Egwugu
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,558
- 8,555
Ni furaha yangu na kwa wote walioweza kuingia mwaka mpya salama lakn pia natoa pole kwa wale wote ambao kwa namna moja ama nyingne wamekutana na vikwazo katika kuumaliza na kuingia mwaka mpya 2012,inshallah Mungu azidi kuwabariki
Ni mda kdogo toka nimepotea hapa jamvini na kikubwa ni kutokana na kuwa safarini Kagera ambako nilipata pia nafasi ya kuhitimisha sikukuu zote mbili za mwisho wa mwaka nikiwa huko,safari yangu hii iliniwezesha kupitia baadhi ya maeneo na mitaa na mambo mengi yakiwemo mazuri bila kuyasahau na mabaya pia katika nyanja mbalmbal za kmaisha kama ifuatavyo
Barabara:Ni jambo la kujivunia kwa wanakagera kwa kuweza kuwa na barabara nzuri na zenye lami kuanzia za kuingia mpaka za mitaani na kwa kiasi kikubwa zikiwa safi
Biashara:Mkoa wa Kagera bado haujafanya vya kutosha katika kuimarisha biashara na kutumia nafasi zilizopo kwa ajiri ya kuwaendeleza wakazi wake,mfano,nimeshangaa kuona mpaka leo hapana kituo cha mabasi chenye hadhi ya kuitwa stand ya mabus kwa maana bado stand ni ndogo na bado ni ya matope,pale kuna connection ya nchi kama 4 na wasafiri wanakutana pale kwenda Uganda,Rwanda,Burundi na hata Kenya..mkoa unahitaji kuliona hili mapema kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini
Kilimo:katika hili nimevutiwa na kuona wananchi wameamua kuwekeza katika kilimo cha miti ya mbao almaarufu 'mipines',ili linaonekana kuwa pozeo la kupungua kwa uzalishaji wa ndizi na mibuni katika kurekebisha hali ya uchumi na kipato kwa ujumla wananchi sasa wanaona huyu pines ndo mkombozi wao kwa sasa
Habari,Mawasaliano na Burudani:Katika burudani nimependa kuona kuna nyimbo nyingi na nzuri zinazoimbwa na wasanii wa huko na ambazo hazipatikani kwingine bado,hili ni tatzo la kukosa mapromota na wabunifu wa kukuza sanaa,binafsi nimerudi na nyimbo nyingi kias kama atahtaji mtu humu ndani basi anipm,sehemu za kumbi za disco 'night club' bado chache sana japo kdogo zilizopo ni nzuri,nimefurahi kuona kuna vituo vya matangazo 'redio' kama v3 japo naona kuna haja ya kuongeza vingine kama itawezekana pia