Budget ya 2011/2012 na uchumia tumbo wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Budget ya 2011/2012 na uchumia tumbo wa CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mku, May 11, 2011.

 1. mku

  mku Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni hari ya kusikitisha sana hasa kiuchumi nchi inavyoaanza kuchumia tumbo baada ya kuwekeza kwenye kuindeleza. Huu ni uchumia tumbo kabisa hasa unaopoona budget ya 2011/2012 ya 11.9 tr/- out of which 7.3tr/- is meant for recurrent votes na 4.5tr/- eti ndo imewekwa kwa ajili ya maendeleo ( Daily News | TANZANIA advised to raise mining tax). Hili japo mie si mwanauchumi najua kuna wanachumi hapa watanisadia ni khali inayoashiria kuwa nchi hii imefirisika kama alivyosema Mh. Zitto. Mkullo kwa moyo wake wa uchumia tumbo uliotukuzwa na serilkali ya chama cha magamba (CCM) anajitapa kwa mbwembwe za utaifa kuwa ni hari ya hatari kuanika uozo wa serikali kwa wahisani eti watakoma kutusaidia. Wakuu hii si huruka ya CCM ya kuficha ugonjwa na kusubiri kifo kiwaumbue?. Uchumia tumbo huu wanauchumi utatutoa kweli mahari tulipo?
   
 2. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  CCM ina wachumi au wahuni? nami si mchumi bali ni MD ila najihoji kama serikali inakopa benki za ndani matrilioni je si kwamba fursa za wananchi binafsi kukopa kwenye benki hizo hizo zitapungua? pia najihoji, kukopa benki za ndani kwa wingi hivyo je, si dalili kwamba godfather wetu nje wametupiga vibuti?
   
 3. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  mhhhh!!!tutafika lakin....................
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tutake tusitake ukweli unabakia pale pale ya kuwa nchi yetu imepoteza dira, imebaki kufuja fedha za walala hoi kwa semina elekezi zisizokuwa na tija yeyote. Kuna haja ya wote wapenda maendeleo kubuni mbinu za kuilazimisha serikali kupunguza matumizi ya kawaida ili kuelekeza fedha nyingi kwenye maendeleo. Hii inawezekana kwanza kwa kupunguza matumizi ya anasa, kama mashangingi, semina zisizokuwa na tija, safari nyingi za nje, usafiri wa daraja la kwanza katika ndege , samani za ofisi na manyumbani zenye bei kubwa n.k. Aidha ukubwa wa serikali nao unapashwa kutupiwa jicho. Hivi kweli Katibu tarafa anafanya kazi gani? Hivi sasa watu hao wanalipwa mshahara wa shs.1.2 milioni kwa mwezi bila mchango wowote wa maana. Vivyo hivyo hakuna haja ya kuwa na serikali kuu wilayani kama kuna halmashauri. Idara ya polisi ambayo mtandao wake unakwenda mpaka wilayani inatosha kuiwakilisha serikali katika ngazi hiyo.
   
 5. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kwa CCM, katika list ya ajenda zao
  Hmna ajenda ya maendeleo!
  Uthibisho ni cheki hali ya nchi baada ya kuitawala kwa miaka 50!
  Hili la budget, hata ya mwaka jana nayo ilikuwa inavituko kama hivi​
   
 6. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Kuna haja ya kutafakari na kuchukua hatua. Kama ni kulalamika watu tumeishalalamika sana na mambo yamebaki yaleyale.
   
Loading...