Hizi gari nazikubali sana kwenye kuchanganya speed ziko fasta yaani nikiendesha hadi raha. Hili game la ASPHALT NITRO limenifanya niendeshe magari ya gharama ambayo ki uhalisia sijui kama nitawahi kuendesha.
Daah hapo kwenye hummer nimepakubali though kutokana na ulaji wa wese wa v8 naona hummer 3 yenye cc 3500 na cylinder 5 is preferred kwa upande wangu mkuu
Hili dude nalikubali yaani katika gari za kifahari na sports cars hii ni habari nyingine. Nilimuona kijana mdogo analiondoa kwa nguvu kidogo tu lilitaka kugeuka kwa power ilionayo, nilitamani kuomba nijaribu hahaha
Mie naona hapa bongo zinapita tu, mbona zina uvungu mkubwa tu...na pia mafundi wanaweza kuzinyanyua kidogo. Ila kiuchumi hazifai, bei ni ndefu sana kwakweli halafu bado insurance...nikufuru....nimeona Mayweather kaichukua hiyo ya bluu hivi karibuni.