Bulyanhulu yabadili mfumo kukwepa makinikia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,610
Kutokana na zuio la Serikali la kusafirisha mchanga wa dhahabu (makinikia) nje ya nchi, mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umebadili mfumo wa utendaji kazi kwa kuanzisha mtambo mpya utakaochenjua mabaki ya awali kwa kutumia kemikali ya sayanaidi (Cyanide).

Njia hii imeelezwa itatoa kiasi kidogo cha dhahabu tofauti na uchimbaji wa awali wa mtambo mkubwa uliokuwa ukizalisha makinikia yenye dhahabu nyingi zaidi.

Meneja mkuu wa mawasiliano kutoka Acacia, Asa Mwaipopo alisema hayo jana Jumamosi wakati wa hafla ya kuwaaga wafanyakazi 2,000 waliopunguzwa.
Wafanyakazi hao wamepunguzwa kutokana na mgodi kupunguza uzalishaji baada ya Serikali kuzuia usafirishaji wa makinikia kwenda nje ya nchi.

Mwaipopo amesema kati ya wafanyakazi 2,000 waliopunguzwa, 1,200 ni waajiriwa wa Bulyanhulu na 800 ni kutoka kwenye kampuni za kandarasi zinazofanya kazi katika mgodi huo.

Amesema katika mfumo mpya wa mtambo wa uzalishaji kwa kutumia kemikali ya sayanaidi wataajiri upya wafanyakazi 150 wa kampuni na wengine 150 kutoka kwenye kampuni za kandarasi ambao watakuwa wakifanya usafi, ulinzi na huduma ya chakula.

Mwaipopo amesema mtambo mkubwa uliokuwa ukitumika kwa uzalishaji umekamilisha kazi jana Jumamosi, hivyo kufikia mwisho wa uzalishaji wa makinikia katika mgodi huo.

Amesema licha ya mgodi kupunguza uzalishaji na wafanyakazi lakini ulipaji wa ushuru wa huduma kwa halmashauri na kodi za Serikali utaendelea ijapokuwa ni kwa kiwango kidogo.

Mwaipopo amesema shughuli za kijamii zilizokuwa zimepangwa zitaendelea kufanyika katika wilaya za Msalala, Kahama na Nyang’wale.
Amesema ni matumaini ya kampuni kuwa mazungumzo yanayoendelea kati yao na Serikali yataleta matunda ya kuanza kazi tena kwa mgodi huo.

Kuhusu wafanyakazi waliopunguzwa, amesema licha ya kuagana nao wamewapa mafunzo ya ujasiriamali na kuwaandaa kisaikolojia kwa kuwafunza namna ya kuishi maisha mbadala tofauti na waliyokuwa nayo wakati wa ajira.

Mwakilishi wa vyama vya wafanyakazi katika mgodi huo, Kazimili Lubigisa amesema jana Jumamosi ilikuwa siku maalumu ya kumuaga Meneja Mkuu wa mgodi huo, Graham Crew lakini kwa masikitiko na hali ambayo haikutarajiwa ilikuwa siku ya kuwaaga wafanyakazi wote.

Lubigisa amesema kufungwa kwa mtambo huo kumesababisha madhara makubwa kwa wafanyakazi na Serikali kwa jumla, ikiwa ni pamoja na familia zao kuathirika kiuchumi, elimu, afya na kisaikolojia.

Amesema pia vijiji 14 vinavyozunguka mgodi vitaathirika kiuchumi, kielimu, afya, miundombinu ya barabara na mapato ya Serikali.
Amesema makandarasi wanaofanya kazi katika mgodi huo nao wameathirika, hivyo ameiomba Serikali kuharakisha mazungumzo ili kuepusha madhara zaidi.

Akiwaaga wafanyakazi, meneja mkuu Crew anayeondoka baada ya kufanya kazi katika mgodi huo kwa miaka miwili amesema hakuna anayefurahia hatua iliyopo lakini akawataka wafanyakazi kuendelea kuwa na imani kuwa mazungumzo yanayoendelea baina ya uongozi na Serikali yataleta muafaka na kampuni kuendelea na uzalishaji.

mwananchi
 
Yule spika Ndugai alisema kufukuzwa wafanyakazi elfu mbili hakumsumbui
Ingawa kutoa posho ya siku moja kusaidia matibabu ya mbunge mwenzao ilimshinda.
 
Wafanyakazi 2000 kwa evarage mtu Ana mafao ya 40m inamaanisha nssf/ppf wajiandae kutoa 80B kama fao la kujitoa.
 
Nani, wafanyakazi 2000 au?
Logically, ni wizi mkubwa uliokuwa ukifanyika kupitia makinikia, dhahabu safi ilikuwa ni geresha tu. Dhahabu nyingi nilikuwa ikifichwa kwenye makinikia hiyo nyingine safi nilikuwa ni kuzuga tu. Na hawa makuwadi wetu wa kitanzania walioshilikiana nao wangepewa kibano cha mbwa mwizi waliojaribu kuhonga hizo kamati e.g Kafumu na wengineo
 
Hujui hata robo unachokiongea. Acha kutumia theluthi ya akili uliyopewa bure na mwenyezi Mungu.

Jumapili njema.
 
Kutokana na zuio la Serikali la kusafirisha mchanga wa dhahabu (makinikia) nje ya nchi, mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umebadili mfumo wa utendaji kazi kwa kuanzisha mtambo mpya utakaochenjua mabaki ya awali kwa kutumia kemikali ya sayanaidi (Cyanide).

Njia hii imeelezwa itatoa kiasi kidogo cha dhahabu tofauti na uchimbaji wa awali wa mtambo mkubwa uliokuwa ukizalisha makinikia yenye dhahabu nyingi zaidi.

Meneja mkuu wa mawasiliano kutoka Acacia, Asa Mwaipopo alisema hayo jana Jumamosi wakati wa hafla ya kuwaaga wafanyakazi 2,000 waliopunguzwa.
Wafanyakazi hao wamepunguzwa kutokana na mgodi kupunguza uzalishaji baada ya Serikali kuzuia usafirishaji wa makinikia kwenda nje ya nchi.

Mwaipopo amesema kati ya wafanyakazi 2,000 waliopunguzwa, 1,200 ni waajiriwa wa Bulyanhulu na 800 ni kutoka kwenye kampuni za kandarasi zinazofanya kazi katika mgodi huo.

Amesema katika mfumo mpya wa mtambo wa uzalishaji kwa kutumia kemikali ya sayanaidi wataajiri upya wafanyakazi 150 wa kampuni na wengine 150 kutoka kwenye kampuni za kandarasi ambao watakuwa wakifanya usafi, ulinzi na huduma ya chakula.

Mwaipopo amesema mtambo mkubwa uliokuwa ukitumika kwa uzalishaji umekamilisha kazi jana Jumamosi, hivyo kufikia mwisho wa uzalishaji wa makinikia katika mgodi huo.

Amesema licha ya mgodi kupunguza uzalishaji na wafanyakazi lakini ulipaji wa ushuru wa huduma kwa halmashauri na kodi za Serikali utaendelea ijapokuwa ni kwa kiwango kidogo.

Mwaipopo amesema shughuli za kijamii zilizokuwa zimepangwa zitaendelea kufanyika katika wilaya za Msalala, Kahama na Nyang’wale.
Amesema ni matumaini ya kampuni kuwa mazungumzo yanayoendelea kati yao na Serikali yataleta matunda ya kuanza kazi tena kwa mgodi huo.

Kuhusu wafanyakazi waliopunguzwa, amesema licha ya kuagana nao wamewapa mafunzo ya ujasiriamali na kuwaandaa kisaikolojia kwa kuwafunza namna ya kuishi maisha mbadala tofauti na waliyokuwa nayo wakati wa ajira.

Mwakilishi wa vyama vya wafanyakazi katika mgodi huo, Kazimili Lubigisa amesema jana Jumamosi ilikuwa siku maalumu ya kumuaga Meneja Mkuu wa mgodi huo, Graham Crew lakini kwa masikitiko na hali ambayo haikutarajiwa ilikuwa siku ya kuwaaga wafanyakazi wote.

Lubigisa amesema kufungwa kwa mtambo huo kumesababisha madhara makubwa kwa wafanyakazi na Serikali kwa jumla, ikiwa ni pamoja na familia zao kuathirika kiuchumi, elimu, afya na kisaikolojia.

Amesema pia vijiji 14 vinavyozunguka mgodi vitaathirika kiuchumi, kielimu, afya, miundombinu ya barabara na mapato ya Serikali.
Amesema makandarasi wanaofanya kazi katika mgodi huo nao wameathirika, hivyo ameiomba Serikali kuharakisha mazungumzo ili kuepusha madhara zaidi.

Akiwaaga wafanyakazi, meneja mkuu Crew anayeondoka baada ya kufanya kazi katika mgodi huo kwa miaka miwili amesema hakuna anayefurahia hatua iliyopo lakini akawataka wafanyakazi kuendelea kuwa na imani kuwa mazungumzo yanayoendelea baina ya uongozi na Serikali yataleta muafaka na kampuni kuendelea na uzalishaji.

mwananchi
Hawa jamaa sasa ndio wameanza rasmi kuhujumu uchumi wanachokifanya wanafanya uzalishaji kwa kiwango cha chini kabisa mpaka siku serikali ikubaliane nao. Kwa uwekezaji mkubwa walioweka hawatavunja mktaba bali uchangiaji wao katika uchumi wetu utakuwa mdogo sana.
Tujitayarishe kufunga mkanda.
 
Wakati ule wa uchaguzi wakati kale kawimbo ka Komba kuwa wacha waisome namba eeehhh kanapigwa watu wengi tulidhani huyu Mwanalizombe amewalenga wapinzani. Lakini lilipoanza sakata la vyeti na kutoongezwa mishahara ya watumishi ikaonekana ni wengi zaidi wameguswa, sasa hapa tulipofikia kupoteza ajira 2,000 kwa mpigo ni pa kusikitisha sana. Mbaya zaidi wazungu walivyo wakaksi watahakikisha kuwa hata tukichimba dhahabu wenyewe tunakosa pa kuiuza. Hii vita ya kiuchumi ilitakiwa tujipange kwanza walau kwa miaka mitano, ila kwa sasa naona kama tumewahi sana
 
Hayo ni madhara ya kupambana na wawekezaji kihuni huni.
Tunakula hasara mpaka basi.
Sasa ajira nzuri za kudumu za wafanyakazi 2000 zimepotea ghafla. Na sote tunajua wazi karibu kila mfanyakazi hapo aliyeachishwa kazi alikuwa na wastani wa watu watano kwenye familia yake waliokuwa wanamtegemea kwa kila kitu. Hivyo huo msiba mkubwa sana.
 
Akili ya kimaskini inawaza tukose wote.. Haijalishi madhara..
 
wakiondoka jumla itakuwa vizuri sana, watakuja wawekezaji wengine na negotiation mpya ambayo itanufaisha nchi! gold si kitu cha kispotispoti, watakuja wengi tu hawa wakiachia gap!
Wakina nani hao wapya watakuja kwenye mazingira hayo ya kihuni huni?
Wachina? Wahindi? Waarabu?
Subiri uone kama kuna mbilikimo atakuja na mtaji mkubwa wa kuja kuwekeza hapo.

Kama hujui tu, ila fahamu kuwa wawekezaji wa sekta ya madini ni watu wale wale waliotapanya mitaji yao katika makampuni tofauti tofauti kwa mtindo wa hisa. Bahati mbaya sana makampuni hayo ni machache sana na huwa wanajuana na kupatana.

Kwenye sekta ya madini Barrick ni kama FISI, ukiona mfupa umemshinda fisi basi ujui paka kamwe hatauweza, paka hata kuunusa hatajaribu sembuse kuulamba.
 
Back
Top Bottom