Ni ipi kauli ya Mh. JK Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM kuhusu MwanaHalisi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni ipi kauli ya Mh. JK Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM kuhusu MwanaHalisi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by cjilo, Aug 4, 2012.

 1. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  Maana nae lilimsema vibaya sana yeye pamoja na chama chake katika matoleo yake, nataka kauli yake, walau aonyeshe furaha yake adharani, kwani Mh. Na CCM yake alishawahi kukubali pia kuwa gazeti hili lilichangia kupungua kwa kura za chama chake kwenye uchaguzi wa 2010

  Pole, Mama Salma Kikwete

  Na Nkwazi Mhango - Imechapwa 07 April 2010

  Madudu mengine ya Kikwete haya hapa | Gazeti la MwanaHalisi
  Na Mwandishi wetu - Imechapwa 19 May 2010

  Umaarufu wa Kikwete 'feki' | Gazeti la MwanaHalisi

  Siri za CCM, CUF zavuja
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 20 October 2010

  Kikwete tumbo moto | Gazeti la MwanaHalisi
  Na Ezekiel Kamwaga - Imechapwa 29 December 2010

  Rais Kikwete aumbuka
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 14 April 2010

  Kikwete ndani ya CCJ | Gazeti la MwanaHalisi
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 18 May 2011

  Kikwete maji ya shingo | Gazeti la MwanaHalisi
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 19 October 2011

  Lowassa, Rostam kumzima Kikwete
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 08 June 2011

  Rais Jakaya Kikwete dhaifu? | Gazeti la MwanaHalisi

  Na Saed Kubenea - Imechapwa 14 September 2011

  Rekodi ya aibu ikulu | Gazeti la MwanaHalisi

  Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 23 November 2011

  CCM sasa wamevuna walichopanda | Gazeti la MwanaHalisi
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 04 April 2012

  Uhalali serikali ya JK ni wa kura tu?
  Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 18 April 2012

  Dua la kuku la CCM laishindwa CHADEMA | Gazeti la MwanaHalisi
  Na Reginald Miruko - Imechapwa 02 May 2012

  Makala hizi na nyingine nyingi zimechangia wananchi kupunguza imani kwa serikali hii ya ccm, nilitegemea basi CCM walau ingeipongeza serikali kwa wazi kabisa kwa kulifungia gazeti linalowanyima usingizi tena kwa muda usiojulikana, inaweza kuwa pia gazeti hili limefungiwa milele
  iwa milele
   
 2. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka ile tume iliyoundwa kufanya utafiti kwa nini ccm imepoteza mvuto kama sikosei iliongozwa na mukama vile(katibu wa ccm wa sasa) ilisema wazi kuwa imepoteza umaarufu kwa sababu magazeti yanawachafua sana hasa mwanahalisi, pengine ndo inaanza kutekeleza mapendekezo ya tume hiyo kuanza kuyapunguza taratibu magezeti hayo na wameanza na shina bila shaka matawi hayatadumu tena
   
 3. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  Wanajidanganya kwani kuna vyanzo vingi vya habari hata jf ni chanzo cha habari huru, ila kwa hili nakosa imani kama jf itaendelea kudumu zaidi ya mwaka, rungu la serikali linaweza kutuangukia muda c mwingi, kwani serikali huwa linatekeleza mapendekezo ya tume za ccm lakini sio tume zinzoziunda zenyewe kama ile ya richmond
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi si tumuache mmiliki achukue hatua zinazostahili dhidi ya hiki kinachoonekana ni uonevu?
   
 5. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ndiyo maana watu wanajificha nyuma ya ID zako coz Ban ingekuwa imeshatembea kwa wote wanao ipinga CCM kupitia waajiri.Nasikia hata kwenye ofisi za serikali wamewapiga biti wafanyakazi ni marufuku kusimama vikundi vikundi.
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kwa nini CCM na JK pekee na siyo watanzania wote wapenda maendeleo? Hivi unaweza kulisifia gazeti ambalo hata siku moja haliwahabarishi wananchi juu hali ya uchumi, mazingira, taarifa za majanga ili kuchukua tahadhari n.k na badala yake kuwa chambo cha baadhi ya vyama vya siasa kujipatia umaarufu. Gazeti ambalo kila mtu anajiuliza ni chuo gani ambacho watumishi wake wamesomea kuangika majungu, fitina, uchochezi na umbea pekee. Hakika kwa Mtanzania ambaye anasimama katika ukweli, lazima ataona umuhimu wa kufungiwa Mwanahalisi kwa vile halipo kwa maslahi ya taifa bali kwa maslahi ya kisiasa tu.
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Ulisoma mapendekezo ya tume hiyo? haya tuambie hilo lilikuwa pendekezo la kwanza, la pili linasemaje? JF hakuna mwelekeo tena kila mtu anaamka anaandika anachokifikiria kichwani ili mradi tu naye aonekane yumo ndani ya JF. Hivi hakuna uwezejano wa kubadili kauli mbui ya JF? ili hata wenye mawazo finyu kama hawa nao waweze kukubalika.
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Siyo sera ya CDM. Unaruhusiwa kusimama vikundi kama mfanyakazi mwenzako ni nduguyo.
   
 9. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60

  Unataka iandikeje hebu check hizi makala

  Reli imetelekezwa, uchumi ukala mweleka | Gazeti la MwanaHalisi

  Hakuna nia ya kuondoa umaskini | Gazeti la MwanaHalisi

  Bila nishati, usalama wa taifa hatarini | Gazeti la MwanaHalisi

  Rekodi ya kuzama kwa meli | Gazeti la MwanaHalisi

  Mkukuta unaufanya umaskini uwe sugu | Gazeti la MwanaHalisi

  umeshawahi kuzisoma hizi makala, jaribu basi kuzisoma hata kwa leo uone kama si za majanga, uchumi na kadhalika? Kama ulikuwa hulisomi kausha acha wanalolijua waseme
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,611
  Likes Received: 4,719
  Trophy Points: 280
  Unategemea JK atoe kauli gani zaidi ya kufurahia kuwa agizo lake la kuvinyamazisha vyombo vya habari vinavyoikosoa serikali yake dhaifu na dhalimu limetekelezwa?
   
 11. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Hayo ni madhara ya kuwa na serikali isiyopenda kukosolewa ,matokeo yake inatumia ubabe kufungia chombo cha habari
   
Loading...