Ni wapi nimeona nchi zingine kuwa bora katika maandishi yangu.Hujui unachoongea,tiss kuingia waingie wapi na tiss IPO kila sehemu Hadi nyumba za ibada!!!..tz Ina resources nyingi tu deep ndani ya majirani,miongoni mwa vitu vilivyomuudhi kagame Hadi kuwa na chuki na tz na kikwete ni baada ya tz kupakua mzigo wa kutosha deep ndani ya intelligence ya rwanda kupitia vijana wa kitanzania wenye muonekano wa kitusi...ndani ya uhamiaji Kuna tiss,na mmoja alikua mwana japo tushazika...hoja yako ya nchi kuparaganyika inatoka wapi!?..kipi kinekuonesha kwamba nchi imeparaganyika!?..Somalia na Congo zitakuaje Kama tz imeparaganyika!?..acheni kuona nchi zingine Bora kuliko ya kwenu!!
Hata hivyo, na hii ni sababu moja inayonifanya niamini kuwa wewe ni mpiga kifua zaidi kuliko hali halisi; ni wazi kabisa kuna nchi bora katika maeneo haya kutuzidi sisi, kwa sababu mbalimbali, moja ikiwa raslimali walizonazo. Sasa hili nalo una ubishi nalo?
Hao Rwanda, hawakuwa hapa kwetu, na inawezekana bado wapo sana hata katika sehemu nyeti zaidi?
Ninaposema nchi kuparaganyika, ni 'relative', kutokana na tulikokuwa tumekufikia nyakati fulani.
Wewe hata CCM unaona ni ileile iliyokuwepo miaka iliyopita? Huoni tofauti yoyote huko?
Ni hawa hawa ndio wanaotuendeshea nchi yetu. Kwa hiyo kama wewe unaona CCM ni chama imara kabisa kinachojali maslahi ya nchi hii, bila shaka watakuwa ndio wanaokupeleka chooni kila baada ya masaa kadhaa.
Na hii tabia ya ushabiki shabiki (uchawa) usiokuwa na maana ndilo anguko la nchi yetu katika nyanja muhimu ikia ni pamoja na hizo unazopigia kifua juu yake.
Tena unapoongelea habari za TISS, unachefua kwelikweli! Tiss ya akina Kipilimba? Hao walioko huko uhamiaji wao hawaoni uraia wa nchi yetu unavyouzwa kama takataka?