Bukoba: Mahakama ya Wilaya yamhukumu Emmanuel Cleophace, miaka 30 jela kwa kosa la kumuoa mwanafunzi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,391
2,000
Mahakama ya Wilaya Bukoba imemhukumu Emmanuel Cleophace (20) kwenda jela kwa miaka 30 kwa kosa la kumuoa mwanafunzi aliyekuwa amehitimu kidato cha nne anayeitwa Adilia Alistides(18). Mwanafunzi aliyeolewa alikuwa akisoma Shule ya Sekondari Kabugaro iliyopo Manispaa ya Bukoba Kagera.

Hukumu hiyo ya Mahakama imesomwa na Hakimu Mkazi Joseph Luambano.

Kesi hii ni ya mwaka 2016

-------------
Hapo sheria inayotumika inaitwa Education Act Chapter 353 s. 60A(1), kinapiga marufuku mtu kumuoa mwanafunzi au mwanafunzi kuoa .
S. 60A (2) inatoa adhabu kwa mtu atakayeoa mwanafunzi wa primary or secondary school adhabu ni 30 yrs, but mutatis mutandis with Cap 16 , kwenye Canons of statutory interpretation ya "intention of the legislature "

Swali; Je, mwanafunzi / uanafunzi unaishia wapi?
Jibu: Uanafunzi wa o-level unashia mpaka Necta wakishatoa matokeo (Ndiyo huyo hakimu alivyotafsiri)

 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,542
2,000
Takukuru iingie kati. Huenda kuna kitu kilitakiwa hapo kwenda kwa hakimu au mtu flan kuanzia umri hadi mazingira ya binti kuolewa sijaona kosa hapo. Ka vip naye binti afungwe kwa kujilengesha kwa kijana
 

Nyendeke

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
1,398
2,000
Daaa.., kweli Kijana Mdogo huyo wanataka akitoka Jela awe amebakisha miaka 5 ya Kustaafu kwa hiari?
 

Tyrone mofekeng

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
698
1,000
Ìla kama angekua anamtinginya tu bila kumuoa haingekua kesi. Miaka 18 na 20 ni almost sawa. Hakuna mtoto hapo. Nafikiri wanaichanganya na issue ya ubakaji.
 

binjo

JF-Expert Member
Feb 22, 2016
2,117
2,000
18 ni mtoto

16anaweza olewa


14 anaweza olewa

Naona namba zinasomwa kinyume nyumeMiaka 10 mtoto anajua matumizi ya kondomu bila pratiko


Miaka 13 anakiherehere cha pratiko

Yooote haya yanatokea yupo katika uangalizi wa wazazi.


Wakati huo mzazi yupo bize na mashamba bize na kutafuta ada ya mtoto akirudi kachoka hoi.

Hawazi lolote zaid ya kesho sijui itakuwaje


Huku mtoto kanogewa kulamba asali pasipo kujua huwa inapalia na Wenda ikakuletea kikohozi.

Mungu tusaidie wazazi.
 

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
16,454
2,000
Aki yamama ,,dunia haina Haki.mamaeeee.

Hapo pesa zimemwaga balaa ...form four wamemaliza mwezi ulopita takriban siku 14 zilizopita .... Maajabu nikwamba AMEOA ????? DUUUHHHHH WAZAZI WAHUYO MTOTO NAWALAANIWE.IYO KESI IMEKIBIZWA MCHAKA MCHAKA SANA .
 

dedon

JF-Expert Member
Jul 6, 2015
1,489
2,000
kama sijakosea sheria ya ndoa si ina hararisha mtt wa kike kuolewa akiwa na miaka 13????
 

Chris14

JF-Expert Member
Oct 2, 2017
3,085
2,000
Huyo jamaa si angesubiri matokeo yatoke. Haraka zake zimemgharimu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom