Kwa hali hii hii iliyopo sasa humu nchini, au pengine una matumaini ya baadae? Ni kipi hasa kinachokupa matumaini wewe ambacho wengine hatukioni?
Hapa naona unajipa matumaini, pengine kutokana na hali ulivyoijua huko siku za nyuma, zamani kidogo. Nikukumbushe, hiyo ni historia, imekwishapita hiyo!
Siyo sasa, na huko tuendako, kama hali itaendelea kuwa kama inavyokwenda sasa usiweke matumaini.
Nchi hii inabadilika sana, hata wananchi wake tumekuwa kama tumepuliziwa na pepo baya la kulaza akili zetu.