Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

"Napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Usalama Barabarani, Sura 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati wa uendeshaji gari barabarani kutoka Sh20, 000 hadi Sh50,000" alisema.

Nani msemakweli - maneno ya mdomoni ya waziri Mkulo au taarifa iliyoandikwa na yeye mwenyewe? Ina maana hakusoma kilichoandikwa; je achukuliwe hatua gani?
84. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Usalama Barabarani, Sura, 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati wa uendeshaji gari barabarani (Traffic Notification Fee) kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 300,000.
 
Shukrani mzee wa rula..ngoja nasi tuifanyie upembuzi yakinifu!
Natumai mwaka huu hakukuwa na bajeti mbili kama mwaka jana ( Ya wafadhili na sie wadanganyika)
Katu Mkulo hawezi kurudia ujinga ule, yaani bajeti ya wafadhili na Watanzania! Iliwagharimu sana kusafisha kote kote kwa wananchi na wafadhili.
 
Mmmmh ila mazee hii itakuwa noma, nakubali kima hiki kiwe 50,000/= ili angalau madereva wafuate sheria za usalama barabarani, kumekuwa na upotevu wa maisha na maisha y watu kwa uzembe wa baadhi ya madereva, ila swala la rushwa nalo litaondoa kabisa maana ya kuwawajibisha madereva wazembe.
 
duh! shukrani mkuu, mwaka huu maasi ya utoaji mimba nadhani yatazidi kwa kasi zaidi .
 
To me this does not make sense,mmiliki wa vitz akitanua alipe faini 50,000 na mmiliki wa basi aliyesimamisha abiria 20 let us say wanaenda mwanza kwa sh.30,000@ which gives him 600,000/= naye alipe hiyo 50,000,mmiliki mwenye lori lenye mzigo worth 200million naye alipe same amount....is this fair...kama wameamua basi waseme hii 50,000 ni minimum amount,then tuwe na viwango tofauti vya juu kutegemeana na kosa lenyewe au makundi ya gari husika.
 
duh! shukrani mkuu, mwaka huu maasi ya utoaji mimba nadhani yatazidi kwa kasi zaidi .
Kwa nini umesema hivyo mkuu? Au unakusudia kwa sababu ya ugumu wa maisha? Usishauri watu wafanye hivyo hata kama kweli maisha ni magumu kwa sababu kufanya hivyo ni dhambi.
 
Ngoja nifuatilie namna ya kuhamia utrafic maana apo kam rushwa lazima iwe kuanzia wekundu!
Labda Mkulo na CCM wameamua kuboresha maisha ya polisi kimtindo!
 
Nani msemakweli - maneno ya mdomoni ya waziri Mkulo au taarifa iliyoandikwa na yeye mwenyewe? Ina maana hakusoma kilichoandikwa; je achukuliwe hatua gani?
84. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Usalama Barabarani, Sura, 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati wa uendeshaji gari barabarani (Traffic Notification Fee) kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 300,000.
katamka 50,000 lakini hotuba imechapwa 300,000 ukweli tutaujua kwenye majadiliano...tatizo sio faini ni namna ya utekelezaji wake unaotoa mianya ya bribery,mbona Majembe+Sumatra was doing the same thing wakaona hawapati pesa wakasimamisha zoezi na sasa wamekuja upya ili wazidake wao.
wawe na mashine kama zile za Electronic Fiscal Device ili ukilipa notification iende moja kwa moja TRA/Hazina na uweze kwenda kuverify ticket yako kama inavyofanyika kwenye VAT returns
 
Kwa nini umesema hivyo mkuu? Au unakusudia kwa sababu ya ugumu wa maisha? Usishauri watu wafanye hivyo hata kama kweli maisha ni magumu kwa sababu kufanya hivyo ni dhambi.

mkuu hiyo ni dhambi kubwa na wala simshauri mtu afanye hivyo, but believe me, ndivyo itakavyokuwa.
 
Mapato
Ndani=7tr
Mikopo/Misaada=6tr

Matumizi
Kawaida=8.6tr
Maendeleo=4.9tr (Kati ya hizi ni 1.8tr tu ndio zinatoka ndani!!)

Kazi ipo....
 
tehe tehe tehe mkuu mtu huwa haulizwi habari za unakokwenda bali huachwa aende kwanza na akirudi ndio huulizwa habari za utokako...ukisharudi nishtue nikujulie hali mkuu za huko ulikotoka lol
Ha ha ha! fananisha mimi kuhama CCM ni sawa na kuhama YAanga....haiji yani.
 
Mapato
Ndani=7tr
Mikopo/Misaada=6tr

Matumizi
Kawaida=8.6tr
Maendeleo=4.9tr (Kati ya hizi ni 1.8tr tu ndio zinatoka ndani!!)

Kazi ipo....
Kwa maana nyingine toka tupate uhuru nchi haijaweza kujitegemea hata kwa matumizi yake ya kawaida! 8.6tr - 7tr = 1.8 deficit. Ina maana ukishindwa kuwachekesha wahisani wakacheka basi hiyo 1.8tr hupati hivyo the whole bajeti kuwa fyongo! Halafu hao hao jamaa wanapigana kishenzi bado kuendelea kuiongoza nchi! Mimi naona bora tupate wawakilishi wengine haijalishi kama watakuwa CDM u CUF bora nao tuwaone watachezaje hiyo sindimba ya bajeti na zoezi zima la kumkomboa mwananchi katika lindi la umaskini?
Kwa maana nyingine the whole prosess of development lipo chini ya wahisani, kwa namana hii nchi wahisani zitafanya zitakavyo!
 
Na zaidi ya hapo tunachangia 30% tu kwenye bajeti ya maendeleo..nyingine tunasubiri wahisani! Huu ni utani...
 
Somo hiki kifungu cha bajeti na ufikirie kwa makini wewe mwenyewe. Ila zingatia angalau maswali ya je hiki kifungu kina maana gani? na je chanzo chake ni nini haswa?

B. Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332
77. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332 kama ifuatavyo: -
i)Kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa Serikali na wanaofanya kazi kwenye Taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya Serikali.
 
Back
Top Bottom