Kiukwel ilipangwa sherehe bab kubwa ifanyike pale mtaani. Sherehe ilipangwa ifanyike wiki nzima kuanzia tar 31 May had tar 7 June. Jumapili paliwekwa ngoma, Jumatatu usiku ikafanyika kitchen party lakini kwa bahati mbaya tulipokea taarifa zilizostua mioyo ya wengi pale tulipoambiwa kaka yao mkubwa anayeitwa Hamis ametutoka duniani.
Alifariki kwa kupigwa risasi akiwa supermarket nchin Afrika Kusini, taarifa ambayo ilizima chereko pale mtaani na kukatisha ratiba ya sherehe iliyosalia ambayo ilitakiwa Jumatano ipigwe baikoko, Alhamis upigwe mnanda, Ijumaa ipigwe taarab live band kutoka kwa mashauzi Classic na Jumamosi wamalizie na rusha roho kisha Jumapili waende ukumbini kwa ajili ya harusi lakini mambo hayakuwa hivyo sherehe yageuka msiba!! unajua chanzo cha marehemu kuuawa?
Ungana nami sehemu ya tatu.
Chanzo: Mimi ni jirani yao.