waziri mkuu anateuliwa lini???
mkuu hao wamejitia upofu kwa makusudi hawawezi kukuelewa , aliyefuta amesema amefuta matokeo ya uchaguzi wa zanzibar .
Rais Magufuli ametangaza tatehe 17/11 kuwa siku rasmi ya bunge la 11 kuanza kazi, bunge linalojumuisha pande mbili za muungano yaani Bara na Tanzania Zanzibar.
Lakini jambo la kushangaza bunge limeitishwa bila kufikia mwafaka wa wabunge wa JMT toka Zanzibar.
Endapo itatokea wabunge toka Zanzibar watakanyaga kapeti jekundu na kuapa bila kuchaguliwa ama kuteuliwa kwa maana uchaguzi wote wa Zanzibar umefutwa, basi bunge la Tanzania litakuwa limeandika historia mpya na pengine inaweza kuwa ajabu ya dunia kwa bunge kuapisha wabunge ambao uteuzi wao umetenguliwa na tume halali ya uchaguzi.
Jambo la msingi kabla ya rais kulihutubia bunge, atumie muda huu uliobaki hadi tarehe 17 kutatua tatizo lililopo.
Nawasilisha.

Unamdanganya nani na kwa faida ya nani, eti wasimamizi tofauti wakati aliyekuwa anatiki ni yuleyule ndani ya daftari lilelile.Jamani kuweni waelewa basi,mlishaambiwa hakuna uchaguzi wa wabunge Zanzibar uliofutwa,umefutwa ni uchaguzi wa ZEC Zanzibar na sio wa NEC,na mtambue kuwa sanduku huwa tafauti na wasimamizi tafauti kila tume inaajiri wasimamizi wake,tuulizeni sisi jamani msiropoke,na ndio maana majimbo yote ya Zanzibar ya ubunge wamewatangaza lkn ya uwakilishi na udiwani Zanzibar umefutwa.
Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unasimamiwa na NEC (Lubuva), Uchaguzi wa Raisi wa Zanzibar, Baraza la wawakilishi na Mashekha unasimamiwa na ZEC hivo tu Zec wamefuta uchaguzi wa sehemu inayowahusu yaani wa Baraza la wawakilishi, Rais na Mashekha tu.
Mwananchi wa Zanzibar hupiga kura 5 yaani (Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Zanzibar, Wabunge wa JMT, Baraza la wawakilishi na Mashekha) wakati sisi tunapiga kura 3 nafikiri wazijua?
Tanzania Bara tukipiga kura tunapaka kidole kimoja ule wino lumaanisha tayari ushamaliza kazi ya kupiga kura, wakati Zanzibar wanapaka vidole viwili yaani ukipoga ya JMT Rais na wabunge unapaka kidole chake na Ukipiga Rais SMZ, Mashekha na Wawakilishi unapaka kidole chake ivo taratibu tofauti.
NB: NEC inaingia mpaka Zanzibar kusimamia uchaguzi wake wa wabunge wa JMT na RAIS wa JMT ndio ukomowake hapa, ZEC inaanza kwa Rais wa SMZ, Wawakilishi na Mashekha.
Wawakikishi wa Zanzibar hawaingii kwenye bunge la JMT
Jamani kuweni waelewa basi,mlishaambiwa hakuna uchaguzi wa wabunge Zanzibar uliofutwa,umefutwa ni uchaguzi wa ZEC Zanzibar na sio wa NEC,na mtambue kuwa sanduku huwa tafauti na wasimamizi tafauti kila tume inaajiri wasimamizi wake,tuulizeni sisi jamani msiropoke,na ndio maana majimbo yote ya Zanzibar ya ubunge wamewatangaza lkn ya uwakilishi na udiwani Zanzibar umefutwa.
Si hakika kama wanatumia daftari moja ila si kila anaweza kupiga kura za Rais wa SMZ na Baraza la wawakilishi na Mashekha anaweza kupiga za JMT
Licha ya nani anasimamia uchaguzi, wapiga kura si walewale? Kila Mzanzibari anapiga kura ya JMT na SMZ lakini asiyemzanzibari akiwa Zanzibar anapiga tu ya JMT. Kwa mantiki hiyo, kama serikali imekubali kwamba uchaguzi ulikua na kasoro, chujio gani limetumika kujua na kujiridhisha kwamba huo uvunjwaji wa taratibu uliathiri tu SMZ?
Mkuu Samaritan,Licha ya nani anasimamia uchaguzi, wapiga kura si walewale? Kila Mzanzibari anapiga kura ya JMT na SMZ lakini asiyemzanzibari akiwa Zanzibar anapiga tu ya JMT. Kwa mantiki hiyo, kama serikali imekubali kwamba uchaguzi ulikua na kasoro, chujio gani limetumika kujua na kujiridhisha kwamba huo uvunjwaji wa taratibu uliathiri tu SMZ?
Daftari ni moja lakini kuna wapiga kura ambao hawana vigezo kupiga kura kwa Raisi na wawakilishi wa Zanzibar bali wanaweza kupiga kura kwa wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano!ZEC walisema haukuwa huru na haki idadi ya majina ilizidi, kwani kulikuwa na daftari mbili tofauti na wasimamizi tofauti na vituo tofauti?
NEC haiko Zanzibar bali ni ZEC inasimamia chaguzi zote, wa muungano wakifanya hivyo kiwakala. Pili hakuna Mashekha wanaochaguliwa katika chaguzi hizi bali ni madiwani. Mashekha uteuliwa ndiyo maana wanalalamikiwa san na vyama vya upinzani.Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unasimamiwa na NEC (Lubuva), Uchaguzi wa Raisi wa Zanzibar, Baraza la wawakilishi na Mashekha unasimamiwa na ZEC hivo tu Zec wamefuta uchaguzi wa sehemu inayowahusu yaani wa Baraza la wawakilishi, Rais na Mashekha tu.
Mwananchi wa Zanzibar hupiga kura 5 yaani (Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Zanzibar, Wabunge wa JMT, Baraza la wawakilishi na Mashekha) wakati sisi tunapiga kura 3 nafikiri wazijua?
Tanzania Bara tukipiga kura tunapaka kidole kimoja ule wino lumaanisha tayari ushamaliza kazi ya kupiga kura, wakati Zanzibar wanapaka vidole viwili yaani ukipoga ya JMT Rais na wabunge unapaka kidole chake na Ukipiga Rais SMZ, Mashekha na Wawakilishi unapaka kidole chake ivo taratibu tofauti.
NB: NEC inaingia mpaka Zanzibar kusimamia uchaguzi wake wa wabunge wa JMT na RAIS wa JMT ndio ukomowake hapa, ZEC inaanza kwa Rais wa SMZ, Wawakilishi na Mashekha.
Wawakikishi wa Zanzibar hawaingii kwenye bunge la JMT
Nipe link ya mada zako zilizodadavuliwa na mimi niongeze ujuzi,Mtoa post unaonekana makala zako unatoaga kwasabab hisia zinakutuma,hutumii udadavuzi huzichambui hufanyi research napata wasiwasi kama ww ni msomi hata kama umesoma basi ulishindia madesa tu,,,,No research no right to speak ,sikudharau lkni huo ndo ukwel
Kwani katiba unasemaje juu ya kufuta baadhi ya kura zilizopigwa na mtu mmoja kwenye kituo kimoja na msimamizi mmoja.Soma katiba