MovingForward
JF-Expert Member
- Nov 10, 2009
- 489
- 49
Ninakumbuka vyema wakati wa Mwl Nyerere, rasimu za bajeti za Serikali zilikuwa zinapelekwa kwa wasomi na wataalamu, vikiwemo vyuo vikuu vyetu, hasa UDSM kupitiwa kabla ya kupelekwa bungeni. Lengo likiwa kupata independent inputs na ukosoaji kutoka kwa wataalamu walio nje ya wizara zinazoandaa bajeti. Utaratibu huu ulibadilika kipindi cha Mh Mwinyi. Hadi sasa. Nadhani haya ni matumizi mabaya ya wataalamu wetu ambao wapo tayari kujitolea kutoa maoni yao bureeeee pasipo kulipwa chochote, kwa maslahi ya taifa.
Kwa sababu ya bajeti hizi kukosa inputs za wataalamu, ndiyo maana kila wakati zinakuwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa wananchi. Wataalamu wetu, waliopo katika wizara husika wanaweza kuwa ni wazuri, lakini haiwazuii kufanya bajeti zenye mwelekeo wa wakubwa wao tu, hasa mawaziri. Kama bajeti hizi zingelikuwa zinapata inputs za wataalamu ambao ni independent, zingelikuwa zinabeba mahitaji na umuhimu halisi wa mahitaji ya nchi.
Tunapeleka bajeti Bungeni, sawa. Lakini je! ni wabunge wangapi ambao wanaouelewa wa kitaalamu kuchambua kwa kina bajeti hizi?? Kwa mfano; wakati wa kikao cha bajeti cha mwaka wa 2009/10; nilimwona kwenye TV moja, Mh Mbunge mmoja akitoa maoni akiifagilia bajeti, baada tu ya Mh Waziri wa fedha kuwasilisha hoja. Nilivutwa niingie kwenye tofuti ya Bunge la Jamhuri ya Muunganao wa Tz kuangalia CV ya Mh Mbunge huyo. Nilishangazwa kuona hakuna chochote wala lolote liliojazwa kuhusu taaluma yake. Kisha nikafuatilia, nikabaini inasemekana aliishia darasa la saba. Sasa kama ndani ya Bunge wataalamu wakuweza kuchambua bajeti zetu ni wachache, na wengi ndiyo kama hawa, na wakati huo huo kupita kwa bajeti ni kwa kura ya kutamka NDIYOOOOOOOOOOOO au SIYOOO, hapo tunategemea nini?.
Bajeti nyingi zitakuwa zinapitishwa tu kwa sababu wataalamu wetu watakuwa wakiziandaa kwa mazoea tu, na kukosa independent check ni ugonjwa!!. Lakini pia, tumeona BoT ambapo sehemu kubwa ya waajiriwa ni watoto wa vigogo!!! Nadhani huenda ikawa muundo wa ajira wa BoT unafanana na wizara zetu pia. Kwa hiyo, wataalamu wengi huenda wakawa ni watoto wa vigogo!! Hapo taaluma ni maswali, uzoefu ni maswali na independance ni maswali!!
Nadhani wakati umefika kwa serikali yetu kuwekeza katika wataalamu wetu badala ya wanasiasa tu!!! Wanasiasa wengi si wasomi waliobobea katika masuala ya kitaalamu. Hawawezi kutumulikia bajeti zetu ipasavyo!
Ni mawazo yangu hayo, ndugu watanzania wenzangu.