadi nilizotoa wakati huo ni kuchukua maoni yenu na kuyawasilisha bungeni. Naomba kwa leo niwape mrejesho kuhusu uwakilishi wangu katika mkutano wa pili wa bunge kwa ajili ya kupata maoni ya kuzingatia katika mikutano ijayo.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 63 (2) Bunge ndicho chombo kikuu chenye madaraka kwa niaba ya wananchi ya kuishauri na kuisimamia serikali. Katika kutimiza wajibu huu kwa nafasi yangu ya ubunge wa Jimbo la Ubungo niliwawakilisha wananchi wenzangu kwenye Mkutano wa Pili wa Bunge la Kumi ulioanza tarehe 8 Februari na kuahirishwa tarehe 18 Februari 2011. Naomba nitoe mrejesho kwa muktasari kuhusu ushiriki wangu katika vikao vya mkutano husika wa bunge.

Katika kikao cha kwanza tarehe 8 Februari wakati wa mjadala juu ya Azimio la kufanya Mabadiliko katika Kanuni za Bunge toleo la 2007 niliomba muongozo wa Spika kwa kurejea kanuni 68 (7) kuhusu haja ya kiongozi wa kampi rasmi ya upinzani kupewa nafasi ya kuzungumza na nikatoa hoja kwa mujibu wa kanuni 55 (3) (b) kwamba mjadala uahirishwe mpaka kwanza kiongozi wa upinzani apewe nafasi ya kuzungumza kama zilivyo mila na desturi za uendeshaji wa Bunge. Spika alilazimika kumpa kiongozi wa upinzani nafasi ya kuzungumza pamoja na kuwa tayari alikuwa amefunga orodha ya wachangiaji hapo awali bila kumpa nafasi. Baada ya hotuba ya kiongozi wa upinzani nilishiriki kutoka bungeni ili kutoshiriki maamuzi ambayo yalilenga kuminya demokrasia ya kambi rasmi ya upinzani bungeni na pia kutoa fursa kwa wabunge wa chama tawala kuchagua wenyeviti wanaowataka kuwakilisha kambi rasmi ya upinzani kwenye kamati za muhimu za usimamizi wa fedha za umma kinyume na misingi ya utawala bora.

Katika kikao cha tatu tarehe 10 Februari mara baada ya maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu niliomba muongozo wa Spika kwa kurejea kanuni ya 68 (7) kutokana na kauli ya Spika ya kumtaka Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuthibitisha papo kwa papo bungeni juu ya uongo wa Waziri Mkuu kwa mujibu wa kanuni 63 (3) (4) na 68 (1). Nilimueleza Spika kwamba Lema hakutumia kanuni 68 (1) ya ‘kuhusu utaratibu' kama Spika alivyodai bali alitumia kanuni 68 (7) ya kuomba muongozo wa Spika wa hatua gani za kuchukua iwapo kiongozi mkubwa kama Waziri Mkuu analidanganya bunge. Aidha nilimkumbusha Spika kuwa alishatoa muongozo kuwa alete taarifa hivyo hakupaswa kutoa ushahidi wa papo kwa papo. Kauli yangu ilimfanya Spika atoe mwongozo mwingine wa kumtaka Lema awasilishe maelezo yake tarehe 14 Februari katika kikao cha asubuhi.

Katika kikao cha nne tarehe 11 Februari nilitoa mchango wangu wa papo kwa papo bungeni wakati wa hoja ya kujadili Hotuba ya Rais Kikwete ya kufungua bunge jipya. Katika hotuba hiyo niliwashukuru wananchi na kuzungumzia suala la viongozi kuepuka kupandikiza mbegu ya udini, haja ya kukabaliana na mfumuko wa bei unaosababisha kupanda kwa gharama za maisha, suala la kufufua viwanda na jitihada za kukabiliana na matatizo ya maji katika jimbo la Ubungo. Nilianza hotuba hiyo kwa kuweka katika kumbukumbu za historia namna tulivyoshinda Ubungo kwa nguvu ya umma ya wazee, wanawake na vijana pamoja na vikwazo vya kikatiba na kisheria. Katika hotuba hiyo nimetaka vyombo vya ulinzi na usalama vimshauri Rais na viongozi wengine kuacha kutoa kauli za mara kwa mara ambazo kimsingi ndizo zinazopandikiza udini. Aidha nimeitaka serikali kuwasilisha taarifa ya hali halisi kuhusu mfumuko wa bei na hatua ambazo inapendekeza zichukuliwe ili kudhibiti kupanda kwa gharama za maisha ambapo kunaweza kuleta migogoro katika taifa. Nilidokeza kuhusu mwelekeo wa kufa kwa kiwanda cha Urafiki Ubungo na kueleza kusudio la kuwasilisha maelezo binafsi kuhusu suala husika. Nilieleza Bunge kuhusu Kongamano la Maji Ubungo na kueleza dhamira yangu ya kuendelea kushirikiana na Wizara katika kutatua kero husika. Sikuendelea zaidi kwa kutokana na muda wa dakika kumi kuisha hata hivyo niliwasilisha mchango wa ziada wa maandishi kuhusu ufisadi hususani kuhusu Dowans na Kagoda na michezo ikiwemo suala la kurudishwa kwa viwanja vya umma ambavyo vimehodhiwa na chama kimoja baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi ( Bonyeza hapa kusoma hotuba husika: http://mnyika.blogspot.com/2011/02/hotuba-yangu-bungeni-katika-mkutano-wa.html )

Katika kikao cha tano tarehe 14 Februari mara baada ya kipindi cha maswali na kauli za mawaziri Spika aliruhusu moja kwa moja Hoja ya Kujadili Hotuba ya Rais ya kufungua bunge kuendelea. Nilitaka muongozo wa Spika kwa mujibu wa kanuni 68 (7) na 63 (6) ambayo inatoa fursa ya mbunge kutoa uthibitisho wa ukweli bungeni ili Lema apewe nafasi ya kuwasilisha maelezo yake bungeni katika kipindi hicho cha asubuhi kama alivyoelekeza Spika mwenyewe katika kikao cha tatu. Hata hivyo, Spika alitoa muongozo mpya kuwa Lema awasilishe maelezo na ushahidi wake kwa maandishi ofisini kwake. Katika kikao hicho pia niliuliza swali la nyongeza baada ya majibu ya Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Swali namba 65 ambapo nilihoji kwa kuwa waraka wa kutengua utaratibu wa wahitimu wenye stashahada wenye kupaswa kurudia mitihani michache kufanya hivyo wakiwa kazini ulisambazwa ukiwa umechelewa huku wakitakiwa kulipia ada ya mitihani na kujiandaa je serikali iko tayari kutoa muda wa nyongeza zaidi ya uliotangazwa wa mwezi Aprili? Katika majibu yake naibu waziri alieleza kwamba serikali itatoa muda mwingine wa walimu hao kufanya mitihani yao ikiwa wakishindwa kufanya mwezi Aprili hata hivyo serikali iliwahimiza wafanye hivyo wakati huu ili kuepuka ushindani wa nafasi za ajira utakaokuwepo kipindi kijacho.

Katika kikao cha sita tarehe 15 Februari mara baada ya kauli za Mawaziri ambapo Waziri wa Nishati na Madini alitoa kauli ya serikali kuhusu hali ya umeme nchini na utekelezaji wa miradi ya umeme katika kipindi kifupi na cha kati nilitoa hoja ya dharura kwa mujibu wa kanuni 55 (3) (e) na kanuni ya 47 ili bunge lijadili jambo la dharura la mgawo wa umeme unaolikumba taifa. Nilitaka jambo hilo lijadiliwe kwa kutoa maelezo ya namna linavyowathiri maisha ya wananchi waliowengi na pia kuathiri uchumi wa taifa. Pia, nilieleza kwamba katika kauli yake Waziri ameeleza hatua za dharura zinazotaka kuchukuliwa na serikali ambazo nyingine kimsingi sio za dharura na pia zinahusisha matumizi makubwa ya fedha za wananchi ambazo nilizikadiria kuwa ni zaidi ya bilioni 300 nje ya bajeti ya serikali hivyo ni muhimu bunge likajadili. Spika wa Bunge akaikataa hoja hiyo pamoja na kuwa iliungwa mkono na idadi ya wabunge inayohitajika badala yake akanitaka kama Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nikazungumzie mambo hayo kwenye kikao cha kamati husika hapo baadaye. Kimsingi nilitaka suala hilo lijadiliwe kwa sababu katika maelezo yake Waziri alitaja kuwa serikali inakusudia kukodi mitambo ya dharura ya MW 260 (hii ni mitambo ambayo gharama yake ni kubwa sana, na inaweza kuchelewa isije wakati wa dharura kama ilivyokuwa kwenye sakata la Richmond), pia Waziri hakuzungumzia kabisa kuhusu mitambo ya Dowans ambayo asubuhi ya siku hiyo nilizungumza LIVE na TBC1 na kutaka serikali iitaifishe mitambo husika kwa kutumia sheria ya uhujumu uchumi na sheria nyinginezo ili iiwashe kwa dharura na kupunguza pengo la MW 120 wakati taifa likiendelea kufanya maamuzi ya namna ya kufidia kiwango kitachobaki. Aidha mjadala huo ungewezesha pia kutaka waziri awajibike kwa kutochukua hatua za mapema za kukabiliana na kinachoitwa dharura ambacho kilishafahamika toka mwaka 2006, 2008 na 2009 na maamuzi ya kuondokana na hali hiyo yakafanyika lakini hayakutekelezwa kwa wakati ( Bonyeza hapa kwa kauli ya awali kuhusu Dowans na mgawo wa umeme: http://mnyika.blogspot.com/2011/02/mitambo-ya-dowans-itaifishwe-waziri.html)

Katika kikao cha saba tarehe 18 Februari niliuliza Swali la Nyongeza kutokana na majibu ya Swali namba 85 kwa Wizara ya Maji. Kwenye swali langu la Nyongeza kwanza nilimkosoa Naibu Waziri kwa kutaja majina ya miradi ya maji ambayo iko Kigamboni na kueleza kwamba ni ya Ukonga na kumweleza Naibu Waziri kuwa pamoja na uwekezaji wa fedha za miradi ya maji za Benki ya Dunia na Wadau wengine wa maendeleo kwenye Ruvu Juu na Ruvu chini ikiwemo kuweka mtandao mpya wa mabomba ya maji maarufu kama mabomba ya wachina; bado maji kwenye kata za Kwembe, Kibamba, Msigani, Mbezi, Saranga, Kimara nk maji hayatoki kwa pamoja na mambo mengine upotevu wa maji na wafanyabiashara wanauza maji bei juu kujiunganishia kinyemela; je Naibu Waziri yuko tayari kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya maji ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa? Naibu Waziri alijibu kwa kunipongeza kwa kuweka kipaumbele cha kwanza suala la maji katika kazi zangu na kuahidi kutembelea miundombinu husika kwa kushirikiana nami. Pia, niliuza Swali namba 91 kwa niaba ya Mbunge wa Mpanda Mjini Said Amour Arfi kwa Wizara ya Fedha kuhusu kero za upatikanaji wa mafao ya wastaafu na mirathi kwa watumishi waliokufa kazini. Baada ya majibu ya Waziri kueleza kwamba sababu ni matatizo ya mawasiliano ukiwemo udhaifu katika mfumo wa kumbukumbu kwa upande wa watumishi wanaohudumiwa na mifuko; niliuliza maswali mawili ya nyongeza, moja kuhusu namna ambavyo serikali imepanga kuondokana na matatizo hayo ya mawasiliano na kumbukumbu hasa kwa kuwa wapo wastaafu na marehemu ambao kumbukumbu zao zote zimekamilika lakini bado kuna kero nyingi katika kupata mafao na mirathi. Pili, niliuliza swali la kutaka tamko la serikali kuhusu wastaafu wengine ambao hawahudumiwi na mifuko kama wale wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki ambao mpaka sasa wanahangaika kuhusu mafao yao. Serikali ilijibu kuwa haina tamko la kutoa kwa sasa kwa kuwa inasubiri kwamba suala la Wastaafu wa Afrika Mashariki lipangiwe jaji mwingine katika mahakama ya rufaa kama walivyoomba.

Kwa muktasari huo ni mrejesho kuhusu ushiriki wangu ndani ya vikao vya mkutano wa pili wa bunge la kumi. Hata hivyo, kuna masuala mengine yanayohusu ushiriki wangu katika shughuli nyingine za kibunge nje ya vikao kwa nafasi zangu zingine kama Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CHADEMA, Katibu wa Wabunge wa Mkoa wa Dar es salaam, Mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, Mjumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo, Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani-Nishati na Madini na nafasi nyinginezo ambayo sijayaeleza katika taarifa hii. Nawashukuru sana wote walitoa maoni kwenye Mikutano ya Mbunge kuwasikiliza na kuzungumza na Wananchi tuliyoifanya Mbezi mwisho na Manzese Bakhresa siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano wa pili wa bunge, sehemu ya masuala mliyonituma nimeyawasilisha. Hata hivyo yako mengine kutokana na ufinyu wa muda na kubanwa na kanuni sikupata wasaa wa kuyawasilisha ikiwemo suala la hoja ya mchakato wa katiba mpya ambalo nililitolea kauli ya tahadhari baada ya serikali kukubaliana nami mchakato husika kuanzia bungeni kwa kutungwa kwa sheria (Rejea kauli yangu ifuatayo: JOHN MNYIKA: Tahadhari kuhusu serikali kupeleka muswada wa katiba mpya bungeni). Nawashukuru kwa kuniunga mkono.

Tuendelee kuwasiliana, kushauriana na kushirikiana.

Wenu katika utumishi wa umma,

John Mnyika (MB)

Hongera sana Mnyika,

Tunaomba utufikishie haya maswala ni muhimu kwa taifa letu:-
a. Serikali ina plan gani na kupunguza matumizi yake kwa sasa hasa ukichukulia hali ya maisha ni ngumu sasa?

b. Serikali ina plan gani na Umeme hasa ukipima hili tatizo ni kubwa sasa, vile vile maendeleo ya kutafuta long term solution ya umeme yanaendeleaje? Vilevile watuambie walilinganisha plan zao za kujenga nuclear plant na kujenga hydro electric plant mto Rufiji, Kiwira Coal Plant and Wind Farm energy?

c. Je serikali ina makusudio gani kupambana na kuporomoka kwa maadili ya kazi serikali ambapo Rushwa imeonekana na sehemu na maadili ya kazi.

Ni hayo kwa sasa na nakutakia kila la kheri usisahau kuwakatia kidogo zile milioni 90 za mkopo wa gari wananchi wako wa Ubungo na vile vile wahanga wa Gongo la Mboto.
 
Hongera sana Mkuu kwa utendaji wako mzuri ndani ya Bunge hili pamoja na vipingamizi vingi toka kwa spika. Wengi tunajivunia utendaji wako na kufuatilia kwa karibu michango yako ndani ya Bunge. Yale ambayo umeshindwa kuyafuatilia katika kikao kilichomalizika hivi karibuni kutokana na ufinyu wa muda bila shaka utaweza kuyafuatilia katika kikao kijacho kitakachoanza April 5th, 2011.
 
Barua ndefu. Tukifanya impact evaluation hapa, hakuna kitu. Chifu, try to accomplish things. And not reiteriating what we have already seen kwenye vikao vya bunge. Come up with ideas and have balls to work with "mafisadi" if you think the cause is worthy it.

And be independent for a minute. Wadau mtaani wanadai whatever Mbowe/Slaa says--John Mnyika doesn't even question it, anatekeleza tu.
 
Hakika ni mwakilishi makini, Songa mbele mheshimiwa tunahitaji mabadiriko makubwa katika nchi yetu na natumai wawakilishi wa aina yako kuna fursa ya kupatikana mabadiriko tunayotarajia TZ. Hongera!!!
 
Mheshimiwa,

Tunataka upeleke drafted bills and bold proposals on policy, sio maswali ya miongozo ya spika na kukosoa semantics za hotuba za mawaziri kuwa bomba la maji limepita Ukonga sio Kigamboni. Wewe una propose suluhisho gani la maji, achilia mbali mawazo ya waziri.

Aidha kusema Rais anapoongelea au kukemea udini ndio anachochea udini kwa sababu "umekaa vijiweni" na kuona hakuna udini ni kuwa nje ya mguso. Udini upo na unaota mizizi. Ongea na wafanyakazi wa mashirika ya Umma hawaishi malalamiko kwamba meneja wa dini fulani anaajili wa dini yake. Soma JF utaona udini unavyonuka humu, kila teuzi zinahojiwa kidini.

Mtu aliyeshinda kijiweni kipaumbele chake cha siku ni kupata hela ya ugali na dagaa, hana muda na udini. Lakini kwa upwardly mobile segment of society udini unawahusu. Utasemaje Tanzania hakuna udini?
 
Mh. John kwanza pole kwa kazi ngumu ya uwakilishi lakin pia nikupongeze kwa ushindi ulioupata jimbon ubungo pamoja na hujuma za ccm. Nami naendelea kuwashauri wabunge wote wa cdm kuwa shikamaneni kwan ni nyinyi tu wananchi waliowengi wanawategemea, msikate tamaa pamoja na hujuma zinazofanywa na ccm na cuf. Tumeona kwenye mlipuko wa mabom hawataki muwe covered na vyombo vya habari. Laki still peoples power is behind you. Keep it up, advice your fellow to use the same method as u did but talk to people openly too. Be blessed
 
Mnyika watu tunakukubali sana; mwangalie sana mwenyekiti wa kamati yako; mwizi yule; mwangalie asije akakuambuzika; pia kuna ushauri mwingi tumeuona; na akukosoae anakuongezea nguvu yakesho
Mhimu songa mbele na ufikirie nje ya box sasa ili hata yale makubwa aliyoyatamka Dr Slaa yaeleweke kwa ufasaha ili kuwafikirisha zaidi watanzania kuwa na uamuzi sahihi kwa kila hatua wanayopiga; ili kwa kweli hatuwezikujua unaweza kuwa mwokozi wetu ambao tuna elimu ila sio wana siasa; na wasio na elimu na si wanasiasa; pigana na katika ukweli Mungu yu pamooja nae; Spika yule mchukulieni alivyo ila drive her hardly; wananchi wameshajua kwa nini alichaguliwa maana niliona mpaka anataka urafiki na wewe (refer anaona kuliko mchezaji) lakin naamini unafiki kwako mwiko mwisho wa siku tutaona matunda yako
Asante sana
 
Nakupongeza sana kwa michango ya bungeni, naomba uchangie kidogo na humu JF (mkono mtupu haulambwi) ili uwe premium member.
 
Back
Top Bottom