Bulendu: Vyama vya siasa, Asasi za kiraia, kidini waliambiwa wasichanganye na siasa. Wamewaacha, wamekwama sasa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Kushuka Kwa hamasa ya wapiga Kura mwaka baada ya mwaka,nini chanzo?

Na Dotto Bulendu

1.Wadau wa Siasa kutokuwa Sehemu ya Hamasa,kwa zaidi ya miaka 25 Sasa tangu mfumo wa vyama Vingi uanze,wadau wakuu katika hamasa ya Kisiasa nchini Ni....

(A).Vyama Vya Siasa,Hawa huzunguka usiku na mchana,mjini na Vijijini kusaka Wafuasi na wanachama huku wakihamasisha Wafuasi wao kujiandikisha,kuhudhuria shughuli za Kisiasa,Kufuatulia Siasa,Kupiga Kura na kulinda Kura,sasa tangu 2015 Serikali iliwaambia wadau hawa muhimu wakae pembeni na kuiacha Serikali ifanye kazi,hii imeshusha Kwa kiwango Kikubwa hamasa ya Siasa nchini.

(B).Asasi za Kiraia(Azaki),hawa walikuwa wadau wakubwa kwenye kutoa Elimu ya Uraia,Siyo siri kwenye Asasi nyingi za Kiraia kumejaa hofu kubwa ya kujihusisha na hata kuongelea Siasa,leo zile semina,makongano,mijadala kuhusu Elimu ya Uraia imesinyaa kwa kiwango kikubwa,hii imeshusha Kwa kiwango kikubwa hamasa ya Siasa nchini Tanzania.

(C).Madhehebu ya dini,Hawa walikuwa Ni wadau
wakubwa,ilikuwa kila tunapokaribia uchaguzi,madhehebu ya dini mbalimbali yalikuwa yakitoa waraka na hata matangazo ya kuhamasisha waamini wake kushiriki kwenye uchaguzi,madhehebu ya dini yalipoambiwa yasijihusishe na Siasa yalitii na kukaa kimya,hatusikii tena Viongozi wa dini wakiwapa maisha waamini wao kushiriki shughuli za kisiasa ikiwemo kujiandikisha,hii imeathiri sana hamasa za Kisiasa nchini.

(D). Taasisi ya Elimu,zilipopigwa stop kuruhusu Siasa vyuoni(Hususani Vyuo Vikuu),hamasa Kwa Kada hii ya wasomi imeshuka Kwa kiwango kikubwa,leo Yale makongamano,midahalo iliyokuwa inaruka mubashara kutoka Vyuo Vikuu haipo,ndiyo maana hata vijana wasomi leo hawana hamasa tena ya kujihusisha na mambo ya nchi na hususani Siasa.

(2).Kauli tata za wenye dhamana,kumeibuka kauli zenye utata kuhusu Siasa za Vyama Vingi,kauli
Kama....
(i )Tukiamua kuleta maendeleo tunaleta na tukiamua kutoleta hatuleti na hamna ya kutufanya kitu.
(ii ).Kwenye Wilaya Yangu,sitaki kuona mgombea wa Upinzani anashinda.
(iii ).Ninyi si mlichagua wenyewe upinzani,haya wafuateni hao hao na ndiyo mjifunze kuchagua.
(iii).Siwezi kushirikiana na Mdudu anyeitwa Upinzani mimi.Kauli Kama hizi hazina Afya kwenye ustawi wa Siasa na Demokrasia nchini na ukweli zimeua hamasa ya Siasa nchini iliyojengwa Kwa miaka 25.

(3). Matukio ya Kuogofya kwenye Siasa na yanayowakuta wanasiasa,
( I )Alikufa Ally Zona pale Msamvu Morogoro kwenye Shughuli za Kisiasa.
(ii ).Alikufa Daudi Mwangosi kwenye shughuli ya Kisiasa.
(iii). Uchaguzi Mdogo Kule Igunga,mtu alimwagiwa Tindikali.
(iv).Akwilina alikufa pembeni ya vuta nikuvute ya Polisi na Waandamanaji.
(V). Mwanasisa Alphonce Mawazo aliuawa Kwa kifo chenye Utata na hata kuagwa kwake kulikuwa na vuta nikuvute.
(vi ).Mwanasiasa Tundu Lissu alipigwa Risasi,badala ya tukio lile kuchukuliwa kibinadamu Baadhi ya wanasiasa wakaweka utu pembeni na hata kuanza kumbeza pigwa Risasi.
(Vii). Kule Arusha mwaka 2011 watu walikufa kwenye mkutano wa kisiasa.

Matukio kama haya yamerejesha Ari za watu wengi nyuma,kwani wanajiuliza hii ndiyo Maana ya Siasa.

(4 ).Shughuli za Kisiasa kutoakisi maisha ya wapiga Kura,watu wengi wanapokwenda kupiga Kura wanaamini Kura aliyoipiga Ina Maana kubwa katika maisha na maendeleo yake yeye binafsi,kimachotokea siyo hicho....
( i ).Siunakumbuka wapiga Kura waliwahi jibiwa Kwa kebehi kuwa Bora wale nyasi lakini ndege ya Rais Itanunuliwa?
(ii ).Si unakumbuka Waziri mmoja bila hofu aliwahi waambia watumishi wa Umma kuwa hamna mpango wa kupandisha maslahi Yao?
(iii).Si unakumbuka kuna Waziri aliwahi sema,yeye kwake Milioni 10 Ni pesa ya mbona tu wakati kuna watanzania wengi wanaishi chini ya shilingi 2300 Kwa Siku?

(5 ). Uchaguzi Umejaa viashiria vya Ulaghai na mazingaombwe,hili hata Katibu Mkuu wa Chama Tawala Dr Bashiru Ally alililalamikia sana,kuna malalamiko huku mtaani,mfumo wetu wa uchaguzi unaruhusu ambaye hajashinda kutangazwa Mshindi,wengi wanaona hakuna haja ya kupiga Kura kwenye mfumo usio na uhakika wa kupata mshindi aliyepigiwa Kura.

(6 ). Tabia ya Viongozi waliochaguliwa kufikiria kwanza maslahi Yao na kuanza kuishi kwa Kujimwambafau,hii ni sikitiko la wapiga Kura,baadhi ya tunaowachagua,hujigeuza wao ndiyo wenye akili,hawasikilizi,wababe,hii inawakatisha tamaa wapiga Kura na imeshusha Hamasa.

Yapo mengi sana yaliyosababisha Hamasa ya wapiga Kura kushuka Kwa kasi.
 
B).Asasi za Kiraia(Azaki),hawa walikuwa wadau wakubwa kwenye kutoa Elimu ya Uraia,Siyo siri kwenye Asasi nyingi za Kiraia kumejaa hofu kubwa ya kujihusisha na hata kuongelea Siasa,leo zile semina,makongano,mijadala kuhusu Elimu ya Uraia imesinyaa kwa kiwango kikubwa,hii imeshusha Kwa kiwango kikubwa hamasa ya Siasa nchini Tanzania.

Hili ni la kuliangalia vizuri.
 
Tukiamua kwenda kujitafutia ka-mkate ka familia wanakuja na maspika kutupigia kelele kutuhamasisha. Kwani sisi ni viziwi?
 
B).Asasi za Kiraia(Azaki),hawa walikuwa wadau wakubwa kwenye kutoa Elimu ya Uraia,Siyo siri kwenye Asasi nyingi za Kiraia kumejaa hofu kubwa ya kujihusisha na hata kuongelea Siasa,leo zile semina,makongano,mijadala kuhusu Elimu ya Uraia imesinyaa kwa kiwango kikubwa,hii imeshusha Kwa kiwango kikubwa hamasa ya Siasa nchini Tanzania.
Hili ni la kuliangalia vizuri.
Sina hakika sana na hii kitu kwani hawa wa vijijini wakipata vipi hamasa toka kwa hizi asasi?
 
Haya mabavu kupuuza na kuzima democrasia chama cha kijani hakipo salama ipo siku hakitavalika.Binafsi yeyote anaevaa kijani naona kivuli cha dhuluma dhidi ya wengine.
 
Kushuka Kwa hamasa ya wapiga Kura mwaka baada ya mwaka,nini chanzo?

Na Dotto Bulendu

1.Wadau wa Siasa kutokuwa Sehemu ya Hamasa,kwa zaidi ya miaka 25 Sasa tangu mfumo wa vyama Vingi uanze,wadau wakuu katika hamasa ya Kisiasa nchini Ni....

(A).Vyama Vya Siasa,Hawa huzunguka usiku na mchana,mjini na Vijijini kusaka Wafuasi na wanachama huku wakihamasisha Wafuasi wao kujiandikisha,kuhudhuria shughuli za Kisiasa,Kufuatulia Siasa,Kupiga Kura na kulinda Kura,sasa tangu 2015 Serikali iliwaambia wadau hawa muhimu wakae pembeni na kuiacha Serikali ifanye kazi,hii imeshusha Kwa kiwango Kikubwa hamasa ya Siasa nchini.

(B).Asasi za Kiraia(Azaki),hawa walikuwa wadau wakubwa kwenye kutoa Elimu ya Uraia,Siyo siri kwenye Asasi nyingi za Kiraia kumejaa hofu kubwa ya kujihusisha na hata kuongelea Siasa,leo zile semina,makongano,mijadala kuhusu Elimu ya Uraia imesinyaa kwa kiwango kikubwa,hii imeshusha Kwa kiwango kikubwa hamasa ya Siasa nchini Tanzania.

(C).Madhehebu ya dini,Hawa walikuwa Ni wadau
wakubwa,ilikuwa kila tunapokaribia uchaguzi,madhehebu ya dini mbalimbali yalikuwa yakitoa waraka na hata matangazo ya kuhamasisha waamini wake kushiriki kwenye uchaguzi,madhehebu ya dini yalipoambiwa yasijihusishe na Siasa yalitii na kukaa kimya,hatusikii tena Viongozi wa dini wakiwapa maisha waamini wao kushiriki shughuli za kisiasa ikiwemo kujiandikisha,hii imeathiri sana hamasa za Kisiasa nchini.

(D). Taasisi ya Elimu,zilipopigwa stop kuruhusu Siasa vyuoni(Hususani Vyuo Vikuu),hamasa Kwa Kada hii ya wasomi imeshuka Kwa kiwango kikubwa,leo Yale makongamano,midahalo iliyokuwa inaruka mubashara kutoka Vyuo Vikuu haipo,ndiyo maana hata vijana wasomi leo hawana hamasa tena ya kujihusisha na mambo ya nchi na hususani Siasa.

(2).Kauli tata za wenye dhamana,kumeibuka kauli zenye utata kuhusu Siasa za Vyama Vingi,kauli
Kama....
(i )Tukiamua kuleta maendeleo tunaleta na tukiamua kutoleta hatuleti na hamna ya kutufanya kitu.
(ii ).Kwenye Wilaya Yangu,sitaki kuona mgombea wa Upinzani anashinda.
(iii ).Ninyi si mlichagua wenyewe upinzani,haya wafuateni hao hao na ndiyo mjifunze kuchagua.
(iii).Siwezi kushirikiana na Mdudu anyeitwa Upinzani mimi.Kauli Kama hizi hazina Afya kwenye ustawi wa Siasa na Demokrasia nchini na ukweli zimeua hamasa ya Siasa nchini iliyojengwa Kwa miaka 25.

(3). Matukio ya Kuogofya kwenye Siasa na yanayowakuta wanasiasa,
( I )Alikufa Ally Zona pale Msamvu Morogoro kwenye Shughuli za Kisiasa.
(ii ).Alikufa Daudi Mwangosi kwenye shughuli ya Kisiasa.
(iii). Uchaguzi Mdogo Kule Igunga,mtu alimwagiwa Tindikali.
(iv).Akwilina alikufa pembeni ya vuta nikuvute ya Polisi na Waandamanaji.
(V). Mwanasisa Alphonce Mawazo aliuawa Kwa kifo chenye Utata na hata kuagwa kwake kulikuwa na vuta nikuvute.
(vi ).Mwanasiasa Tundu Lissu alipigwa Risasi,badala ya tukio lile kuchukuliwa kibinadamu Baadhi ya wanasiasa wakaweka utu pembeni na hata kuanza kumbeza pigwa Risasi.
(Vii). Kule Arusha mwaka 2011 watu walikufa kwenye mkutano wa kisiasa.

Matukio kama haya yamerejesha Ari za watu wengi nyuma,kwani wanajiuliza hii ndiyo Maana ya Siasa.

(4 ).Shughuli za Kisiasa kutoakisi maisha ya wapiga Kura,watu wengi wanapokwenda kupiga Kura wanaamini Kura aliyoipiga Ina Maana kubwa katika maisha na maendeleo yake yeye binafsi,kimachotokea siyo hicho....
( i ).Siunakumbuka wapiga Kura waliwahi jibiwa Kwa kebehi kuwa Bora wale nyasi lakini ndege ya Rais Itanunuliwa?
(ii ).Si unakumbuka Waziri mmoja bila hofu aliwahi waambia watumishi wa Umma kuwa hamna mpango wa kupandisha maslahi Yao?
(iii).Si unakumbuka kuna Waziri aliwahi sema,yeye kwake Milioni 10 Ni pesa ya mbona tu wakati kuna watanzania wengi wanaishi chini ya shilingi 2300 Kwa Siku?

(5 ). Uchaguzi Umejaa viashiria vya Ulaghai na mazingaombwe,hili hata Katibu Mkuu wa Chama Tawala Dr Bashiru Ally alililalamikia sana,kuna malalamiko huku mtaani,mfumo wetu wa uchaguzi unaruhusu ambaye hajashinda kutangazwa Mshindi,wengi wanaona hakuna haja ya kupiga Kura kwenye mfumo usio na uhakika wa kupata mshindi aliyepigiwa Kura.

(6 ). Tabia ya Viongozi waliochaguliwa kufikiria kwanza maslahi Yao na kuanza kuishi kwa Kujimwambafau,hii ni sikitiko la wapiga Kura,baadhi ya tunaowachagua,hujigeuza wao ndiyo wenye akili,hawasikilizi,wababe,hii inawakatisha tamaa wapiga Kura na imeshusha Hamasa.

Yapo mengi sana yaliyosababisha Hamasa ya wapiga Kura kushuka Kwa kasi.
Kinachonisumbua ni kwamba hata wanaccm waliopewa nafas Yáñez kujimwámbafai wamegoma
 
Nashauri Serikali kama inataka kufanya Uchunguzi wa Kina juu ya sababu ya hali hii yote basi itumie huu Uchambuzi wa ' Comrade ' wangu wa SAUT Mwanza Dotto Bulendu kwani alichokiandika amemaliza kila Kitu na tena amewasaidia mno kwa Kuwaonyesha sehemu walizokosea hivyo wajitathmini na wasahihishe ili mwakani wasjie ' Kuumbuka ' zaidi.
 
Kwangu mimi hili ni Andiko bora kuwahi kutokea ktk historia ya uwepo wa vyama vingi nchini.. Kongole kwako mr Bulendu Mungu akubariki
 
Wakina Azory.Ben Saanane,Mawazo Alphonce na Mtikila watapiga kura, maan mmewaweka pahala salama
 
Back
Top Bottom