Bugando wamtimua mgonjwa aliyeoza makalio wodini

Bugando wamtimua mgonjwa aliyeoza makalio wodini

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,356
KASHIFA nzito imeikumba Hospitali ya rufaa ya Bugando ya Jijini Mwanza baada ya kudaiwa kumtimua Mgonjwa wake ambaye ameozea Wodini hapo na sasa anaendelea kuoza akiwa nyumbani kwa mganga wa tiba za asili. Aliyetimuliwa Hospitalini hapo ni Joseph Luhogola (38),mkazi wa Kitongoji cha Nyabugera,Kijiji cha Mganza Wilaya ya Chato katika Mkoa wa Geita.

Luhogola alipokelewa Hospitalini hapo Apr 22 mwaka huu akitokea katika Hospitali ya Wilaya ya Chato ikiwa ni saa chache baada ya kupata ajali. Ajali hiyo ilitokea Apr 22 katika Kijiji cha Lubambagwe Wilayani Chato,ambapo gari aliyokuwa ameipanda Luhogola aina ya Hiace akitokea Geita kwenda Mganza ilipofika eneo hilo na kupinduka baada ya kuchomoka gurudumu la mbele na baadaye la nyuma.

Kufuatia ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 7 mchana, Luhogola huku akiwa amepoteza fahamu alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chato ambako hata hivyo alipatiwa huduma ya kwanza kabla ya kuchukuliwa na gari la Hospitali hiyo hadi Bugando. Kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bugando alipokelewa na kulazwa wodi E namba 803 ambayo ni ya wanaume iliyoko katika ghorofa la 8 kwenye majengo ya Hospitali hiyo.

Hata hivyo imeelezwa kuwa,baada ya madaktari kuchunguza afya yake ilibainika kuwa alikuwa na tatizo la uti wa mgongo na alishauriwa kulala chali muda wote kama tiba ya tatizo alilokuwa nalo. Wakati wote akiwa Wodini hapo, mke wake Keflini Kafaransa(36) alikuwa akizuiwa kukaa wodini kwa mumewe kwa alichoelezwa sheria za Hospitali hiyo haziruhusu mwanamke kukaa kwenye wodi ya wanaume kwa muda mrefu.

Kutokana na hali hiyo, Kafaransa alilazimika kumtafuta shemeji yake Hatari Petro(21)ambaye ni mdogo wa Luhogola na ndiye aliyechukua jukumu la kumuuguza kaka yake huyo kuanzia Apr 28 hadi anatimliwa kwenye hospitali hiyo. Akisimulia mkasa huo,Luhogola ambaye kwa sasa yu mahututi nyumbani kwa mganga wa tiba za asili za mifupa katika Kitongoji cha Elimu,Kijiji cha Nyankumbu Wilayani Geita alisema hakutegemea kama Hospitali kubwa kama Bugando ingeweza kumuaga akiwa katika hali hiyo.

Luhogola ambaye kwa sasa amepooza kuanzia kifuani hadi miguuni anadai kuwa, iwapo angejua hayo yangetokea angewashauri ndugu zake wasimpeleke kwenye Hospitali hiyo kwa kuwa tatizo alilonalo la kuoza makalio yake lilisababishwa na wauguzi.

LUHOGOLA+AKIWA+AMELALA+NYUMBANI+KWA+MGANGA+WA+JADI+22222.jpg


Joseph Luhogola (38),mkazi wa Kitongoji cha Nyabugera,Kijiji cha Mganza Wilaya ya Chato katika Mkoa wa Geita akiwa amelala nyumbani kwa mganga wa tiba za asili Paul Chasama ambaye ni mtaalamu wa tiba za jadi kwa kuunga mifupa na kurudisha viungo vya mwili vilivyochengana ambaye ni mkazi wa Kitongoji cha Elimu,katika kijiji cha Nyankumbu Wilayani Geita amedai kuwa,kutokana na uzoefu kwenye kazi hiyo anao uhakika wa asilimia mia kwamba Luhogola atapona.

Baadhi ya watu wamedai iwapo mganga Chasama atafanikiwa kumponya kijana huyo aliyeoza makalio yake kama unavyoona pichani basi watalazimika kuwaondoa wagonjwa wao hospitali na kuwapeleka kwake.Picha zote na Victor Bariety-Geita

Kama umeguswa na habari hii ya kusikitisha wasiliana na mwandishi wa Malunde1 Blog mkoani Geita ndugu Victor Bariety kwa simu namba 0763 681 747 kwa ajili ya msaada kwa mgonjwa aliyeoza makalio ndugu Joseph Luhogola.


Chanzo;malunde1.blogspot.
 
Ametimuliwa au amerudishwa nyumbani kwa kushindwa kitibitwa
 
Kumbe janja ya nyani blog inataka misaada sio?y tusimpe mgonjwa direct ww mwenye blog ndo unaomba commission????acha njaaa get well soon mgonjwa mungu yu nawe


Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
 
nyumbani kuna ndiyo kuna tiba mkuu?

Mkuu wagonjwa wengi tu wanarudishwa nyumbani, sio jambo la kwanza wala la ajabu, yawezekana kabisa hawezi tena kutibiwa hospitali, kwenye nchi zenye kujali raia kuna mfumo mzuri wa palliative care kwa wagonjwa kama huyo, wale wa kansa nk. si kitu kipya

I know how good EMT is kwenye kuleta habari zake dnio maana nikauliza lile swali ili ku-validate kama hakuna bias yoyote

end of life care is different from treatment!!!

anyway, it all depends on how you took my question... kitaaluma zaidi, wagonjwa kurudishwa nyumbani after treatment failure haijaanza leo
 
Ninaona kama mgonjwa ana simu pemveni yake why not usiweke namba yake hapa ili tuone tunaamua nn cha kumsaidia?????
 
Haya sasa tuone kama wala vumbi mta-step up na kumsaidia huyo bwana....

sisi ni typists aka keyboarders tu na kokoro nyingi

hata buku yule jamaa hapati from JF

wengine wameshaanza kulalama kwanini katoka hospitali, ukiwauliza wangefanya nini atasema abaki, ukiomba mchango wa tiba utaskia subiri kwanza

no wonder IQ zetu kimo cha mbuzi
 
sisi ni typists aka keyboarders tu na kokoro nyingi

hata buku yule jamaa hapati from JF

wengine wameshaanza kulalama kwanini katoka hospitali, ukiwauliza wangefanya nini atasema abaki, ukiomba mchango wa tiba utaskia subiri kwanza

no wonder IQ zetu kimo cha mbuzi

Karibu wiki mbili zilizopita kuna mdau alienda pale hospitali ya Ocean Road (ndo alivyodai). Aliyoyakuta huko eti yalimsikitisha sana.

Akaja humu kuanzisha uzi wa kuhamasisha watu wafunge safari waende hapo hospitalini kuwafariji wagonjwa.

Tokea wakati huo sijasikia wala kusoma popote kama wapo watu waliofanya hiyo ziara achilia mbali hata kuwa na mpango.

But of course, wala vumbi ni watu wenye upendo na ushirikiano sana (Cc: Husninyo). That is, ni watu wenye upendo na ushirikiano wa midomoni na vidoleni tu (ku-type na kunyooshea wengine vidole vya lawama)!!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Hii habari imechapishwa ktk gazeti jamhuri
Na tarehe 17/06 itaendelea. Kitaaluma ni vema kuonesha habari imetoka wapi. Hii ya kudaka juu kwa juu bila ku-attibute source ni makosa kitaaluma.
 
Karibu wiki mbili zilizopita kuna mdau alienda pale hospitali ya Ocean Road (ndo alivyodai). Aliyoyakuta huko eti yalimsikitisha sana.

Akaja humu kuanzisha uzi wa kuhamasisha watu wafunge safari waende hapo hospitalini kuwafariji wagonjwa.

Tokea wakati huo sijasikia wala kusoma popote kama wapo watu waliofanya hiyo ziara achilia mbali hata kuwa na mpango.

But of course, wala vumbi ni watu wenye upendo na ushirikiano sana (Cc: Husninyo). That is, ni watu wenye upendo na ushirikiano wa midomoni na vidoleni tu (ku-type na kunyooshea wengine vidole vya lawama)!!!!!!!!!!!

sisi ni wanafiki... period

kutazama mgonjwa si kumsaidia mgonjwa, kumpatia nafuu ya mahitaji ni kumsaidia
 
Back
Top Bottom