British Series: Suspicion

British Series: Suspicion

Stavros Myles

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2020
Posts
350
Reaction score
390
Kama unapenda series kali zisizo na mbwembwe za hovyo hovyo basi fanya kuitafuta hii series ya Ki-British inayoitwa 'Suspicion'. Kabla sijakupa premise yake nataka nikupe sifa zake mapema ili nikupe hamasa ya kuitafuta.

1. Accent

Humu kuna waigizaji wanaotumia accent tofauti, kuna wale wanaotumia American accent na wale wanaotumia Accent ya Britain. Yaani mambo ya I can hii yu yanatoa hamasa mno.

2. Stori Nzuri.
Humu hakuna stori za mtu kuwa na uwezo wa kutoboa ukuta kwa kutumia ubongo, kuna mambo ya kitaalamu mno.

3. Yupo na Guenevere wa Merlin!
Yap, yule mwanamama aliyekuwa msaidizi wa Morgana (Mchawi 😹😹). Kama umefanikiwa kuitazama series ya Merlin na kuimaliza basi yule Guenevere saizi kabadilika. Kwenye hii series ni mfanyakazi wa kitengo cha NCA huko Britain. Guene amefanya noma na nusu humu amefanya kazi ya hatari mno.

Kabla uzi haujawa mrefu ngoja niwape Premise ya hii series.

Long Premise (😹😹😹😹):

Mtoto wa mwanamama tajiri anayefahamika kwa jina la Leo Newman anatekwa na watu waliovaa masks. Kutekwa kwake kunarekodiwa kwenye camera ya CCTV camera kwenye ghorofa ya 11 katika hoteli ya Park Madison. Baada ya kutekwa kwa huyo kijana video hio inatumwa online kupitia mtandao wa Goleaks.com. FBI wanaingia kwenye utaratibu wa kumtafuta kijana huyo, katika maongezi ya kwanza ya mama wa mtoto - Katherine Newman special agent Scott Anderson anapata habari ya kwamba Leo Newman alikuwa mwanafunzi wa chuo cha Oxford nchini Uingereza.

Huko uingereza watu watatu wanakamatwa wakiusishwa na utekwaji wa Leo Newman, mtu wa kwanza ni Lecturer wa Oxford anayefahamika kwa jina la Tara McAllister, mtu wa pili ni Natalie Thompson ambaye ni mfanyakazi kwenye kampuni ya biashara. Mtu wa tatu kukamatwa ni Aadesh huyu ni Guru wa Computer. Kila mtu alikamatwa muda wake na kuulizwa maswali kuhusu utekwaji wa Leo Newman, wakati wa mahojiano special Agent Scott Anderson alikuwa akihusika kukaa kwenye chumba cha mahojiano lakini hakuruhusiwa kusema chochote kulingana na mambo ya mipaka ya kazi (Jurisdiction). Guess what?, anayefanya mahojiano ni mwanamama Guenevere ambaye jina lake la ukoo analotumia ni Okoye.
Mahojiano hayo yanamkuta Tara McAllister akiwa na muunganiko na utekaji wa Leo Newman ambao ukichimbwa zaidi utafanya ausishwe kabisa na kesi hiyo. Tara McAllister alikuwa miongoni mwa walimu waliokuwa wakikataa admission ya Leo Newman hapo Oxford baada ya kugundua ya kwamba mama yake Leo alitoa msaada wa kifedha katika chuo cha Oxford, sababu kubwa aliyoitumia ilikuwa ni kwamba Leo hakuwa na vigezo vya kuingia chuoni hapo ila alipewa nafasi ya kuingia hapo kwasababu ya msaada wa mama yake. Mahojiano yalivyoenda mbali zaidi iligundulika ya kuwa Tara alitoa speech huko Marekani baada ya kukaribishwa na kampuni ya mwanamama Katherine Newman akiwa anashukuru kwa chuo cha Oxford kupata msaada kutoka kwenye kampuni hiyo. Tia kapuni tuendelee tena.

Aadesh yeye baada ya kutiwa katika chumba cha mahojiano anaulizwa kwanini alienda marekani na kutoa taarifa za uongo kwenye kampuni iliyotaka ifanye naye kazi, jibu rahisi ti linamtoka "nilitaka wajue nafanya kazi ki professional, nakumbuka niliwaambia nakaa Marekani na ndio maana nilikubali waliposema tukutane New York".

Bibiye Natalie Thompson baada ya kuingizwa chumba cha mahojiano anaanza kujitetea akijinasibu ya kwamba mumewe mtarajiwa (kwakuwa alikamatwa akiwa kanisani akitaka kufunga ndoa) ambaye anafahamika kwa jina la Joe atakuja kumtoa mahali hapo. Huko mbele kunavyoendelea Natalie anakutwa hatia ya kusaidia makampuni kuwa tax efficient (😹😹) yaani kama kampuni inatengeneza kiasi cha £9000 kwa mwaka kampuni hiyo inafanya mchakato wa kuzitoa £3000 kwenye utaratibu formal unaotambulika na Serikali na Natalie anatumika kuzitawanya hizo hela na then baada ya mambo kutulia Natalie anawarudishia wahusika pesa zao kwa mfumo safe (usioruhusu wala kuhusisha Serikali kabisa) na yeye anapata malipo yake. Natalie akiwa anaongea na Guene anakiri ya kwamba mdogo wake wa kike anayefahamika kwa jina la Monique ana uwezo mzuri sana (Akili nyingi) na alivyoona mdogo wake amefanikiwa kupata Nafasi ya kusoma Marekani alipambana na kujihusisha na hiyo biashara ili akidhi pesa za kumlipia mdogo wake.

Kwa upande wa Aadesh yeye alienda marekani ili apate pesa zitakazomsaidia atoke kwenye nyumba ya Wakwe zake (Mama na Baba wa mke wake) na aanzishe maisha mapya, Mke wa Aadesh alikuwa akikataa kupata ujauzito kwakuwa alimuona Aadesh kama mtu asiyeweza kutegemeeka kabisa na hii ndiyo drive iliyompa moyo Aadesh kupambania kupata mega deal ambayo ingeweza kumfanya atusue kwenye maisha. Lakini bahati haikuwa upande wake kwani alijikuta ndani ya Chumba cha mahojiano akishukiwa kuwa miongoni mwa accomplice wa utekaji.

Kukamatwa kwa hawa watatu kunatokana na wao kuwepo katika hoteli moja aliyotekewa Leo Newman. Na katika hoteli hiyo hiyo kuna muuaji ambaye ana experience na mafunzo ya Kijeshi anayefahamika kwa jina la Sean Tilson alionekana akiingiia humo humo na baada ya dakika chache naye Aadesh aliingia sehemu ya bafu ambako Tilson aliingia hapo awali. Tara yeye baada ya kupata kinywaji alijituliza maeneo ya kaunta. Kwa upande wa Natalie yeye naye alikuwamo hotelini.

nisije nikaimalizia fanya mchakato uitafute
 
Jamii forum bwana,movie ina rating ya 6.2/10 Imdb unaisifia hivi,je ukija angalia movie yenye ratings za 9.5/10?
 
clinician, rating za idmb ni maoni ya wadau kulingana na vitu vingi walivyoviangalia wao, wengine wanaangalia characterization, story, character engagement, mwanzo na mwisho wa episodes, graphics na mengine mengi.

Kwa upande wangu nimependa story na ndio maana nimeamua kuianzishia thread humu Jf. Ninaamini katika mawazo yangu na mtazamo wangu, ila sipingi ratings za idmb.

Tumetofautiana kwenye vitu tunavyovipenda kwenye movie/series. Japo Fast Furious hii ya recent ni kali ila siwezi kuifagilia kwa upande wangu kwakuwa nimeona matukio ambayo siyakubali kabisa. So in a simple explanation kila mtu ana radha yake 🤣🤣
 
Kila nikiiona nilikuwa natamani kuidownload ila naiacha. Ngoja nitaipakua sasa.
 
Kiukweli accent ya British hua siipendi, ndio maana series ya Last Kingdom ilinishinda
 
accent yao sio nzuri sana wakiongea wanazingua utaskia mate “hau abaut glaas of wooaa” ila wanawake wakiongea inakua tamu
 
Kama unapenda series kali zisizo na mbwembwe za hovyo hovyo basi fanya kuitafuta hii series ya Ki-British inayoitwa 'Suspicion'. Kabla sijakupa premise yake nataka nikupe sifa zake mapema ili nikupe hamasa ya kuitafuta.

1. Accent

Humu kuna waigizaji wanaotumia accent tofauti, kuna wale wanaotumia American accent na wale wanaotumia Accent ya Britain. Yaani mambo ya I can hii yu yanatoa hamasa mno.

2. Stori Nzuri.
Humu hakuna stori za mtu kuwa na uwezo wa kutoboa ukuta kwa kutumia ubongo, kuna mambo ya kitaalamu mno.

3. Yupo na Guenevere wa Merlin!
Yap, yule mwanamama aliyekuwa msaidizi wa Morgana (Mchawi 😹😹). Kama umefanikiwa kuitazama series ya Merlin na kuimaliza basi yule Guenevere saizi kabadilika. Kwenye hii series ni mfanyakazi wa kitengo cha NCA huko Britain. Guene amefanya noma na nusu humu amefanya kazi ya hatari mno.

Kabla uzi haujawa mrefu ngoja niwape Premise ya hii series.

Long Premise (😹😹😹😹):

Mtoto wa mwanamama tajiri anayefahamika kwa jina la Leo Newman anatekwa na watu waliovaa masks. Kutekwa kwake kunarekodiwa kwenye camera ya CCTV camera kwenye ghorofa ya 11 katika hoteli ya Park Madison. Baada ya kutekwa kwa huyo kijana video hio inatumwa online kupitia mtandao wa Goleaks.com. FBI wanaingia kwenye utaratibu wa kumtafuta kijana huyo, katika maongezi ya kwanza ya mama wa mtoto - Katherine Newman special agent Scott Anderson anapata habari ya kwamba Leo Newman alikuwa mwanafunzi wa chuo cha Oxford nchini Uingereza.

Huko uingereza watu watatu wanakamatwa wakiusishwa na utekwaji wa Leo Newman, mtu wa kwanza ni Lecturer wa Oxford anayefahamika kwa jina la Tara McAllister, mtu wa pili ni Natalie Thompson ambaye ni mfanyakazi kwenye kampuni ya biashara. Mtu wa tatu kukamatwa ni Aadesh huyu ni Guru wa Computer. Kila mtu alikamatwa muda wake na kuulizwa maswali kuhusu utekwaji wa Leo Newman, wakati wa mahojiano special Agent Scott Anderson alikuwa akihusika kukaa kwenye chumba cha mahojiano lakini hakuruhusiwa kusema chochote kulingana na mambo ya mipaka ya kazi (Jurisdiction). Guess what?, anayefanya mahojiano ni mwanamama Guenevere ambaye jina lake la ukoo analotumia ni Okoye.
Mahojiano hayo yanamkuta Tara McAllister akiwa na muunganiko na utekaji wa Leo Newman ambao ukichimbwa zaidi utafanya ausishwe kabisa na kesi hiyo. Tara McAllister alikuwa miongoni mwa walimu waliokuwa wakikataa admission ya Leo Newman hapo Oxford baada ya kugundua ya kwamba mama yake Leo alitoa msaada wa kifedha katika chuo cha Oxford, sababu kubwa aliyoitumia ilikuwa ni kwamba Leo hakuwa na vigezo vya kuingia chuoni hapo ila alipewa nafasi ya kuingia hapo kwasababu ya msaada wa mama yake. Mahojiano yalivyoenda mbali zaidi iligundulika ya kuwa Tara alitoa speech huko Marekani baada ya kukaribishwa na kampuni ya mwanamama Katherine Newman akiwa anashukuru kwa chuo cha Oxford kupata msaada kutoka kwenye kampuni hiyo. Tia kapuni tuendelee tena.

Aadesh yeye baada ya kutiwa katika chumba cha mahojiano anaulizwa kwanini alienda marekani na kutoa taarifa za uongo kwenye kampuni iliyotaka ifanye naye kazi, jibu rahisi ti linamtoka "nilitaka wajue nafanya kazi ki professional, nakumbuka niliwaambia nakaa Marekani na ndio maana nilikubali waliposema tukutane New York".

Bibiye Natalie Thompson baada ya kuingizwa chumba cha mahojiano anaanza kujitetea akijinasibu ya kwamba mumewe mtarajiwa (kwakuwa alikamatwa akiwa kanisani akitaka kufunga ndoa) ambaye anafahamika kwa jina la Joe atakuja kumtoa mahali hapo. Huko mbele kunavyoendelea Natalie anakutwa hatia ya kusaidia makampuni kuwa tax efficient (😹😹) yaani kama kampuni inatengeneza kiasi cha £9000 kwa mwaka kampuni hiyo inafanya mchakato wa kuzitoa £3000 kwenye utaratibu formal unaotambulika na Serikali na Natalie anatumika kuzitawanya hizo hela na then baada ya mambo kutulia Natalie anawarudishia wahusika pesa zao kwa mfumo safe (usioruhusu wala kuhusisha Serikali kabisa) na yeye anapata malipo yake. Natalie akiwa anaongea na Guene anakiri ya kwamba mdogo wake wa kike anayefahamika kwa jina la Monique ana uwezo mzuri sana (Akili nyingi) na alivyoona mdogo wake amefanikiwa kupata Nafasi ya kusoma Marekani alipambana na kujihusisha na hiyo biashara ili akidhi pesa za kumlipia mdogo wake.

Kwa upande wa Aadesh yeye alienda marekani ili apate pesa zitakazomsaidia atoke kwenye nyumba ya Wakwe zake (Mama na Baba wa mke wake) na aanzishe maisha mapya, Mke wa Aadesh alikuwa akikataa kupata ujauzito kwakuwa alimuona Aadesh kama mtu asiyeweza kutegemeeka kabisa na hii ndiyo drive iliyompa moyo Aadesh kupambania kupata mega deal ambayo ingeweza kumfanya atusue kwenye maisha. Lakini bahati haikuwa upande wake kwani alijikuta ndani ya Chumba cha mahojiano akishukiwa kuwa miongoni mwa accomplice wa utekaji.

Kukamatwa kwa hawa watatu kunatokana na wao kuwepo katika hoteli moja aliyotekewa Leo Newman. Na katika hoteli hiyo hiyo kuna muuaji ambaye ana experience na mafunzo ya Kijeshi anayefahamika kwa jina la Sean Tilson alionekana akiingiia humo humo na baada ya dakika chache naye Aadesh aliingia sehemu ya bafu ambako Tilson aliingia hapo awali. Tara yeye baada ya kupata kinywaji alijituliza maeneo ya kaunta. Kwa upande wa Natalie yeye naye alikuwamo hotelini.

nisije nikaimalizia fanya mchakato uitafute
Nimechek episode mbili tu naona kali kinoma, mkuu me pia napenda series au movies za akili nyingi katika mazingira ya kawaida kabisa sio mambo ya G.O.T mafiction kibao unaona kabisa hamna uhalisia na watu wanairate 5 stars. Serie kama breaking bad imetulia kabisa.

Nitajie nyingine kama hizo mkuu niruke nazo
 
Back
Top Bottom