DOKEZO Bundi anyemelea TIRA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Makongoroso

New Member
Nov 17, 2022
2
1
RIPOTA PANORAMA

MWENENDO wa mambo katika Sekta ya Bima si shwari baada ya kubainika kuwa Kamishna wa Usimamizi wa Bima (TIRA), Abdallah Baghayo Saqware ameshiriki kuanzisha Chuo Kikuu cha Bima na Mifuko ya Jamii barani Afrika, ambacho kwa jina la kimombo kinaitwa Africa College of Insurance and Social Protection (ACISP.)

Tayari baadhi ya wadau wa Sekta ya Bima wameanza kupasa sauti zao kulalamika kuwa baada ya kuanzishwa kwa chuo hicho kumekuwa na vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa maadili katika utendaji wa soko la Bima hapa nchini.

Nyaraka ambazo Tanzania PANORAMA Blog imeziona zinaonyesha kuwa Chuo cha Africa College of Insurance and Social Protection kimesajiliwa Brela kwa nambari 140997609, Oktoba 2, 2020 kikiwa na Ofisi zake Mikocheni, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa nyaraka hizo, wana hisa wa chuo hicho wako wanne akiwemo Saqware mwenye hisa 250. Mtaji wa hisa za kampuni hiyo ni Shilingi milioni 50 na thamani ya kila hisa ni Shilingi 1000. Wana hisa wote ni raia wa Tanzania.

Tanzania PANORAMA Blog imedokezwa kuwa chuo kikuu hicho kinaendesha shughuli zake katika chumba kimoja kilichopo eneo la Mikocheni mkoani Dar es Salaam na taarifa zaidi zimedai kuwa Saqware amekuwa akitumia madaraka ya ukamishna aliyonayo TIRA kukiwezesha kifedha chuo chake hicho.

Alipotafutwa leo kupitia simu yake ya kiganjani kuzungumzia madai hayo, Saqware alisema yupo eneo baya atafutwe baada ya muda mfupi na alipotafutwa baadaye hakupatikana, simu yake haikuwa hewani.

Tanzania PANORAMA itaripoti zaidi sakata hili.
saqware-696x464.jpeg
 
Tanzania PANORAMA itaripoti zaidi sakata hili.View attachment 2449021

Hii taarifa nadhani haiko sawa. Kwa maini yangu ni muhimu watumishi wa umma wakaanza kujua namna ya kuishi nje ya ajira zao ili waweze kua huru kiuchumi.
Kwa nafasi aliyonayo hawezi kukosa pesa za kuanzisha biashara yeyote. Mimi binafsi nampongeza kwa kutumia taaluma au maarifa yake kuanzisha taasisi ambayo itakuza weledi wa taaluma hiyo.
Wengi wamefanya hivi na tunastahili kuwapongeza ila shida itakuja km atatumia mamlaka yake kusema wakala wa bima lazima awe na elimu hii ba inapatikana kwenye chuo chake.
Watanzania tujifunze kuthamini jitihada za mtu au mnataka aibe au mnataka wote tuwe maskini.
Km kuna conflict of interest ungeonyesha ndio nyie mnataka tushike vyeo vikibwa badae tuwe tunawaomba omba mitaani uko.
Tafadhali sana muombee jamaa chuo kisimame hata watoto wako wataenda kufanya kazi hapo badae.
Kuna mmarekani alikuwa CEO wa General Electric anataasis yake inaitwa Jack Welch Management Institute unahisi kuisimamisha alisubiri astaafu kabisa lahasha mipango inaanza mapema.
Kwa mtazamo wako utakua maskini na ukiendelea hivyo utakua mchawi.
 
shida itakuja km atatumia mamlaka yake kusema wakala wa bima lazima awe na elimu hii ba inapatikana kwenye chuo chake.
Kwa upeo wako umeona hii ndilo tatizo pekee?

Vipi kuhusu tuhuma hii kwa mujibu wa huyo "wistle blower"

taarifa zaidi zimedai kuwa Saqware amekuwa akitumia madaraka ya ukamishna aliyonayo TIRA kukiwezesha kifedha chuo chake hicho.
 
Back
Top Bottom