Bunge kusimamisha Shughuli zake zote za kawaida Kuujadili Mgomo wa Madaktari!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Baada ya vuta nikuvute ya wiki mbili sasa, hatimaye Bunge letu tukufu, leo litasimamisha shughuli zake zote za kawaida na kuijadili hoja ya dharura ya mgomo wa madaktari unaoendelea karibu nchi nzima!.

Mjadala huo, umefuatia Naibu Spika, Mhe. Job Ndugai, kuikubali hoja ya Mbunge wa Kigoma, Mhe. Peter Serukamba, akiwa ni mbunge wa 6 kuomba muongozo spika kwa jambo hilo hilo.

Japo mimi ni miongoni mwa tuliolaani udikiteta wa Job Ndugai, nilipomsikia jana, nakiri Mhe. Job Ndugai is better 100times than madame spika!.

Update:

Wanabodi,

Hata hivyo leo asubuhi, bunge lilisitisha shughuli zake zote na kuanza kwa taarifa ya spika kuhusu mgomo wa madaktari na kwa vile bunge limependekeza maamuzi makubwa ya ajabu, Spika amempigia simu rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Pinda muda wa usiku wa manane (bila kujali kama viongozi hao wamejipumzikia au la!), na kuwaeleza mapendekezo ya kamati hiyo ya bunge, hivyo I was very right!. Mengine yote yanafuatia kauli hiyo ya Spika!.

Hata hivyo, hoja yangu niliileta na kuiconfirm mimi mwenyewe kufuatia uzoefu wangu wa shughuli za bunge. Kwa vile huu mgomo wa madaktari ni dharura zaidi, kamati ya bunge imekamilisha kazi yake jana usiku nilitegemea hoja ya mgomo ndio ingetangulia na kufuatiwa na hoja ya marekebisho ya katiba, lakini sasa mambo yamekwenda vice versa, mjadala wa marekebisho ya katiba ndio umetangulia, hivyo shughuli badala ya kisimama leo, leo shughuli zinaendelea!. Hivyo nakiri kosa la kulazimisha mgomo wa madaktari kuwa ni dharura kihivyo kwa bunge letu.

Nimekubali makosa, nawaombeni minisamehe sana!.

Mtu mzima akishakiri kosa na kuomba msamaha, sio busara kuendelea kumshutumu, kwani wengine tunajifunza kwa makosa hata mara sabaini fii sabaa!.

Samahanini Sana!.

Pasco.
 
Nchi yangu Tanzania...

Siku zote alikuwa wapi anakuja kukubali leo? Yaani baada ya vifo na mateso mengi kwa wagonjwa?

Au ameikubali kwa kuwa hoja imetolewa na Peter Serukamba Lowassa?
 
Namuona madame spika kwenye kiti chake, jana Ndugai alidai leo atakuwepo Spika ili jambo hilo lijadilike BUNGENI.
 
sasa limebaki pango la wanyang'anyi, ndio maana wanajipandishia posho hovyo, wanalala bungeni, hawahudurii vikao, wanapitisha sheria kandamizi, wakao kwa maslahi ya kichama zaidi na wanaongoza kwa kula starehe
Bunge tukutu lilishapoteza utukufu wake miaka mingi iliyopita kwa kweli.
 
Wanabodi,

Baada ya vuta nikuvute ya wiki mbili sasa, hatimaye Bunge letu tukufu, leo litasimamisha shughuli zake zote za kawaida na kuijadili hoja ya dharura ya mgomo wa madaktari unaoendelea karibu nchi nzima!.

Mjadala huo, umefuatia Naibu Spika, Mhe. Job Ndugai, kuikubali hoja ya Mbunge wa Kigoma, Mhe. Peter Serukamba, akiwa ni mbunge wa 6 kuomba muongozo spika kwa jambo hilo hilo.

Japo mimi ni miongoni mwa tuliolaani udikiteta wa Job Ndugai, nilipomsikia jana, nakiri Mhe. Job Ndugai is better 100times than madame spika!.

Mwongo sana wewe
 
Kuna kitu kinaniambiua Ndugai angeweza kuwa spika mzuri kuliko Makinda. Mwanzoni huyu baba alianza kwa mikiki ya kidikteka lakini kadri siku zinavyokwenda anaoneka kusoma alama za nyakati, inawezekana angetaka kufunguka zaidi lakini (pengine) boss wake (Anna Makinda) ni tatizo. Ukiangalia maamuzi yoyote ya maana ya bunge yamefanywa na huyu baba e.g. kuunda kamati ya bunge kuchunguza Jaira saga, kamati ya bunge kwenye mgomo wa madaktari, na sasa bunge kujadili mgomo wenyewe.

Makinda anawaandalia bomu wabunge wa ccm 2015, sijui kwa nini hawajafikiria kumtosa kabla bomu halijalipuka?
 
But, is it true that Bunge linajadili hii issue?

Hawa wanatuchezea hawa.....wameacha kujadili muda wote huo, hadi muda wa kikao unaisha kesho ndo wanataka kujadili?
Au wanataka kujadili sasa hivi kama geresha, ili muswada wa marekebisho ya katiba mpya usiwekwe bungeni this time?
 
Bunge linaendelea na maswali na majibu.
 
Inaonekana issue itajadiliwa jioni maana this morning ''Mtoto wa Mkulima'' anakutana na ma Dr huko DSM.

Ila kuliita Bunge la TZ eti ni tukufu naona ni kuwadhihaki Watanzania
 
Serikali iliyozea kujifunza on the hard way!!! Bunge nalo, wamejisemea wengine humu "tukutu" Makinda naye, hata sijui utamuweka sehemu ipi...poor woman.:washing:
 
Serikali iliyozea kujifunza on the hard way!!! Bunge nalo, wamejisemea wengine humu "tukutu" Makinda naye, hata sijui utamuweka sehemu ipi...poor woman.:washing:

Wanawake wakiwezeshwa, wanaweza.
 
Bunge tukutu lilishapoteza utukufu wake miaka mingi iliyopita kwa kweli.

Siyo kwamba lilipoteza utukufu wake,hakuna utukufu kwa mwanadamu hata siku moja,utukufu una mungu tu,utasemaje bunge ni tukufu au liliwai kuwa tukufu wakati hao wabunge wengi wao wameingia kwa hila!!!?na yanayoongelewa mara nyingi ni porojo tu,utukufu hauna porojo mkuu,dhihaka hizi kwa mungu ndiyo maana tumelaaniwa na tunatangatanga mpaka leo.
 
Back
Top Bottom