Broken hearted | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Broken hearted

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mwalimally, May 3, 2010.

 1. m

  mwalimally Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimetumiwa email na mdada mmoja akitaka nione kwa jinsi gani sisi wanaume tunawaumiza wake zetu. Yeye ameipata kutoka katika blogu moja ya kitanzania. Wadau tumshauri huyu dada katika hili lililomsibu.........

  Mimi ni mdada wa miaka 28 nimeolewa na ndoa yangu ina mwaka 1. Nilianza kuishi na huyu mume wangu kabla ya kufunga ndoa ila kwa wakati huo tayari alikuwa ameshajitambulisha na mipango ya mahari na ndoa ilikuwa inaendelea.


  Dada hii siku sitaisahahu maishani mwangu, ilikuwa wiki 2 kabla ya mahari nilipogundua mume wangu anatembea na housegirl wetu ambae alikua akitusaidia kazi ndogo ndogo pale tunapokwenda kazini.

  Iliniuma sana nilipombana msichana akaniambia ukweli wote na kuniomba msamaha. Nilimsamehe ila nikamwambia aondoke ili inisaidie kusahau machungu na kuniwezesha kuendelea na mipango ya kufunga ndoa.

  Nilitamani kusitisha mipango yote lakini ningewezaje kuiambia familia yangu ambao tayari walikuwa busy na maandalizi ya mahari na vikao vya harusi? tuliongea na mume wangu na akaniomba msamaha nikamsamehe nikijua atajirekebisha na kama ni ujana labda ataacha tukishaoana.

  Tulifunga ndoa salama na maisha yakaendelea kama kawaida bila tatizo. Baada ya miezi 6 nikagundua mume wangu ana mwanamke mwingine this time sio yule house girl tena ila alikuwa ni binti umri wa mdogo wangu wa mwisho ambaye amezaliwa 1988!! Sikuona haja ya kugombana na mtoto mdogo kama huyu ila nilimpigia simu nikaongea nae friendly tu nikijifanya kama ni dada wa bwana wake (mume wangu).

  Baada ya kujua kila kitu ndio nikamwambi yule binti kwamba HUYO BWANA WAKE NI MUME WANGU WA NDOA. Yule msichana alishtuka na kuniomba tuonane ili ahakikishe, kweli nilikwenda hadi kwao na picha za harusi ndio binti na mama yake wakaamini.

  Akaniomba msamaha kwamba yeye hakujua kwa sababu huyo mwanaume alimwambia yeye ni bachelor na pia hakumtajia jina la ukweli na alikua akivua Pete kila wanapoonana. Baada ya wiki moja mume wangu aligundua nimeonana na mwanamke wake na aliponiuliza sikumficha nilimueleza ukweli na nilivosikitishwa na hiyo tabia.

  Kwa mara nyingine aliniomba msamaha kama kawaida yetu wanawake, nilimsamehe ili kuiokoa ndoa yetu changa. Maisha yakaendelea ila haikupita hata miezi 3 nikaona mwenzangu amebadilika tabia, kuyachunguza zaidi nikagundua kwamba bado wanaendelea na yule msichana na worse enough ameanzisha mahusiano mengine na ex-girlfriend wa rafiki yake.

  Dada hapo ndio nimezidi kuchanganyikiwa naiona ndoa chungu! Sikuishia hapo nikaamua kuongea nae kwamba tabia anayofanya sijaipenda this time alikuwa mkali na kusema kwamba nisimuingilie kwenye life style yake kwasababu kila kitu amenipa na mimi ndio mke wake hao vimada niwaache kama walivyo.

  Dada ni kweli huyu mwanaume amenipa kila kitu hadi gari la kifahari ameninunulia na pesa za matumizi sio tatizo kwake yaani nakula ninachotaka navaa ninachotaka lakini tatizo langu kubwa sio pesa wala chakula na wala sio wivu kama wengi watavodhania bali sina uhakika kama huyu mwanaume ananipenda kweli au la??

  Pia mwenzangu haogopi magonjwa na kila nikijaribu kuongea nae kuhusu magonjwa hanielewi, je nifanyeje?? naogopa kupeleka hili swala kwa wazazi nahisi kama ni mapema mno kuanza vikao vya mashitaka ukizingatia ndio kwanza tuna mwaka mmoja na bado nampenda mume wangu ila simuamini tena.

  nisaidieni nifanye nini?

  ni mimi dada B wa DSM.
   
 2. bht

  bht JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  kutenda kosa sio kosa kosa kurudia kosa

  hapo huyo dada aamue either to live with that(kwamba mumewe ni fuska) au achape mwendo
   
 3. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo dada hana ht la kujishauri...!aachane naye tu!mumewe ni fuska ataletewa ukimwi ndani!
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  May 3, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Tell sister girl to just leave him...coz it's not worth it at the end of the day. But then again that's her call...if she wants to put up with his bullshit....then it's all gravy.

  But this further proves what I've been preaching...that marriage is so overrated....monogamy is an unrealistic expectation at best and an unrealistic fantasy at worst.
   
 5. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Mdogo wangu hapo ndio pa kuhama mapema sana maana munapoelekea sio pazuri. Samahani utaniona mchungu lakini hayo magari ya kifahari na hizo fedha zitakusaidia nini kama ukiambukizwa hili gonjwa la siku hizi? Hayo anayokufanyia ni dharau kwa kuwa ana fedha na anakuona wewe unamhitaji sana. Inaonyesha dhahiri kwamba huko mbele kuna kiza kikubwa.

  Nakuomba kajihakikishie kama uko salama halafu utimue mbio haraka sana. Ukijilinda vizuri Mungu atakupa mwengine mwenye heshima zake ambae mutapendana kwa usalama.
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,578
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Mie naona huyo jamaa ni tabia yake kama dada anapenda mauti yake kwa njia ya hilo gonjwa letu aendelee kukaa tu huku akisubiri kuletewa lakini kama anapenda maisha yake .akate shauri kuishi maisha ya peke yake ..
  Huyu mwanamme kashindikana kitabia ,hawezekaniki labda aupokee uponyaji..
  si bure!
   
 7. C

  Cozcoz Member

  #7
  May 3, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku hizi ngoma droo wanaume na wanawake ngoma sawa
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  halafu mpwaaz hiyo ''b'' hiyo haya tu...........
   
 9. bht

  bht JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hahaa mpwaz wewe bado, kula kwanza tamu......

  mpwazz jamani hebu muone huyu ndoa ina mwaka mmoja tu uchafu umetapakaa kila kona?

  lakini hii taasisi kama inapoteza 'utakatifu' wake vile?
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hehehehe!kwenye redi ai miiin kwenye bolded,black and underlined hapoooooooooooooooooo.......
  utakatifu upo sana tu,lakini WANA-TAASISI wa karne hii ''DOTIKOM''....haki ya mungu upupu mtupu
   
 11. bht

  bht JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  jamani nyie wanandoa wakati mnaingia huko huwa kweli mnajua wat it takes to be 'wanandoa?'

  siku hizi kweli kuna wanandoa orijino na chipolopolo(doticomu)

  mpwazz wea are u?
   
 12. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  yaani haya mambo ni magumu sana kwa wanandoa weeengi sana!.....lakini mwisho kabisa wanandoa wanaathiriwa na LACK OF EXPOSURE.....!unakuta mtu anaamua kuoa labda anataka umaarufu tu pale kijijini kwao,baada ya muda fulani akija dar anakuta vibintiiiiz na vi-totooooooooooooz vya kufa mtu.anapagawa navyo halafu siku hizi totooooz nyingi huwa zinapenda sana kutoa ''SECTION B'' kwenye gemu.hapo mpwaaz kuna tatizo kubwa sana

  pili kwenye ndoa kuna ile hali ya KUZOEANA!hii hupunguza sana mapenzi KAMA ITAENDEKEZWA

  TALKING OF ME,kwa sasa mambo yangu yanakwenda supaaaz,lakini ni ngumu sana kuniweka mimi kama ''icon'' ya successful marriage kwasababu nina muda mfupi sana kwenye hii mambo

  may be tumuulize x-pin au kaizer ambao ni wakongwe
   
 13. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mmmh broken heart ya kijitakia...
   
 14. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kama maelezo haya ni ya kweli ushauri mzuri unaoweza kumpatia huyo mama katika zama hizi za magonjwa mengi na ya hatari ni kuachana na huyo mume kwa sababu inaonekana huyo bwana ni mgonjwa wa NGONO. Umri wa mwaka moja wa ndoa ni mfupi sana kwa mume kumchoka mke kiasi cha kufanya vile. Labda kuwe kuna tatizo lingine ambalo hakukwambia ukweli
   
 15. m

  mwalimally Member

  #15
  May 3, 2010
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bht umenikosha na hiyo chipolopolo nimecheka mpaka basi. Ni kweli kabisa kuna wengine wanaoa/olewa bila kujua sababu ya ndo.
   
 16. bht

  bht JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  kwenye red haramu imefanywa halali....Mungu tusamehe
  kwenye bluu pia nina shaka kwamba watu wanakurupuka

  hao wa kuwauliza hivi wapogi wapi tena siku hizi??
   
 17. S

  Shebi Gwara Member

  #17
  May 3, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Me naona huyo dada hana haja ya kujiuliza maswali mengi na kuzidi kuumiza kichwa chake, Cha msingi ni kuachana na huyo jamaa na kuangalia mambo mengine ya msingi ya kufanya.
   
 18. D

  Dear Member

  #18
  May 3, 2010
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Inauma sana tena inauma,uyu kaka hana muda mrefu wa kupata UKIMWI,ni anautafuta au anao amekwisha jichokea na maisha sasa anausambaza.
  Dah kwa dunia ya sasa hivi mtu uliyeleta hii email copy hizi msg zipeleke huko kwenye iyo site akazisomemhii ni Hatari HATARI SANA
  RED ALERT Dah
  Na uyu dada ni mvumilivu sana mara tatu kavumilia kisa VItu dah,ndio maana tunaambiwa kila siku wanawake tufanye kazi kwa bidii kuepuka kuwa watumwa wa Mapenzi.na hii sio ndoa ni Ndoano,Dada kimbia na usiangalie nyuma,uyo sio wako,na ndoa huletwa na Mungu kama mwanadamu ukilazimisha haya ya Dunia ndio yanakukuta.
   
 19. m

  mwalimally Member

  #19
  May 3, 2010
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Asante sana Dear kwa ushauri nitamfowardia haya maushauri.
   
 20. bht

  bht JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  mwalimu wee acha tu, naona siku hiz hii kitu ni fasheni tu
  mnaoana asubhi jioni mnaachana.....
   
Loading...