BRN: na udhalilishaji wa walimu, je taifa litapona?

BRN: na udhalilishaji wa walimu, je taifa litapona?

ferre.g

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2013
Posts
2,215
Reaction score
329
Habari wote wana JF,

Nianze tu kutoa tafisiri sahihi ya neno BIG RESULT NOW-yaani MATOKEO MAKUBWA SASA kama ilivo tafsiriwa ktk waraka huu wa serikali na wanasiasa wetu.

Katika ukurasa wa 3,kwa upande wa elimu zimeanishwa sababu saba[7] zilopelekea kuanguka kukubwa kwa elimu na ukurasa huohuo likawekwa suluhisho kama ntakavoonesha humu,naomba niende moja kwa moja ktk sababu zilopelekea anguko la elimu nchini;

  • 1.Uelewa mdogo wa walimu kitaaluma na kiutalaamu.
  • 2.Kukosa utayari kwa wanafunzi kujifunza na uelewa mdogo ktk masomo utokanao na walimu.
  • 3.Upungufu wa vitabu vya kiada na ziada mashuleni.
  • 4.Ukosefu wa madawati ya kujifunzia na kujifunza.(haya ni yale ya kukalia wanafunzi)
  • 5.kumomonyoka kwa maadili ya wanafunzi na walimu shuleni na ktk jamii nzima.
  • 6.Walimu kujiingiza ktk siasa na kuendesha siasa mashuleni na maofisini.
  • 7.Kukosekana kwa motisha kwa wote walimu na wanafunzi.

SULUHISHO LINALOPENDEKEZWA;
  1. 1.Kuwepo na muda wa masomo ya ziada baada ya muda wa masomo MF;kila siku kutakuwa na vipindi viwili vya lisaa moja moja yani kama leo jumatatu ni PHYSICS NA GEOGRAPHY.
  2. 2.Kwa shule za kwanza ambazo zitaingia 300 bora kitaifa zitapewa cheti cha kufanya vizuri kitaifa.
  3. 3.Shule zingine 600 zitakazo fuatia zitapewa kipaumbele(hakijaainishwa)ili ziingie kundi bora la hapo juu.
  4. 4.Walimu watakao baki kufundisha muda huo wa ziada wapewe chakula cha mchana na ikibidi na fedha kidogo kwa makubaliano na wakuu wao wa shule/walimu wakuu.
  5. 5.Kutakuwa na semina kwa walimu wote watakao husika na programme hii.

UTEKELEZAJI WA WARAKA NA KASORO ZAKE.
  1. 1.Semina wamepewa maafisa elimu mikoa,wilaya na wakuu wa shule/walimu wakuu(walimu wametengwa)
  2. 2.Wakuu wa shule wameagizwa watoe pesa ktk akaunti za shule za kulipia kazi hii(hali halisi shule ziko hoi huu ni mwaka wa pili hazipati fedha na zinaendeshwa kwa mishahara ya walimu wakuu na wakuu wa shule hizi ni zile za kata)
  3. 3.Wakuu wa shule wamepewa ratiba za masomo na kuzileta mashuleni na wanatakiwa kila wiki wapeleke majina ya walimu na vipindi alofundisha kwa muda wa ziada na ni nini alofundisha.
  4. 4.Pamoja na kudai walimu ni wadhaifu kitaaluma...hakuna semina wala pendekezo linalotolewa kuboresha elimu ya walimu hawa.
  5. 5.Walimu wanapewa tshs 1000 hadi 3000 kwa kipindi tofauti kabisa na kanuni na taratibu za utumishi zinazoelekeza mtumishi kulipwa tshs 45000 kwa muda wa ziada utokanao na kuongezwa majukumu tofauti na ya kawaida.
  6. 6.Shule zinapewa vyeti kwa kufanya vizuri,hivi anatakiwa mwalimu apewe cheti hicho sambamba na motisha nzuri,hapa shule zitapewa vyeti....(ukwepaji majukumu)
  7. 7.Maslahi kwa walimu haionekani kama kigezo cha kuanza kuitupa taaluma hii bali inaelezwa ni kukosa taaluma kwa walimu na hakika haitaji maslahi zaidi ni kebehi na hao hao watende wema.
  8. 8.Chama cha walimu hakijui na ni kama kipo likizo...kwani walimu wanaidai serikali mambo mengi sana na ni kama haitaki kulipa na imeziba masikio na imeamua kuongeza mzigo.

Naomba kuwasilisha na nahitaji tujadili kwa pamoja na si kuleta kebehi.
 
Hakuna litakalo tendeka ndani ya serikali dhalimu hii eti big results now huu ni ufisadi mwingine na kauli zao mbiu, mara mkukuta 1 mara 2 mara kilimo kwanza ni vitengo vya ufisadi tuuu
 
Big Result Now-BRN!

Mkuu, kosa kubwa unaloweza kufanya katika maisha yako ni kuweka rehani maisha yako kwa binandamu mwenzako!

Kwa kifupi hakuna serikali hapa tz, ni bunch of wapiga deals! take it or leave it!
 
Hakuna litakalo tendeka ndani ya serikali dhalimu hii eti big results now huu ni ufisadi mwingine na kauli zao mbiu, mara mkukuta 1 mara 2 mara kilimo kwanza ni vitengo vya ufisadi tuuu

Aione ferre.g!
 
Last edited by a moderator:
kiongozi sisi ndo watendaji halisi wa hii big result kiukweli hadi sasa nimemkatalia mkuu wangu kwa kutumia hoja sahihi na hata wale waoga wanaotumikishwa wamenijuza kuwa hakuna jipya litakalofanikiwa na wametoa kasoro pia ikiwemo njaa kali kwa wanafunzi kwani wanakaa shuleni toka asubuhi hadi saa kumi na moja sasa kweli itafanikiwa na je kama kashindwa elewa kuanzia asubuhi hadi saa 9 je ikifika jion ndo ataelewA KWELI HUYU MTOTO KAMA SI MATESO MAKALI KWA HAWA VIUMBE..................anguko kubwa sana laja na magamba wajipange kuona aibu tena na kuandaa upya matokeo ya kupika.
 
watanzania kwa umoja wetu bila kujali dini,chama,rangi au kabila inatakiwa kuungana pamoja kuhakikisha tunafanya mabadiliko ya kiongozi kwa maana chama kilichopo madarakani kimeshindwa kutuongoza vizuri.Nchi haina mwenyewe.
 
kiongozi sisi ndo watendaji halisi wa hii big result kiukweli hadi sasa nimemkatalia mkuu wangu kwa kutumia hoja sahihi na hata wale waoga wanaotumikishwa wamenijuza kuwa hakuna jipya litakalofanikiwa na wametoa kasoro pia ikiwemo njaa kali kwa wanafunzi kwani wanakaa shuleni toka asubuhi hadi saa kumi na moja sasa kweli itafanikiwa na je kama kashindwa elewa kuanzia asubuhi hadi saa 9 je ikifika jion ndo ataelewA KWELI HUYU MTOTO KAMA SI MATESO MAKALI KWA HAWA VIUMBE..................anguko kubwa sana laja na magamba wajipange kuona aibu tena na kuandaa upya matokeo ya kupika.

Umenifanya nicheke, ila kiukweli hali mbaya,
enzi za mwalimu watu walipiga Mikate ya SIHA na Maziwa shuleni bila kusahahu menu za kutisha watu wakiwa shule.
 
Walimu ukataeni ujinga huu na upuuzi huu a serikali dhalimu.
 
Hiyo orodha mbona hawajaonesha kuwa chanzo cha wanafunzi kufeli ni Baraza la Mitihani kama ambavyo Tume ya Pinda ilielekeza na hadi Baraza likalazimishwa kufuta matokeo?

Habari wote wana JF,

Nianze tu kutoa tafisiri sahihi ya neno BIG RESULT NOW-yaani MATOKEO MAKUBWA SASA kama ilivo tafsiriwa ktk waraka huu wa serikali na wanasiasa wetu.

Katika ukurasa wa 3,kwa upande wa elimu zimeanishwa sababu saba[7] zilopelekea kuanguka kukubwa kwa elimu na ukurasa huohuo likawekwa suluhisho kama ntakavoonesha humu,naomba niende moja kwa moja ktk sababu zilopelekea anguko la elimu nchini;

  • 1.Uelewa mdogo wa walimu kitaaluma na kiutalaamu.
  • 2.Kukosa utayari kwa wanafunzi kujifunza na uelewa mdogo ktk masomo utokanao na walimu.
  • 3.Upungufu wa vitabu vya kiada na ziada mashuleni.
  • 4.Ukosefu wa madawati ya kujifunzia na kujifunza.(haya ni yale ya kukalia wanafunzi)
  • 5.kumomonyoka kwa maadili ya wanafunzi na walimu shuleni na ktk jamii nzima.
  • 6.Walimu kujiingiza ktk siasa na kuendesha siasa mashuleni na maofisini.
  • 7.Kukosekana kwa motisha kwa wote walimu na wanafunzi.

Walimu ukataeni ujinga huu na upuuzi huu a serikali dhalimu.
Huo Mradi umeshindwa kabla hata hujaanza, huwezi kupata BRN kama hujatatua matatizo yaliyopo na mpaka sasa hakuna kinachoendelea shuleni kuhakikisha changamoto za kielimu zinatatuliwa. If any, juhudi zilizopo ni za kudhoofisha zaidi elimu kwa kutojali walimu na kukimbilia standardisation ili kupandisha kiwango cha ufaulu.

Ipo hatari miaka ijayo hata wasiojua kusoma watajiunga na Vyuo Vikuu
 
BRN kwa mkoa wa RUVUMA walimu walikusanywa pale chuo cha ualimu songea(matogoro) na kulipwa tsh 40000 tu kwa muda wote waliokaa sasa kwa hari hiyo unategemea kupata matokeo makubwa kama sio kuamsha hasira za walimu zilizoanza kusaulika.
 
BRN kwa mkoa wa RUVUMA walimu walikusanywa pale chuo cha ualimu songea(matogoro) na kulipwa tsh 40000 tu kwa muda wote waliokaa, sasa kwa hari hiyo unategemea kupata matokeo makubwa kama sio kuamsha hasira za walimu zilizoanza kusaulika.
 
Back
Top Bottom