Rais Magufuli ametangaza tatehe 17/11 kuwa siku rasmi ya bunge la 11 kuanza kazi, bunge linalojumuisha pande mbili za muungano yaani Bara na Tanzania Zanzibar.
Lakini jambo la kushangaza bunge limeitishwa bila kufikia mwafaka wa wabunge wa JMT toka Zanzibar.
Endapo itatokea wabunge toka Zanzibar watakanyaga kapeti jekundu na kuapa bila kuchaguliwa ama kuteuliwa kwa maana uchaguzi wote wa Zanzibar umefutwa, basi bunge la Tanzania litakuwa limeandika historia mpya na pengine inaweza kuwa ajabu ya dunia kwa bunge kuapisha wabunge ambao uteuzi wao umetenguliwa na tume halali ya uchaguzi.
Jambo la msingi kabla ya rais kulihutubia bunge, atumie muda huu uliobaki hadi tarehe 17 kutatua tatizo lililopo.
Nawasilisha.