emaJenerali
Member
- Mar 7, 2014
- 11
- 1
BUNGE Maalum la Katiba limeahirishwa Aprili 25, kupisha Bunge la Bajeti ambalo linataraji kuanza mwezi wa tano mwaka huu.
Bunge hilo Maalum la Katiba limeahirishwa huku kukiwa bado hakuna mwelekeo wa kupatikana kwa katiba ambayo kwa mujibu wa ratiba, Katiba ya Watanzania ingetakiwa ikamilike ndani ya siku sabini (70) au nyongeza ya siku 20 ambazo zinakamilisha siku 90, kama kazi hiyo haitakuwa imekamilika katika siku zilizokuwa zimetarajiwa.
Kwa mujibu wa sheria za nchi inampa mamlaka Rais kuongeza muda kwenye Bunge Maalum la Katiba endapo muda uliotarajiwa hautatosha ambapo Rais ameongeza tena siku nyingine 60 za Wajumbe kukamilisha kuipata Katiba mpya.
Lakini pamoja na Rais kuongeza muda, bado hakuna dalili zinazoonesha kwamba katiba inayo tarajiwa na wananchi itapatikana ilehali tayari mipasuko ndani ya Bunge hilo imesha jitokeza tukishuhudia baadhi ya vyama na makundi yakitoka nje kuashiria kutoridhika na mchakato unaoendelea ndani ya Bunge.
Kuna dalili za wazi zinazoonesha kwamba huenda zoezi hili la kuipata Katiba Mpya lisifanikiwe kwa wakati, au hata likifanikiwa huenda lisitimize matarajio ya wengi kutokana na kuchakachuliwa kwa Rasimu ya Katiba ambayo ndiyo maoni ya wananchi.
Kwa matokeo hayo, tayari vyama vya siasa vinarushiana mpira, Chama tawala kinalaumiwa kinachelewesha mchakato wa Katiba ili Katiba ya zamani iendelee kutumika kwenye uchaguzi wa 2015 kwa vile Rasimu ya sasa inayojadiliwa ikipita itakibana Chama tawala hasa kwenye upande wa Madaraka.
Vyama vya upinzani navyo vinalaumiwa kwamba hawataki marekebisho ya rasimu ya Katiba iliyoletwa Bungeni kutokana na kung'ang'ania muundo wa serikali tatu kwa sababu Muundo huo utavinufaisha vyama vya upinzani kwenye suala la Madaraka. Hizi zote ni tuhuma ambazo vyama vya siasa vinarushiana vijembe kuhusu muundo wa Serikali.
Yote tisa.... Nyongeza ya siku 60 walizopewa wajumbe bado ni mzigo kwa wananchi wengi wa hali ya chini. Kwa mahesabu ya haraka kama Wajumbe wote 630 watalipwa posho ndani ya siku 60 watatumia zaidi ya Bil. 20 za Kitanzania, fedha ambazo ni nyingi ukilinganisha na umaskini tulio nao Watanzania.
Fedha hizi kama zingepelekwa kwenye Bajeti ya wizara ya Elimu ambayo ina matatizo lukuki, zingeweza kutatua matatizo yanayoiandama Wizara ya Elimu, mfano uhaba wa shule, maabara, mishahara ya waalimu nakadhalika.
Kwa upande mwingine wa shilingi, fedha hizi si kitu kama Katiba inayotarajiwa na wananchi wengi itapatikana. Katiba ambayo itatatua matatizo ya muda mrefu yanayo waandama wananchi. Katiba ambayo itawaleta watanzania pamoja, katika makabila yao, dini zao, rangi zao, na hata hali zao za kipato. Katiba ambayo italeta maendeleo ya Pamoja.
Aidha, Bunge Maalum litakapo rejea mwezi wa nane halina budi kuunda Tume huru itakayoshughulikia tuhuma zinazoibuliwa na vyama vya siasa. Kwa mfano kuna tuhuma mbalimbali zimeripotiwa na vyama vyama vya siasa ambazo ni nzito kiasi kwamba zinatishia mustakabali wa kupatikana kwa Katiba Mpya.
Kuna masuala ya msingi ambayo yanahitaji kuwepo kwa Tume huru ambayo, Tume hii itakuwa na kazi ya kuchunguza tuhuma zinazo ibuliwa na wanasiasa, vyama vya upinzani, hata vikundi mbalimbali ndani ya Bunge na kuyafanyia uchunguzi wa kina na kuja na jibu ambalo litaondoa mikwaruzano ndani ya Bunge.
Kwa mfano, kuna baadhi ya tuhuma ambazo zimeripotiwa lakini hakuna ufafanuzi wowote au uchunguzi uliofanywa kudhibitisha tuhuma hizo. Tuhuma zilizoripotiwa ni kuhusu Chama tawala (CCM) kulaumiwa na vyama vya upinzani kwamba wamekuwa wakichakachua maoni ya wananchi yaliyo pendekezwa na Tume ya Warioba na tayari chama hicho kimeshatengeneza rasimu yao ambayo inatekeleza matakwa ya Ilani ya chama.
Tuhuma kama hizi zinawafanya baadhi ya Wajumbe kutoelewa lipi ni sahihi linalo ongelewa. Lakini sio tu kwa wajumbe, pia wananchi wanaofuatilia kwa karibu mchakato wa Katiba wanataka waelewe matokeo ya ripoti za uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazoibuliwa Bungeni.
Zipo pia tuhuma zinazoelekezwa kwa vyama vya upinzani, kwamba wanataka serikali tatu zipite ili wahalalishe ushoga na udini, ukabila, pamoja na tuhuma nyingine ambazo zimesababisha mivutano ndani ya Bunge.
Kwa hiyo, Tume huru itakayo patikana itakuwa si tu inatolea ufafanuzi bali itakuwa ni muhimili wa maridhiano ndani ya Bunge.
Tukiachana na hayo, Bunge la Bajeti linaanza vikao vyake Mei 6 Mwaka huu. Ni wakati wa kushuhudia baadhi ya bidhaa ambazo zinawalenga wananchi zikipaa kwa maana kwamba ongezeko la kodi kiasi cha kuhatarisha maisha ya watumiaji ambao ni wananchi wa hali ya chini.
Imekuwa ni jambo la kawaida kusikia bidhaa kama Petroli, diseli, mafuta ya taa ambayo ndio muhimili wa bidhaa ambazo zinatumiwa na wananchi wengi kwa namna moja ama nyingine zikipandishiwa kodi na kusababisha bidhaa nyingine nazo kupanda bei.
Kwa mfano, Kupanda kwa ushuru wa Petroli kwenye bajeti ya serikali ya mwaka 2013/2014 kumesababisha baadhi ya bidhaa na huduma nazo kupanda bei. Mfano wa bidhaa za vyakula, bidhaa kama nguo, bidhaa za nyumbani (farniture) huduma za usafiri, kodi za nyumba, huduma za vyakula mfano migahawa, Hotelini nakadhalika. Adha ambayo kwa asilimia kubwa inawakumba wananchi wa hali ya chini.
Bajeti ya serikali ya mwaka 2013/2014 tulishuhudia baadhi ya bidhaa muhimu zikipandishiwa ushuru ambapo ongezeko la ushuru lilizikumba baadhi ya bidhaa kama mafuta ya diseli kwa asilimia 2, mafuta ya petroli, pamoja na mafuta ya taa.
Pia, kupanda kwa ushuru kwenye huduma za simu za kiganjani (Mobile phone service) kwa asilimia 14.5, Ongezeko la ushuru kwa asilimia 15 kwenye samani zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, Ushuru wa bidhaa kwenye huduma za simu za mezani (zinazojulikana kama simu za TTC), bidhaa zisizokuwa za mafuta kama vile vinywaji baridi, mvinyo, pombe, vinywaji vikali, sigara kwa asilimia 10.
Bidhaa nyingine zilizopandishwa ushuru, ni pamoja na magari yasiyo ya uzalishaji (Non-Utility Motor Vehicles) kutoka asilimia 20 hadi 25, viwango vipya vya magari ya uzalishaji ((Utility Motor Vehicles) kwa asilimia 5, bidhaa mbalimbali zinazozalishwa au kuingizwa nchini kama vile Mazulia, vipodozi, mafuta ya kujipaka, bidhaa na mifuko ya ngozi, bunduki na risasi, boti za kifahari, ndege na helikopta kutoka asilimia 10 hadi 15.
Ongezeko ambalo kwa namna moja ama nyingine mzigo wa kupanda kwa ushuru unakwenda moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida.
Kwa hiyo, ongezeko la ushuru wa bidhaa kama wa magari, huduma za simu ya kiganjani na zile za mezani, bidhaa zisizokuwa za mafuta kama vile vinywaji baridi, bidhaa zinazozalishwa au kuagizwa nchini pamoja na bidhaa za mafuta kama Petroli, kwa namna moja ama nyingine zimelazimisha bidhaa nyingine nazo kupandisha ushuru wake.
Mikakati ya kukabiliana na changamoto ziimarishwe kwenye bajeti kuu 2014/2015
Katika bajeti ya serikali ya 2013/2014, serikali iliweka mikakati ya kukabiliana na changamoto hasa kwenye sekta ambazo zinawagusa moja kwa moja wananchi walio wengi, kwa mfano kwenye sekta ya Kilimo serikali iliweka mikakati ya kuboresha mfumo wa kilimo kutoka kwenye kilimo cha mazoea kwenda kwenye kilimo chenye tija.
Aidha, uvuvi na ufugaji ulitafsiriwa uwe wa kibiashara badala ya ule wa kujikimu. Kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji, kuongeza upatikanaji na utumiaji wa pembejeo za kilimo, kuimarisha huduma za ugani, upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, kusimamia upatikanaji wa masoko, na kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya kilimo.
Mikakati mingine ya kukabiliana na changamoto katika bajeti ya serikali 2013/2014 ilikuwa ni kudhibiti matumizi ya fedha za umma ambapo ni pamoja na kuwajengea uwezo watumishi wa kada za uhasibu, ununuzi, uhakiki mali na wakaguzi wa ndani.
Kudhibiti mfumuko wa bei kwa kuhakikisha kwamba uzalishaji na usambazaji sawia wa mahitaji muhimu kama vile chakula, mafuta ya nishati, sukari, vifaa vya ujenzi na huduma za usafiri. Pia katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi. Bajeti ilisema, Serikali itaimarisha kamati za kisekta za kuratibu mifumo ya kuhimili na kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Kuongeza makusanyo ya mapato, hasa ya ndani kwa kuanzisha vyanzo vipya na kuboresha vilivyopo. Lengo likiwa ni kujitosheleza kwa mapato yatakayowezesha kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi.
Pia bajeti hiyo, inaendelea kuboresha miundombinu ya kiuchumi, kifedha na kijamii ili kuongeza fursa za ushiriki wa wananchi katika uzalishaji na kuboresha hali zao za maisha.
Kwa hiyo, kutokana na mikakati ya kukabiliana na changamoto kwenye sekta mbalimbali katika bajeti ya 2013/2014 serikali haina budi kutenga kiasi cha kutosha kwenye miradi na mipango ya maendeleo kwenye bajeti ya mwaka 2014/15 ili maendeleo ya haraka yawafikie wananchi.
Ukitazama bajeti ya 2013/2014 kiasi cha shilingi trilioni 5.67 tu, ambacho ni sawa na asilimia 31.9, kilitengwa kwenye miradi ya maendeleo, fedha ambazo ni kiasi kidogo ukilinganisha na mipango ya maendeleo iliyotazamiwa.
Aidha, Mkakati wa Matokeo makubwa sasa (BRN), utafanikiwa kama serikali itaona umuhimu wa kutenga kiasi cha kutosha kwenye mipango ya maendeleo ili kufanikisha azma ya Matokeo Makubwa katika wakati ulio kusudiwa.
Mikakati ya kukabiliana na changamoto kwenye sekta mbalimbali utafanikiwa kama serikali itatafuta vyanzo vya kuaminika vya mapato kuliko kutegemea ushuru bidhaa ambazo kwa kiasi kikubwa huwaathiri wananchi hasa wale wa kipato cha chini.