Bukoba tour report

Lucas

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
2,457
1,108
Hellow wana JF na kina Nshomile woote mliopo hapa (BIshanga, Muganyizi, Nitonye etc) napenda kuwataarifu kuwa nimerudi rasmi kutoka huko kwenu. Nimekaa Bukoba ndani ya siku chache lakini nimejitahidi angalau kufika maeneo kadhaa ikiwemo Bukoba mjini, Kasharu, Hamugenbe, Kashozi, Custom, Kaitaba, Njia panda Katerero, Kemondo, Kagondo, Muhutwe, Kaboya, Katoke, Kagoma, MUleba, Rubungo, Iyangilo, Humura, Rulongo, Rubya, Ijumbi, Ibuga, Kamachumu, makumbusho ya wahaya, Nyawaipaga, Ruhanga, Nyailigamba, BUjingo falls, Rushwa, Mushabago, Nshamba, Njia panda Mgana hosp, Kyaka, Izigo, Mtukula, Kyamirowa, Kiziramuyaga, Nyakabango....etc

sasa kuhusu nini nimejifunza huko hebu kuweni wavumilivu kidogo nitawaletea hapa muda si mrefu... ila Nshomile mna vituko!!

Kama nimetaja kijiji chako basi pokea salamu, maana huko mvua zinanyesha na barabara zinapitika vizuri tuu. maharage bado uko ni cheap kg 1 shs 700 - 1000, ndizi zipo nyingi tu kama kawaida nasikia!

Pia napenda niwajulishe kuwa ndugu zenu huko wananunua sana gari aina ya Forester, zimejaa sana kwa kina Nshomile sasa ivi.

Ukimsikia Nshomile anasema nakuja na boxer usidhani anakuja na **** bali ana kuja na pikipiki aina ya boxer maana ndio zimejaa huko.

Pia nimefurahi kumuona Nshomile mmoja yeye anaishi DSM lakini alienda kwao akajenga kijiji cha kisasa na kuweka umeme na kuwapangisha bure wafanyakazi wa serikali waliopo hapo yaani walimu, wauguzi na polisi. amejenga pia kituo cha polisi, soko, mahakama na maduka na yeye wala sio mwanasiasa! hongera kwake na uwe mfanmo kwa wengine

sikupenda kabisa kwa baadhi ya gest hapo mjini magodoro kufunikwa na nylonkwa sababu ambazo nisingependa kuzitaja hapa! MBADIRIKE NYIE WATANI WANGU!!

Ahsante kwa walionielekeza kwenda kula 888 maana kweli wana menu saaaaaaaafi sana. nitawamiss sana

Tabia yao ya kuongea ki-nshomile muda wooooote na mahali pooote nayo sikuipenda maana ukiwa wewe huelewo wanakunyanyapaa kiasi fulani

mikoa mingine tumechanganyika sana nowadays, lakini kwa kina nshomile bado wanadominate sana huko kwao unaweza fika sehemu ukauliza mtu wa kabila tofauti na kumpata ikawa shida sana! na ukimpata more than 60% amesakuwa nshomile!!

Mengi nikikumbuka nitayaleta hapa,

ni salamu na report kutoka Nshomile city - Bukoba....... wadau mpo?
 
hongera sana mkuu hujapewa senene? Hilo swala la nylon tuachie sisi nyinyi haliwahusu
 
Nashukuru... nawasubiri wenyeji waniambie walikuwa wapi nilipopita vijijini kwao? SL yuko wapi?
Niko hapa SS...

Nimeleta ujumbe toka kwa my boss Bishanga naomba niunukuu kama ulivyo... SL dear, naomba uende chit chat kwenye uzi wa 'bukoba tour report' mwambie mtoa mada wewe ni sekretare wa Bishanga, mwambie niko bize nahangaikia kusafirisha yatch yangu kuileta bukoba, next time akija bukoba nitamkaribisha kwenye yatch tule dina, tukielea lake victoria. Mi ndo Bishanga bana. Mwisho wa kunukuu...
 
kina Nshomile kwa proud!! Mzee aliyeishia shule ya msingi, anakuambia nimesoma hadi "Standard seven" ili ujue anajua kizungu!! halafu hiyo yatch, Magufuli atamruhusu? ama kiboti kidogo kama cha kuvulia samaki? na pia Mwambie kabisa iwe well covered juu maana kwa sasa kuna wadudu wanafanana na mbu ni wengi sana kule beach/custom
 
hongera sana mkuu hujapewa senene? Hilo swala la nylon tuachie sisi nyinyi haliwahusu

nilikuwa nakusubiri sana kwa hamu hapa!! Hah! Yaani amini usiamini Nsenene wako cheap ukiwanunua nje ya BUkoba, I mean hii mikoa yetu mingine hii, lakini they are so expensive kwa kina Nshomile!! ila nilipewa mihogo ya kutafuna ikiwa imefungwa kwenye Mgomba
 
kina Nshomile kwa proud!! Mzee aliyeishia shule ya msingi, anakuambia nimesoma hadi "Standard seven" ili ujue anajua kizungu!! halafu hiyo yatch, Magufuli atamruhusu? ama kiboti kidogo kama cha kuvulia samaki? na pia Mwambie kabisa iwe well covered juu maana kwa sasa kuna wadudu wanafanana na mbu ni wengi sana kule beach/custom
Hahaha! Wahaya wana EGO usisikie... Umeleta zawadi gani?
 
nilikuwa nakusubiri sana kwa hamu hapa!! Hah! Yaani amini usiamini Nsenene wako cheap ukiwanunua nje ya BUkoba, I mean hii mikoa yetu mingine hii, lakini they are so expensive kwa kina Nshomile!! ila nilipewa mihogo ya kutafuna ikiwa imefungwa kwenye Mgomba

Dah naona hujafika kijijini kwetu maana ungepata bahati ya kuziona gari za aina cardilac, kama hujapewa ile pombe inayoitwa ''embandule'' basi hujafaidi
 
Back
Top Bottom