BRN ya Kikwete yazikwa rasmi Ikulu

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,509
2,000
BRN YA KIKWETE YAZIKWA RASMI IKULU.

Rais John Magufuli ameagana na wafanyakazi wa iliyokuwa Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (President’s Delivery Bureau - PDB) ambao wamehamishiwa katika Ofisi na taasisi nyingine za Serikali kwa ajili ya kuendelea na utumishi wa umma.

Wafanyakazi hawa ndio walikuwa wakisimamia utekelezaji wa mpango wa matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now - BRN).

Rais Magufuli amekutana na wafanyakazi hao Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo amewashukuru kwa kazi nzuri waliyoifanya wakiwa PDB na amewataka kuendelea kulitumikia Taifa kwa juhudi na maarifa wakiwa katika ofisi nyingine walizopangiwa.

“Natambua kuwa nyie ni wafanyakazi wazuri wenye ujuzi na maarifa muhimu kwa ajili ya Taifa letu. Mmetoa mchango mkubwa mlipokuwa PDB nategemea mtaendelea hivyo na hata zaidi katika ofisi mbalimbali mlizopangiwa, mkachape kazi kwa kutanguliza maslahi ya Watanzania” amesema Rais Magufuli.

Yaani ameshindwa kuwaambia ukweli kuwa walikuwa wakila mamishahara ya bure
tmp_20019-FB_IMG_14985653603211089783109.jpg
 
Mgodo visa

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
3,304
2,000
BRN YA KIKWETE YAZIKWA RASMI IKULU.........

Rais John Magufuli ameagana na wafanyakazi wa iliyokuwa Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (President’s Delivery Bureau - PDB) ambao wamehamishiwa katika ofisi na taasisi nyingine za Serikali kwa ajili ya kuendelea na utumishi wa umma.

Wafanyakazi hawa ndio walikuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now - BRN).

Rais Magufuli amekutana na wafanyakazi hao Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo amewashukuru kwa kazi nzuri waliyoifanya wakiwa PDB na amewataka kuendelea kulitumikia Taifa kwa juhudi na maarifa wakiwa katika ofisi nyingine walizopangiwa.

“Natambua kuwa nyie ni wafanyakazi wazuri wenye ujuzi na maarifa muhimu kwa ajili ya Taifa letu. Mmetoa mchango mkubwa mlipokuwa PDB nategemea mtaendelea hivyo na hata zaidi katika ofisi mbalimbali mlizopangiwa, mkachape kazi kwa kutanguliza maslahi ya Watanzania” amesema Rais Magufuli.

Yaani ameshindwa kuwaambia ukweli kuwa walikuwa wakila mamishahara ya bure... View attachment 531422
Ndio hawa wameagwa kwa CHIPSI YAI (Zege)...

Kweli AKUFUKUZAE.....
 
kichwa panzi

Senior Member
Sep 18, 2015
119
225
Kulikuwa na vichwa sana mle! Namfahamu jamaa yangu Msellemu!
Kaka vichwa una maana gani? Mimi nina jamaa zangu walikuwa pale kutokea balozi mbalimbali, upigaji ninaousemea hapa ni kwamba matumizi ya BRN hayaendani na kasi hii ya magu, ninavyofahamu hawa jamaa walikuwa benchi toka JPM aiengie sema leo ndio wametangaza kwenye Public.
 
Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
1,384
2,000
Hiyo ingeitwa Poor Result Now

Wameboronga,wameshindwa kushauri kama baada ya shule nyingi za o-level sasa serikali ijenge zaidi shule nyingi za advance na vyuo vya stashahada ili kupokea wahitimu zaidi sasa waliofaulu wapotu mtaani wamekosa shule

Kumbe sasa wamevuna walichokipanda
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom