Mpe pole sana huyo dada kwa yanayomsibu. Pia mpongeze sana kwa kutokata tamaa katika harakati za kuokoa ndoa yake. Lakini ajaribu haya yafuatayo, huenda zikamsaidia;
1. Ajiangalie yeye mwenyewe kama ana mapungufu yeyote yanayowezakuwa yanachangia hayo kwa mumewe, then ajirekebishe, if any; Kama vile kutomtosheleza mumewe nk.
2. Hata kama alishawahi kukaa chini naye, na kumueleza hayo, basi asichoke na sasa asisite kuitisha vikao kwa sababu bora kinga kuliko tiba, sasa hivi ndio muda wa kukalisha hivyo vikao ili aibike na aache hayo.
3. Atambue kuwa kosa analofanya ni kuwa muwazi sana kwa mume wake, japo sio dhambi bali ni jambo jema, lakini sasa hapaswi kuanika kila unachohisi kwake. Akusanye data za kutosha, ili siku akiamua kumbana, basi apone kwa huruma na msaada wake tu.
4. Inaonekana huyo dada amempenda sana mumewe, na mumewe ameliona hilo, japo hana appreciation na hilo, amekwishaamini kuwa hataweza kuondoka, let her try to have peace of mind, na pale inapobidi, bora ndoa ivunjike kuliko kujikuta una magonjwa kwa ajili yake.