Bukoba: Mahakama ya Wilaya yamhukumu Emmanuel Cleophace, miaka 30 jela kwa kosa la kumuoa mwanafunzi

Mbona Lulu jaji alisema 17 ni.mtu mzima sababu alikuwa anafanya vitu vya kiutu uzima?? Hizi sheria zimekaaje??
 
Hapo sheria inayotumika inaitwa Education Act Chapter 353 s. 60A(1), kinapiga marufuku mtu kumuoa mwanafunzi au mwanafunzi kuoa .

S. 60A (2) inatoa adhabu kwa mtu atakayeoa mwanafunzi wa primary or secondary school adhabu ni 30 yrs, but mutatis mutandis with Cap 16 , kwenye Canons of statutory interpretation ya "intention of the legislature "

Swali; Je, mwanafunzi / uanafunzi unaishia wapi?
Jibu: Uanafunzi wa o-level unashia mpaka Necta wakishatoa matokeo (Ndiyo huyo hakimu alivyotafsiri)
 
Huyo jamaa si angesubiri matokeo yatoke. Haraka zake zimemgharimu.
Hivi hamsomagi nyuzi mkaelewa? Kesi ni ya mwaka 2016 mtoto alihitimu kipindi hicho. Hapa hela ilitafutwa weeeee, dogo kakosa hela ya rushwa wakamfunga.
 
Hivi hamsomagi nyuzi mkaelewa? Kesi ni ya mwaka 2016 mtoto alihitimu kipindi hicho. Hapa hela ilitafutwa weeeee, dogo kakosa hela ya rushwa wakamfunga.
Waambie mod wasiwe waretrieve nyuzi zilizopita msomi.
 
Je ndoa ilifungwa wakati uyo binti akiwa kamaliza shule au bado mwanafunzi? Hakimu aache ujinga na kutaka sifa za kujulikana kipuuzi, utamfungaji mtuhumiwa ambae ata nae anaonekana ni immature miaka 30 kwa kosa ambalo bado halielezeki? Walitakiwa wajue ukomo wa uanafunzi unaishia lin na wapi na tukio lilitokea wakati gan, na probably ukomo hua unaoshia siku ya mtihani wa mwisho wa kumaliza shule, mengine yajayo hua ni options tu.
 
Back
Top Bottom