Bunge la anza kesho Dodoma - je muswada wa fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii vipi?

Mimi nimekuwa nafatilia jambo ili kwa ukaribu sana, nilimsikia mbunge wa jimbo la Ubungo akisema "hatua zinazotakiwa kuchukuliwa na wafanyakazi na watanzania wengine ni kuwezesha RAIS wetu JK kuingilia kati kabla ya mkutano wa bunge kuanza Oktoba 31, ambayo ndo kesho! Je kuna hatua gani rais kafanya? Na tukumbuke kuwa yeye ndiye aliyeweka sahihi ili sheria kulipwa baada ya miaka 55 ianze kutumika.
 
Sijajua shirikisho la vyama vya wafanyakazi katika nchi hii wamechukua hatua gani katika kuhakikisha haki za wafanyakazi kuhusu mafao yao zinatekelezwa. Kama wafanyakazi wenyewe hawatasimama na kujitetea basi wasimlaumu mwingine bali wao wenyewe kwa kukubali kunyanyaswa kwasababu ya wao kutokuwa na umoja!!!!!!

Wanachama wengi waliopo kwenye haya mashirikisho ni waajiriwa wa serikali hivyo wengi wao wana ajira ya kudumu na kitu viongozi wake wanachojua haki yao ni kulalamika kuhusu nyongeza ya mshahara na posho bila kujua ipo siku hali itabadilika redundancy zikachukua nafasi
 
KAMA KUNYENYEKEA WATANZANIA TUNA ONGOZA. hakuna cha kuwaonea haya wabunge wetu, kama hawataki kutufanyia kazi basi tuwatoe hata kama ikibidii kubadirisha katiba. NGOJA NGOJA, HUUMIZA MATUMBO!!!
 
Mimi nimekuwa nafatilia jambo ili kwa ukaribu sana, nilimsikia mbunge wa jimbo la Ubungo akisema "hatua zinazotakiwa kuchukuliwa na wafanyakazi na watanzania wengine ni kuwezesha RAIS wetu JK kuingilia kati kabla ya mkutano wa bunge kuanza Oktoba 31, ambayo ndo kesho! Je kuna hatua gani rais kafanya? Na tukumbuke kuwa yeye ndiye aliyeweka sahihi ili sheria kulipwa baada ya miaka 55 ianze kutumika.

Ni kweli mheshimiwa Mnyika alikuwa anahojiwe kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii kwenye StarTV ktk kipindi cha tuongee asubuhi, alinena kwamba hatua zinatakiwa kuchukuliwa mapema. Sikuelewa ni hatua zipi wafanyakazi tuzichukue' je tuendelee kupiga porojo tunapokutanika kwenye viti virefu au kwenye daladala n.k, na je kama ni maandamano nani wakuongoza jahazi ili?
 
Kama ukichunguza utagundua ya kwamba, Wabunge ni waowao wanaopata mishahara minono kuliko wote, wabunge ni wao wao wanaopata mikopo minono kuliko wote, wabunge wao wao wanaongoza kwa kufanyia kazi mahali penye usasa na usafi kuliko wote; wabunge waowao waliingiza kuitana waheshimiwa kwa faida zao; wabunge waowao wanakaa kimya kutochukua hatua huku wakiona madaktari na wagonjwa wakiteseka; wabunge waowao wanakubali kukaa kimya huku wakiona reli yetu ikielekea kufa! BASI ULE MSEMO WA KUWA AFRICANS ARE JUST LIKE MONKEYS KUNA KA UKWELI FULANI!!!
 
...Wakati kikao cha Bunge kinategemewa kuanza kesho, cha kushangaza wabunge wamedai kuwa hawajui ajenda za kikao hicho na wanaenda kama maboya. Akiongea na ITV mbunge wa Mkanyageni-CUF Mheshimiwa Mnyaa amesewa..ni mara ya kwanza kwenda Dodoma kama maboya wasiojua wanaenda kufanya nini.

My Take:

Hili ndilo bunge linalofanya kazi kwa niaba ya wananchi, sijui katibu wa bunge na wasaidizi wake wanafanya nini.
 
Hajui wanaenda kufanya nini kweli, hajui kama kuna burning issues kama NSSF,mpuuzi sana huyo mbunge hana maana hata kidogo.Nafuu angesema kuwa kikao hiki hawajapewa agenda yoyote though kuna burning issues A,B,C.Navowajua hawa ndugu wataongea mambo yao ya ushuzi eti kamati teule sijui ndogo au kubwa whatever they call it eti kuvujisha siri badala ya kujadili mambo ya msingi na mstakabari wa taifa na usalama wake.Wasipozungumzia NSSF wasirudi uraiani wafie hukohuko Dodoma
 
Spika yuko busy anabadilisha ndege, hivyo hakuna cha kushangaza hapo.
 
Kazi bado ni kubwa, katika mahojiano ya ITV nimeona mbunge moja akilezea kuwa anaenda bungeni kama boya ambalo halina mwelekeo, amelezea kuwa hajui anaenda kufanya nini au ni maswala yapi yatawekwa mezani kuanzia kesho, kwa maana hiyo yawezekana wabunge wengi hawajui utaratibu wa kikao kinachoanza kesho, na kwahiyo basi hawajajiandaa bali ni bendera fata upepo. Je kweli kwa kauli hiyo ya Mh. Mnyaa "kuwa wako kama boya" kuna mikakati ya aina yoyote ya kuwasaidia wafanyaka kurudisha utaratibu wa zamani wa mifuko ya hifadhi ya jamii?
 
Wabunge lazima wapewe hadidu za rejea juu ya kikao husika kama ofisi ya bunge imeshindwa kutoa kwa wakati muafaka ni uzembe wa kupindukia na tunarudi palepale. "Tumefika hapa tulipo kwa sababu ya udhaifu wa rais na upuuzi wa ccm" toka kwa JJ. Mnyika
 
wasilaumu mtu wajilaumu wao wenyewe.wabunge wamekuwa too cheap kiasi cua serikali kuwadharau...kama mnawesa kuunda kamati ya kuwasafisha watu wezi na mkakubali kutumika kipuuzi kiasi hicho nani wa kuwaheshimu...sijawahi kushuhudia Bunge oa kipuuzi kama hili...ni bunge linawajibika kwa serikali..ngoma inayopigwa na serikali ndiyo iinayochezwa na bunge.....Bunge linatoa maelekezo kwa serikali na serikali haichukui hatua yoyote, bunge halichukui hatua ya kuiwajibisha serikali.alafu tutegemee Bunge la namna hii kuheshimika . this is the cheapest parliament ever on earth..with no authority over the executive arm of the state,,wity no power to enforce its decision,,the Bunge that sits in the pockets the corrupts...Hili si Bunge ni Genge la wapiga yowe,wala rushwa, wachumia tumbo,......alSimply Cheap...The country is on sale and nobody cares...tumechagua wabunge wanaoshiriki deal na walarushwa na mafisadi against the wider interest of the country,s sovereign/wananchi....HILI NI Bunge gani hili
 
Kazi bado ni kubwa, katika mahojiano ya ITV nimeona mbunge moja akilezea kuwa anaenda bungeni kama boya ambalo halina mwelekeo, amelezea kuwa hajui anaenda kufanya nini au ni maswala yapi yatawekwa mezani kuanzia kesho, kwa maana hiyo yawezekana wabunge wengi hawajui utaratibu wa kikao kinachoanza kesho, na kwahiyo basi hawajajiandaa bali ni bendera fata upepo. Je kweli kwa kauli hiyo ya Mh. Mnyaa "kuwa wako kama boya" kuna mikakati ya aina yoyote ya kuwasaidia wafanyaka kurudisha utaratibu wa zamani wa mifuko ya hifadhi ya jamii?

Endelea kuwaombea kwa sala zako hao wanaoenda bungeni kama boya.
 
ndugu yangu tanzania bado sana, serikali yetu yenyewe inatia kichefufu, wabunge nao wapowapo tu kama boya alilosema huyu mheshimiwa. Kwa ujumla inaumiza sana kuona mtu anayewakilisha wananchi anasema waziwazi kuwa hajui jambo gani lakufanya, ni sawasawa na mwanafunzi anayekwenda kufanya mtihani na hajui ni somo anaenda kujibia maswali, kwa wabunge wetu ni bora liende tu, yeye posho inaingia, haijalisha anajua au hajui kinachoendelea.
 
Endelea kuwaombea kwa sala zako hao wanaoenda bungeni kama boya.

mkuu, mimi nina amini kuwa Mungu ndiye Mwenye mamlaka yote: uwinguni hata duniani, jambo lolote linawezekana kwa uwezo wake, na si kwa nguvu na akili ya kibinadamu, kwahiyo kesho wakati bunge linaanza tuwe pamoja katika dua itakayoongozwa na spika.
 
Ok jifungie ndani na endelea kuomba.
 
Tuone yatakayojiri. Then tutafanya maamuzi magumu. Kuna wengine wetu tumesha panga kufanya maamuzi magumu ambayo yatakua historia katika nchi hii, kwenye suala la mifuko ya hifadhi ya jamii.

mkuu, kama kuna njia mbala iliyoandaliwa, kama kutakuwa nautofauti na mategemeo yetu, sisi tutaunga mkono juhudi hizo, ingawaje itakuwa ni mahamuzi magumu kama ulivyotujuza... Tuko standby...
 
Hivi yule mama spika alisharudi toka india?...inawezekana kuwa alificha baadhi ya mafaili yenye mipango ya kikao cha bunge wakati aikiandaa safari yake ya tiba INDIA
 
huyo mbunge anataka ajue cha kufanya huko ili iweje...yeye aende aanze kupata allowance yake kuanzia kesho, kula bure kulala bure..kuleni maisha wabunge maisha mafupi
 
Back
Top Bottom