Bunge la Bajeti laiua kabisa CCM

Bunge la Bajeti laiua kabisa CCM

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,605
Reaction score
551
Ni jambo la wazi kwa sasa kuwa bunge limekuwa ni tanuru la moto la kuchoma magamba ya CCM.

Kuanzia Spika(Makinda), Naibu spika(Ndugai), Katibu mkuu wa CCM(Kinana), Naibu katibu wa CCM(Mwigulu) hadi mwenyekiti wa CCM(Kikwete) na baraza lote la mawaziri, wote wamevuliwa nguo na kuingia aibu baada ya CHADEMA kuwaumbua watu hao ndani ya bunge la bajeti.

Kwa sasa hata TBC inapata wakati mgumu kurusha matangazo ya bunge 'live' kwani yamekuwa sumu ya kuia CCM kijamii na huku yakiipandisha Chati kisiasa CHADEMA.

Hapo kabla alipangwa kuwa bunge lisirushwe tena 'live' lakini kelele za wadau zikawafanya waogope na kusitisha mpango huo. Kwa sasa ni TBC pekee ndio wamepewa ruhusa ya kurusha matangazo ya bunge na wakati huo huo TBC inaonekana mikoa michache na kwa sasa haionekani kwa baadhi ya mikoa iliyokuwa inatumia Satelite kuona TBC. Na mara kadhaa TBC imekuwa akikata matangazo ya bunge pasipo sababu hususani pale CCM na washirika wake wanaporaruliwa.

Ni juzi tu, Naibu spika wa bunge, Job Ndugai amakaririwa akisema kuwa hatawagusa tena wabunge wa CHADEMA kwa kuwa kila akifanya hivyo wabunge hao wameonekana mashujaa mbele ya jamii na yeye kuambulia aibu kutoka kwa wananchi na jamii kwa ujumla.
 
Napita tu japo kama unafuatilia bunge unatajua hii ni habari ya kishabiki tu
 
Serikali ya CCM imevaa miwani ya mbao (Deo Filikunjombe-CCM). Serikali ya CCM mmeshindwa kulinda tembo wetu, hadi lugha ya Kiswahili? (Joseph Mbilinyi-CHADEMA). Mawaziri na baadhi ya viongozi wakubwa ndani ya CCM wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya nchini. (Kangi Lugola-CCM) Sitawagusa tena wabunge wa CHADEMA maana vyombo vya habari vinawapamba na kunilaumu mimi (Job Ndugai-Naibu Spika) Nadhani mlolongo huo hapo juu unajieleza kuhusu mwelekeo wa CCM
 
Tatizo lililopo ni kuwa wabunge tulionao hawajui kuwa kazi ya bunge ni kuisimamia serikali Ugumu unakuja pale kila mbunge anapogeuka kuwa waziri au naibu waziri kama si msemaji wa chama badala ya mtetezi wa wananchi wake dhidi ya vitendo viovu

mi nadhani ni bora kila mbunge atambue wajibu wake kwa taifa lake
 
Kinana ameliteka Bunge na vitendo vyake viovu vya kuua bila huruma tembo wetu
Ingelikuwa zama za manabii basi Kinana pengine angelaaniwa na angeota pembe za ndovu mwili mzima hapo magamba ndio mngeamini kama Mheshimiwa Kinana ni kweli Muuaji wa Tembo wetu,
Lakini kadiri siku zinavyoenda sura yake inabadirika na kuwa kama rusra te ndovu KINDA si haba
 
Hivi ni nani anatakiwa kuongoza mapambano ya kudai haki ya uhuru wa kupata habari za bunge kwa wananchi? Maana nadhani huku kulimt eti TBC peke yake ndio wanaotakiwa kurusha matangazo ni kuwanyima wananchi haki ya kupata habari...
 
Serikali ya CCM imevaa miwani ya mbao (Deo Filikunjombe-CCM). Serikali ya CCM mmeshindwa kulinda tembo wetu, hadi lugha ya Kiswahili? (Joseph Mbilinyi-CHADEMA). Mawaziri na baadhi ya viongozi wakubwa ndani ya CCM wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya nchini. (Kangi Lugola-CCM) Sitawagusa tena wabunge wa CHADEMA maana vyombo vya habari vinawapamba na kunilaumu mimi (Job Ndugai-Naibu Spika) Nadhani mlolongo huo hapo juu unajieleza kuhusu mwelekeo wa CCM
Ongezea quote nyingine hii,wabunge wa CCM,tumesahau wajibu wetu wa kuisimamia serikali,badala yake tumekuwa wapiga propaganda wa CCM, swali kama sisi wabunge wa CCM,tutafanya kazi za Nape Nnauye,sasa tunataka Nape Nnauye,asiwe na kazi ya kufanya?!

By Deo Filikunjombe,mbunge wa Ludewa.
 
Wabunge wa CCM,kutumia mbinu ya kuwatukana wabunge wa CDM,wanazidiwa hoja na CDM.

Mifano, Serukamba,Juma Nkamia na Lusinde,ni dhahiri kuzidiwa nguvu na hoja za CDM.

Hiyo haina tofauti kwa timu 2 za mpira wa miguu zinapokuwa uwanjani,timu itakayokuwa inacheza rafu zaidi ni ile timu ambayo itakuwa imezidiwa kwa kila hali kimchezo.
 
chadema ni mwiba.....imewafanya wabunge wa ccm kuwa kama mawaziri naku tetea serekali kila kukicha.....
wapunge wa ccm hawawakilishi wanachi wao. hilo nalo limepa chati chadema
 
CCm kupambana kuwaangusha wabunge makini wa upinzani kama vile Tundu Lisu ili aingie mtu wa CCM ni kujiangusha wenyewe. waangalie kama mbunge anafanya kile wananchi wapendacho wamwache aendelee wasubiri uchaguzi mkuu. kupinga hoja nzuri za upinzani pia ni kujiangusha. CCM may contain the seed of its own destruction
 
Tatizo lililopo ni kuwa wabunge tulionao hawajui kuwa kazi ya bunge ni kuisimamia serikali Ugumu unakuja pale kila mbunge anapogeuka kuwa waziri au naibu waziri kama si msemaji wa chama badala ya mtetezi wa wananchi wake dhidi ya vitendo viovu

mi nadhani ni bora kila mbunge atambue wajibu wake kwa taifa lake

Bunge limezidiwa na uzee.
 
Napita tu japo kama unafuatilia bunge unatajua hii ni habari ya kishabiki tu

Mleta mada hafuatilii bunge kabisaaaa, kama ni kufa basi hili bunge limekimaliza CHDEMA, wameonesha udhaifi mkubwa sana wa kuongoza kambi ya upinzani
 
Naona mmeanzisha uzi wa kujifariji baada ya ule wa namna hii unaosema bunge la bajeti chadema imefia hapo
 
Kambi ya chadema bungeni imejimaliza na kukimaliza chadema kwa ujumla...saivi ukipita mitaani wanasema chadema ni cha wahuni na wafanya vurugu...hatuwataki
 
CCm kupambana kuwaangusha wabunge makini wa upinzani kama vile Tundu Lisu ili aingie mtu wa CCM ni kujiangusha wenyewe. waangalie kama mbunge anafanya kile wananchi wapendacho wamwache aendelee wasubiri uchaguzi mkuu. kupinga hoja nzuri za upinzani pia ni kujiangusha. CCM may contain the seed of its own destruction

Sdhani kama wamekosea kama kuna kweli kuna taratibu zimkekeukwa, haki ya mtu inapiganiwa bila kujali gharama, ni bora CCM wakaachwa waendelee na mchakato wao na ukweli utajulikana huko kunakotafutwa haki.
 
Naona mmeanzisha uzi wa kujifariji baada ya ule wa namna hii unaosema bunge la bajeti chadema imefia hapo

Hivi inawezekana hii ni tabia ya CHADEMA ya kuwageuzia wengine kibao, tunaona suala la USHOGA wanavyojaribu kuwageuzia CUF wakati kila mtu anajua wao ndiyo washika dau wa ushoga. Inasemekana hata mdogo wa kiongozi mkubwa ndani ya CDM USHOGA ndiyo shughuli zake huko majuu.
 
Back
Top Bottom