Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,673
- 149,860
Mods naomba muweke uzalendo mbele na muwe na uchungu na hii nchi na muache watu tuhoji mradi hatuvunji sheria za nchi wala za JamiiForums na sio kila mada mnaunganisha tu.
Turudi kwenye mada.
Sioni tofauti kati ya Spika wa Bunge na Mkulu katika kusigina katiba na sheria za nchi ili kulinda maslahi ya watu fulani fulani kwasasababu ambazo hazina tija kwa Taifa.
Halikadhalika hakuna tofauti kati ya Spika na wabunge wa chama fulani katika kupindisha kanuni za Bunge,sheria za nchi na hata kutetea uvunjaji wa katiba ili tu kuwalinda vibaraka wa chama fulani.
Kwa hali hii iliyojitokeza leo Bungeni, Bunge hili limepoteza moral authority ya kuhoji habari za Bashite maana wao kama watunga sheria wameshindwa kabisa kutetea sheria na kanuni wanazozipisha wenyewe na badala yake wamekuwa mstari wa mbele kubariki uvunjwaji wa sheria za nchi na hata kanuni za Bunge walizozitunga na kuzipitisha wao wenyewe.
Sasa najiuliza watu wa aina hii wanapata wapi uhalali wa kuhoji habari za Bashite ili hali nao wanafanya yale yanayofanana na Bashite?
Watanzania wenzangu hili swala la Bashite kwa sasa tuachane nalo kabisa bali tujipange tu kuja kuwahukumu watu hawa mwaka 2020.
Kwa mfano,watu waliobariki wagombea kutoka CUF A na CUF B wanapata wapi uhalali wa kuhoji habari za Bashite?