Brown ashika tama II | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Brown ashika tama II

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzizi wa Mbuyu, Jul 2, 2010.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,066
  Trophy Points: 280
  Ni mzee wa miaka 88 sasa, lakini anakumbukumbu nzuri ya alichokiona Tanzania miaka kama nane baada ya uhuru wa Tanzania....

  Hii ni mara yake ya tatu sasa kuja kuishi Nchini na mara zote huwa anafikia maeneo ya mbalizi mkoani Mbeya; kwanza ilikuwa kabla ya uhuru alipokuwa Ofisa wa kizungu katika mashamba ya kizungu huko Mbalizi...baada ya uhuru akaondoka na kurudi kwao. Lakini aliporudi baada ya miaka kama 10 hivi baada ya uhuru alikuta maendeleo makubwa ya wananchi wa Tanzania waliokuwa wakifuta siasa ya ujamaa na kujitemea wakati huo, alishangaa mno kuona majengo mazuri yaliyo jengwa, mashule, na ari kubwa ya wananchi kujiongezea maendeleo yao na nchi yao kwa ujumla n.k Kiasi ambacho kilimfanya ashike tama akishangaa kuona kumbe mtu mweusi akipewa uhuru anaweza kujiletea maendeleo kiasi kikubwa namna ile!!!!
  ..Sasa amekuja tena mwaka huu Tanzania, tena kule kule Mbalizi Mbeya...
  Amekuta hali ni mbaya mno ya wanachi!!! majengo aliyo yaacha yamebomoka lakini bado yanatumika, shule mbovu kabisa, wananchi wanaishi kwa shida mno njaa, madawa hamna, hosp hazipo hata kamazipo mbovu,watumishi wa serikali anao wahoji wanamwambia kulala njaa kwao ni jmabao lakawaida..... Mh..., anashangaa!!
  Mara anaona angani helikopta..ikipita tuktuktuk....anauliza serikali inafanya nini huku wakati hakuna maendeleo yoyote?? ..anajibiwa hiyo siyo ya serikali ni mali ya mkurugenzi mstaafu wa usalama wa taifa anakwenda kwenye shamba lake la hekari 400 huko huko mbalizi..
  Brown Macho yanamtoka kwa mshangao!!! ..anauliza yaani wananchi wanaishi kwa shida hivi yeye amewezaji kupata utajiri woote huu!? wa hadi kumiliki helikopta?? hapa anapata majibu tofauti kutokana na mitizamo tofauti ya waliomuuliza....
  Huyu nasema" mzee anaakili sana huyu hakulaza damu wakati wa utumishi alipiga dili za kufa mtu sasa anaishi kama Obama!"..., mwingine anasema "huyu fisadi tu hana ujanaja wowote tena inaaminika hela hizi kazipata kwa kuuza uraisi kwa mtu ambye hana sifa kabisa, amelipwa mamilioni na mwanae kapewa ubunge na raisi"...

  Basi yanasemwa mengi mno,....lakini Brown anakuja kutambua kuwa uongozi huu uliopo madarakani ni uongozi wa wezi ambao wanajineemesha wao tu na marafiki zaon.n bila kujali wananchi woote..ikiwa tofauti kabisa na uongozi alioucha alipokuja kwa mara ya pili yaani wa mwalimu.
  Brown alipoondoka mbalizi alienda kujionea maeneo mengine nchi, akashangaa wanachi wa kawaida wanaishi mwasha ya shida mno kama wako Dafur!! lakini viongozi wanaishi kama wako kwenye nchi iliyoendelea ssana!!!

  Akahuzunika sana, akatamka hivi ilikuwaje mkachagua KIWETE kuwa raisi? ndivyo alivyomuita JK,
  "Kiwete, mbona umeharibu nchi iliyo kubha nzuuri ssana bhebhe!? Kiwete huogopi Laana za watanzania na Nyerere wewe!??...
  Akakaa kwenye gogo na kuegesha mkono wake shavuni (kushika tama)...na kuendelea kuisikitia Tanzania jinsi iliyo bomolewa...............
   
 2. R

  Rayase Member

  #2
  Jul 2, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sitaki kuamini kuwa mashamba hayo yapo mbalizi labda itakuwa Mbozi.
   
 3. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,066
  Trophy Points: 280
  Poa, ni mwananchi aliesema hivyo...yeye ndivyo anavyojua na kuamini hivyo au ndivyoalivyo ambiwa...
  ...alaa kumbe yako mbozi!!???? jamaa aliwekeza eeh?
   
Loading...