Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,781
- 50,302
Lakini unawezaje kupima ujinga wa mtu kwa kutumia kiwango cha usomi? Kati ya mwenye shahada ya uchumi na mwenye shahada ya kiswahili ni nani kati ya hao mwenye elimu kuliko mwingine!?Mfumo haujakaza wasomi kugombea na kuwashinda hao kina Lusinde... wananchi ndio wamepeleka wajinga wenzao wakawawakilishe!
Rais anasaini sheria au Rais husaini Muswada wa sheria?Bunge ndiyo linalotunga Sheria. Ukitoa maelezo kuonesha kuwa bunge halitungi Sheria, jua unajiongoza vibaya.
Mswada kwa lugha nyepesi ni mapendekezo. Kwa ivo mapendekezo siyo Sheria.
Mapendekezo yawe ya serikali ama ya mbunge binafsi, ili yawe Sheria ni lazima yapitie hatua kadhaa ndani ya bunge.
Huo mchakato wa kuyageuza mapendekezo kuwa Sheria ndiyo utungaji wenyewe wa Sheria.
Kama mbunge ama Serikali wakaleta mapendekezo Yao (Mswada) na Bunge wakayakataa mapendekezo hayo, basi hayawezi kuwa Sheria.
Na ndiyo maana Rais hutia Saini Sheria zilizotoka bungeni na siyo miswada iliyopelekwa bungeni.
Sasa hoja ya kiwango cha Elimu za wabunge ni jambo jingine kabisa lisiloondoa mamlaka ya kikatiba ya bunge kutunga Sheria.
Allen unawezaje kuweka fani tofauti na kutaka kufananisha mkuu..Lakini unawezaje kupima ujinga wa mtu kwa kutumia kiwango cha usomi? Kati ya mwenye shahada ya uchumi na mwenye shahada ya kiswahili ni nani kati ya hao mwenye elimu kuliko mwingine!?
Elimu ya mtu inaweza isikupe uhakika wa kiwango ya akili, ila inakupa mtu aliyewekeza kwenye kujiongezea maarifa. Inawezekana pia kuna mtu hakwenda shule sio kwa kuwa hana akili, ila ni mazingira tu magumuLakini unawezaje kupima ujinga wa mtu kwa kutumia kiwango cha usomi? Kati ya mwenye shahada ya uchumi na mwenye shahada ya kiswahili ni nani kati ya hao mwenye elimu kuliko mwingine!?
Sheria. Kwake unakuwa ni mswada kwa kuwa yale huwa ni mapendekezo ya bunge kwake.Rais anasaini sheria au Rais husaini Muswada wa sheria?
Nimefanya makusudi. Maana kama kusoma ndiyo kigezo cha kuwa mbunge Bora, basi pia tujue kusoma kupi ndiyo usomi.Allen unawezaje kuweka fani tofauti na kutaka kufananisha mkuu..
Elimu bora ni msingi wa vitu vingi sana mimi huwa nafatilia pia Bunge la SA ukimsikiliza Waziri wao wa fedha au Mwanasheria wa Serikali unaridhika kwa kinachojadiliwa hata yule Malema aliambiwa ili awe na hoja Bungeni aende shule na alifanya hivyo ila kama unaamini shule sio kigezo cha maendeleo endelea kuamini hivyo mkuu..Nimefanya makusudi. Maana kama kusoma ndiyo kigezo cha kuwa mbunge Bora, basi pia tujue kusoma kupi ndiyo usomi.
Maana anaweza kuchaguliwa nguli wa fizikia akachemka, watu wakasema bora tungechagua nguli wa Jiografia.
Kwa ivo tukubaliane ni usomi upi utatupa wabunge Bora! Lakini kitaalamu Elimu (Literacy) ni nini? Kamusi zote za kiingereza zinasema Literacy ni uwezo wa mtu kujua kusoma na kuandika. Mjadala upo wazi.
Kuna mahali nimesema shule siyo msingi wa maendeleo? Shule ni nini? Maana neno shule tumelitohoa toka kwenye lugha ya kijerumani "Schule" Sasa shule ni nini?Elimu bora ni msingi wa vitu vingi sana mimi huwa nafatilia pia Bunge la SA ukimsikiliza Waziri wao wa fedha au Mwanasheria wa Serikali unaridhika kwa kinachojadiliwa hata yule Malema aliambiwa ili awe na hoja Bungeni aende shule na alifanya hivyo ila kama unaamini shule sio kigezo cha maendeleo endelea kuamini hivyo mkuu..