Building Permits Tanzania: Kweli ujenzi hoela utaisha!

Building Permits Tanzania: Kweli ujenzi hoela utaisha!

LostSoldier

Member
Joined
Apr 15, 2013
Posts
8
Reaction score
2
Ni jambo ambalo kwangu haliingii kichwani eti kupata kibali (Building Permit) cha kujenga hata nyumba ya kuishi (Residential House) hapa Dar es Salaam Tanzania ni mlolongo unaochukua zaidi ya miezi 7. Ni vema kuwa taasisi zinazohusika zikapata muda wa kuchanganua na kupitia maombi yote ya vibali vya ujenzi, lakini miezi 7 au 9 ni muda mrefu kupitiliza. Inasemekana vibali hivi kupitishwa katika vikao vya manispaa husika (madiwani), ambazo hukaa mara moja kwa mwezi. Katika vikao hivi vya mara moja kwa mwezi, huwa kuna agenda nyingi za kushughulikiwa, kwahiyo hata katika vikao hivi, muda wa kupitisha vibali hivi huwa finyu.

Mimi bado sielewi, ni kwanini Mama Tibaijuka anaachia hali kama hii iendelee na upeo wake wote. Inasemekana kuwa kuna maslahi (POSHO) ya madiwani na wajumbe wengine ambao hukaa katika vikao hivi vya kupitisha vibali ambavyo hawatataka viguswe na pengine wizara inaogopa kuwatibua wahusika, Siasa kama kawaida. Waziri Tibaijuka, tafadhali, hili suala ni la kuangalia upya, kuwe kuna comittee ya kupitisha vibali vya ujenzi ndani ya mwezi mmoja maximum. Hakuna haja ya kibali cha ujenzi kucheleweshwa kwa miezi 6, 7 hadi 9 na bado tunategemea na kuota kuwa ujenzo holela utaisha katika nchi hii. Tuweke siasa pembeni,hili suala la Building Permits halijatulia na wala hatuhitaji viongozi wenye PhD kuliona hilo, labda uwoga wa kupambana na wenye posho zao.
 
Askari uliyepotea hilo ni moja. Lingine linalosikitisha ni ubadilishaji wa hati za kumiliki ardhi. Unapotaka kubadili jina unaweza
kuchukuwa hadi miaka mitano. Hii ndio sababu watu wengi wanamiliki ardhi zikiwa na majina ya watu wengine ambayo
inapelekea hata kukosa sifa za kukopesheka wakati mikopo mingi huitaji hati za umiliki wa ardhi.
 
Siasa ambazo zinatufanya tuogope kufanya hata mambo ambayo yapo Obvious na kwa manufaa ya waliowengi.
 
Kaka, huko kwenye hati ndo uozo kabisa. Kikubwa alichokifanya waziri wetu ni kuongeza tozo mbali mbali za malipo yanayohusika na ardhi, eti ili kupata fedha za kufidia/kujenga New Kigamboni City. Vipi haya mengine yanayotukwaza?. Kuna kitu kinaitwa Kigambini Development Authority (KDA) hata ofisi hawana na wamesimamisha shughuli za upimaji wa ardhi maeneo mengi ya kigamboni. Kuna haja ya katiba kuruhusu Kuajiri Viongozi kutoka nje ya nchi.
 
duh! ata mimi nimhanga wa hii kitu cha building permit,nataka kujenga na shindwa ukianza tu bila pb unawekewa alama ya x ,ila nilivyo tafiti ukitaka upate permit kwa haraka au kubadili matumizi ya ardhi kwa manispaa ya ilala nenda pale kwenye ofisi ya mhandisi wa manispaa kuna watu wao ukiwapa hela wanakufanyia kila kitu!utashangaa maajabu ya nchi hiii
 
Serikali inakosa Mapato Mengi sana kwa wananchi kukalia makazi kiholela bila ya kupimwa. Uzembe huu huchangiwa na Viongozi wasio na VISION ya Baadae, kuwa Tanzania especially Miji yake inapanuka kwa kasi sana.

Sasa wananchi wanapoenda kujenga makazi kiholela bila kupimwa hapo serikali ijui kuwa wanakosa Mapato na pindi wakiamua kuja kupaendeleza inatugharimu pesa nyingi za Mlipa kodi kufidia watu kwa ajili maboresho ya Makazi. Mfano Mzuri ni Manzese.Hivi sasa Serikali ikishirikiana na World Bank wanatarajia kuboresha Makazi ya Manzese na kuyaweka kwenye Mpangilio uliopangika kama Majiji mengine uyaonavyo.

Halafu ishu ya kubadili jina la hati ya kiwanja. Usiombe ukutane nalo,mbona utalia. Mm nna mwaka wa 3 saivi nnazungushwa.

Kingine, Nmejenga kwenye squater area, nkaenda kuomba kupimiwa. Hivi sasa ni mwaka wa 4 sijapata hati wala Offer. Mm nnakazana ili niweze kuipatia serikali kodi lakini kuna wash**zi wachache wanaokwamisha serikali isinufaike na kodi ya tutakayochangia kupitia Ardhi.
 
proffessionals zimeingiliwa na siasa ni matatizo matupu.
 
There is no rule of law here. go to the police. go to court. go to the ministries. go to immigration wololololooooo
 
Naomba kujuzwa hizi permit nikwa maeneo yabiashara tu ama hata makazi? Maana sisi wengine tumejenga na kuhamia bila hiyo permit ila squatter area.
 
Tukiwaambia hakuna impact ya div one zenu nchi hiyo mnabisha na kuja juu. Sasa kibali cha ujenzi wapitishe madiwani, madiwani wenyewe ni KK(kusoma na kuandika); si uhuni huo?
 
Halafu kuna wale jamaa wa sijui board ya quantity surveyors. Ukianza ujenzi tu wanaingia saiti na usumbufu kibao!
 
Ujenzi wa nyumba kwa watanzania wengi ni shida sana. Mtu unapata shida kuanzia kutafuta hela ya kununua eneo la kujenga. Ukipata hiyo hela unapotafuta eneo la kununua ili ujenge inatakiwa uwe makini usije kutapeliwa na matapeli watakaojifanya wana viwanja. Ukishapata kiwanja uangaike na upatikanaji wa building permit ambayo inaweza ikakuchukua zaidi ya mwaka kuja kupatikana. Sasa mazingira haya yanapelekea watu wengi kujenga nyumba bila kuwa na building permits na wengi uzifuatilia baadae wakati wakiendelea kujenga au hata baada ya kukamilisha kabisa ujenzi ingawa hii ni risk kubwa. Kuna watu kadhaa nawafahamu waliojenga nyumba zao hadi kukamilika na kuhamia na baada ya hapo ndipo wakapata vibali vya ujenzi.Kifupi unapozungumzia suala la building permits unagusa masilahi ya watu kwenye Halmashauri za miji yetu. Matatizo mengine yapo kwenye kupata hati (title deed) baada ya kuwa mtu amepewa offer ya kiwanja. Usumbufu uliopo pale mtu anapohitaji kupata title deed upelekea wengi kubakia tu na offer. Kwenye kupimiwa na kumilikishwa maeneo binafsi ndiyo usiseme.
 
Hili nalo ni jipu... Naomba mwenye namba ya mh. Lukuvi tafadhali..
 
Back
Top Bottom