Bunge la anza kesho Dodoma - je muswada wa fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la anza kesho Dodoma - je muswada wa fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii vipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kbm, Oct 29, 2012.

 1. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,964
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wafanyakazi na watanzania wote amka tufanye maombi, ni usiku wa manane sasa! Ili muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria za mifuko ya hifadhi ya jamii ipelekwe bungeni katika mkutano wa bunge ambao utaanza kesho mjini Dodoma na kudumu kwa wiki mbili tu. Je Mh. Jaffo mbunge wa Kisarawe (ccm) atatetea wafanyakazi kwa kasi alioanza nayo au tayari ndiyo hivyo tena? Au ni Mh. Mnyika, mbunge wa jimbo la Ubungo? Au wafanyakazi asubiri mpaka miaka 55? Ndugu wadau naomba tuanze kufanya maombi yatakayotupatia majibu swala hili. Karibu...
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Eti Watanzania wote amka tufanye maombi yatakayotupatia majibu swala hili.
  Utafikiri sheria zinapitishwa au kutopitishwa bungeni kwa kufanya maombi.
   
 3. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Huu ndo uzuzu mwingine na wahali ya Juu, ndo maana nasema Wafanyakazi ndo watakao chelewesha Mageuzi katika nchi hii.
  Maombi ya kazi gani? wafanyakazi wanatakiwa kupambana kwa njia yoyote ile na si kuomba, pesa zi ni za wafanyakazi?
   
 4. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kama kuomba tumeomba sana na maombi yetu mpaka sasa hatujajibiwa toka kwa huyo tumuombae,kuna wakati tunahitaji zaidi ya maombi na wenzetu huamua kuchukua kilicho chao na baadae maisha yanaendelea kama kawaida
   
 5. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Kuna jamaa ananiambia kila siku_'walokole ndio wanaoharibu dunia'....huwa nambishia ila nimeanza kumuelewa sasa....yaani mtu mzima na akili zako unasema tuombe wakati ni haki yetu
   
 6. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,964
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  basi tujaribu maandamano kama yale ya wauni wa mbagala waliochoma makanisa labda tunaweza kufanikiwa.
   
 7. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,964
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kesho kabla ya bunge kuanza itatangulia dua (sala) je kama hao wanaotunga sheria wanaimani kuwa bila ya dua mambo hayawezikuwa sawa bungeni, iweje mimi ninaye amini kuwa kwa nguvu ya Mwenyezi Mungu jambo hili litawezekana.
   
 8. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,964
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mkuu, nimeona umekubali kuwa "kweli God is great" kwenye jamii photo ya mdau Mbuzi Mzee. Kwahiyo unakubaliana nami kuwa kwa nguvu ya Mwenyezi Mungu MAOMBI ni muhimu kuweza kufanikisha jitihada zinazofanya na wabunge wetu kwa kuwatetea wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii, ili Muswada wa marekebisho ya sheria ya mafao ya kujitoa KUWASILISHWA BUNGENI
   
 9. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Yeah..alwayz God is great mkuu,..lakini kwa mambo kama haya ya kuporwa haki zetu na majambazi fulani wa kisiasa...halafu tukae chini na kuanza kuomba_hapo ndio naona tutakuwa hatujafanya sehemu yetu kwenye hili mkuu...ni lazima tufanye kitu kudai hii haki yetu_otherwise haya majambazi yatatupora hii haki yetu na kuishia kwenye matumbo yao na watoto wao...get me now?
   
 10. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Tufanye maombi!! inatakiwa wafanyakazi wagome kwa siku moja tuu,utaniambia kesho yake muswada utapelekwa kwa hati ya dharula!
   
 11. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Ni watanzania pekee duniani wanaweza kufanya maombi tena ya kufunga badala ya kupambana ili kudai haki zao za msingi,...na hapo ndipo wajanja wachache wanapotupigia bao kwa uvivu wetu.
   
 12. Bwaksi

  Bwaksi Senior Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuone yatakayojiri. Then tutafanya maamuzi magumu. Kuna wengine wetu tumesha panga kufanya maamuzi magumu ambayo yatakua historia katika nchi hii, kwenye suala la mifuko ya hifadhi ya jamii.
   
 13. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,964
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kufuatia maelezo yaliyotolewa Oktoba 14, naibu waziri wa kazi na ajira Mh. Mahanga alitoa maelezo kuwa marekebisho ya kurejesha fao la kujitoa yatafanyika mpaka mkutano wa 10 wa bunge wa mwezi Februari mwakani kukinzana na tangazo la serikali lililotolewa, pia kuna mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii ambayo hakuhusishwa kwe marekebisho hayo, mfano: NSSF, PSPF & LAPF. Hapa wakuu hamuoni kuwa tayari wafanyakazi wamegawanywa makundi? Na ni kwa nini mfuko wa Mashirika ya Umma (PPF) tu?
   
 14. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Sijajua shirikisho la vyama vya wafanyakazi katika nchi hii wamechukua hatua gani katika kuhakikisha haki za wafanyakazi kuhusu mafao yao zinatekelezwa. Kama wafanyakazi wenyewe hawatasimama na kujitetea basi wasimlaumu mwingine bali wao wenyewe kwa kukubali kunyanyaswa kwasababu ya wao kutokuwa na umoja!!!!!!
   
 15. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,964
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kufuatana na uzoefu wa muda mrefu, viongozi wa vyama vya wafanyakazi, sijaona walipoweza kufanikiwa pale wanapopendekeza jambo fulani kwa serikali, hususa ni wanapodai haki za wafanyakazi, mfano kima cha chini cha mshara, hawakuweza kufanikiwa, tukaambiwa watoa muda wa siku kadhaa, lakini serikali haikujali ikafumba macho, na haikuchukuliwa hatua zozote zile, angalu hata kuitisha mgomo wa siku moja tu, Je ni njia ipi vyama vya wafanyakazi vinaweza kufanya serikali ikalifanyia kazi swala la Fao ka Kujitoa?
   
 16. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni kweli Mungu ni mkuu na anaweza kufanya lolote tuombalo,lakini naona kama kuna wakati
  tunamchosha Mungu kwa maombi ambayo majibu yake yako wazi tayari hayahitaji hata kuombwa.
   
 17. O

  Oscardious Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  loh wala siyo uzuzu' ingekuwa ni busara kama ungetoa wazo mbadala na hatua gani ichukuliwe kuanzia sasa na kabla ya kikao cha bunge la mwezi ujao kuhitimishwa. Kwani kwa sheria hii mpya ya mifuko ya jamii, mwenzetu inamunyima usingizi ndiyo maana kaamuka saa tisa usiku, akifikiria mpaka afikishe umri wa miaka 55 ndiyo apewe pesa yake. Pia mwenzetu kwenye heading yake anaulizia kuhusu muswada wa sheria ya kujitoa vipi?
   
 18. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,964
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Asante sana kwa kuwaelimisha wadau wenzetu. Mara nyingi nimesikia wafanyakazi wengi wakilalama juu ya sheria hii mpya ya pensheni, na pia nimekuwa ni fatilia hata wabunge wetu, kila wakati wanasema "Imefika wakati wafanyakazi kuchukua hatua" je ni hatua gani hizo?
   
 19. k

  kifumbiko JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Dar serikali hii mbona 2takoma! hapo utekelezaji ni f!
   
 20. S

  Simba Yuda Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maombi hayashindwi kama unavyofikri. kila jambo linawakati wake.
   
Loading...