BRELA inakimbiza wawekezaji

BRELA buana, unabadili jina na directors inachukua miezi10. Wanakupa certificate of change of name halafu ukiomba brela search report wanakuletea data za zamani kabla hujabadili.
Na hapo kila service unalipia😎😎
 
Mkuu uko sahihi kabisa. Nina miezi kadhaa nafanya annual return isiyokamilika. Kila mara unaambiwa ufanyie marekebisho/nyongeza ambazo toka mwanzo hazikuonekana. Yaani ni kama mnafanya mchezo wa kujibizana usiokwisha
Umeshindwa elewa nn hapo.Kuhani ula vya madhabauni
 
Nakubaliana na wewe mkuu. Brela ni wapuuzi sana. Kila ukisubmit baada ya siku unakuta umerudishiwa document wanakuambia urekebishe. Hawajali kabisa kuna karaha ya kusaini tena hiyo midocuments. Kuna minimum ya watu watatu wa kusaini kama kampuni ina shareholders wawili. Hao shareholders na company secretary. Usumbufu wa kuwapata hao watu wa kusaini kila mara documents zinaporudi brela hawajali kabisa. Hawa jamaa watumbuliwe.
 
Lipo tatizo kubwa watendaji, pia hawatoi ufafanuzi mzuri hizo additional information. Nimekwama kuhuisha kampuni zaidi ya miezi miine wakidai address directors na hoja minor ambazo zipo tayari...
 
Kuna kitu hakipo sawa hapa
Haiwezekani miaka nenda rudi wawekezaji wanakimbia tu kisa usajili tu
Wafukuzwe wote kama haendi na kazi walizojiamini kuwa wanaziweza
Inasikitisha sana ajira na mapato yanapotea kwa wazembe wachache
 
Shida ya mitano tena,ni kila mamlaka kuibua chanzo cha mapato kwakuwa uchumi ulisha kufa muda,hivyo anayeweza kumnyonga mnyonge kuibua chanzo cha kipato anaonekana shujaa mtaa wa kijani.
 
Kuna kitu hakipo sawa hapa
Haiwezekani miaka nenda rudi wawekezaji wanakimbia tu kisa usajili tu
Wafukuzwe wote kama haendi na kazi walizojiamini kuwa wanaziweza
Inasikitisha sana ajira na mapato yanapotea kwa wazembe wachache
Na kwa Tabia za kitanzania na mifumo yake amini usiamini Hadi tamati ya mitano tena,tutawapoteza wengi,na hakuna anayejali zaidi ya kuangalia chanzo kipya cha mapato.
 
Mimi nalia na Tanesco Geita.
Nilitaka kufungua kiwanda hadi leo wanazunguka tu na maneno.
Tusipobadilika hakuna tunapokwenda
 
Nilidhani kuwa tatizo liko kwangu, kumbe ndo utendaji wa BRELA! Wiki ya nne sasa, ninahangaikia usajili wa kampuni online. Marekebisho yasiyokwisha kila nikituma documents zinaenda, wanarudisha kutaka marekebisho yasiyokwisha. Hii ni HUJUMA, waihujumu serikali yao inayowalipa mshahara na marupurupu kibao.
 
Mimi nilianza kujaza document zao miezi 3 kila siku naambiwa hiki nikiweka naambiwa hiki mara andika sehemu Maarufu ilipo ofisi nikajaza maana nipo karibu na stendi kubwa kabisa hapa mjini lakini wanadai hawaitambui ikabidi nibuni tu sehemu maarufu nikampa jamaa mwingine akanisajilia,
Kitu kingine hawana namba ya huduma kwa mteja zile walizoweka huko kwenye website yao ni personal za watu binafsi ukizipiga kupokea ni shida na wakipokea mara wakwambie hizi ni namba binafsi yaani ni shida sana unatumia gharama nyingi kurudia mara kwa mara kuscan document ileile.!
 
Hivi kuna ubaya gani tukiajili Warundi au wakenya kwenye sekta nyeti kama hizi? Huyu mdudu hawezi kukomeshwa bila kufumua wote na kuanza upya!
 
Hizi tuhuma nzito sana Seniour, nakubaliana na wewe kuwa hii kadhia ipo ila haimaanishi kweli kuwa maofisa wa chini wanafanya makusudi ili wapate "chochote kitu"

Inawezekana maofisa wa chini tofauti tofauti wanashuhulikia Application moja nyakati tofauti.

Ila Brela mjirekebishe hili wakuu, unaseza tuma return ukajikuta unakasirika tu kisa mwenendo.
 
Ngoja majizi chadema waje
Hata Kama unatumwa,Basi tumia na za kwako,hapo kinachoelezwa no uozo wa brela,chadema wanahusika vipi,haki ya mungu,ningekua mod ningekufuta kabisa sio kupiga ban,Kuna wakati mwingine unatakiwa kuwa Makini na kinachojadiliwa,sio Kila wakati Mambo ya vyama tu.
 
Kioja cha mwaka! Taasisi nyeti kama hii haiwezi kutoa namba maalum za ofisi kwa watendaji wake!! Majukumu ya kiofisi yana husiana vipi na nambari binafsi ya simu!? BRELA ni janga kama majanga mengine! Labda hawataki sekta binafsi.
 
Kuna siku nilikwenda pale Brela kisajiri kampuni yangu nyingine maana hapa Shinyanga nilipigwa mizengwe. Nilipofika nikakutana na watumishi wa Brela ambao niliwahi kuwaona Shinyanga kuna mmoja ni Afisa Utumishi. Nikajulishwa yule ndio anayeamua Brela ifanye nini na bahati mbaya hajui chochote pale hakuna uongozi mtendaji mkuu wa Brela ni Hopeless fulani anayefundishwa kazi na mtoto mmoja mshirikina Anaitwa Tulizo aliyekuwa hapa Shinyanga. Siku yule mtendaji mkuu atakapo tenganishwa ni huyu muhujumu watumishi aitwaye Tulizo ndipo Brela wanaweza kufanya kazi kiweledi. Nilifanikiwa baada ya marekebisho mengi sana huku mtendaji wa pale akiwa hana analolijua zaidi kuita maofisa wake ambao wamekata tamaa kwa kudharauliwa na kudhalilishwa na huyu mtu aitwaye Tulizo. Hapa Shinyanga hawapendi kumsikia maana watu wengi waliikimbia halmashauri ya Shinyanga kutokana na ushirikina wa huyo afisa mpaka mkuu wa mkoa akaingilia Kati. Pale kuna hujuma ili kumkomoa yule mtendaji mkuu.
 
Umeibua tatizo na kero kubwa kwa taasisi za serikali. Mosi hazina mifumo rafiki ya kiteknolojia inayoungana. Mfano unaweza kuomba tathimini ardhi kinondoni badala ya mtendaji wa ardhi aingie kwenye system aone ramani atakwambia nenda wizarani ukaulize. Yote anakujengea mazingira ya kujiongeza (Rushwa umpatie)

Ilitakiwa kila kitu kijazwe mara moja Brela na upate majibu sio system iku reject urudie mara 5 hapo kwa tunaofahamu systems ni kwamba aliyeitengeneza systems alipewa tenda kwa mgongo wa rushwa hakufanya vizuri kwenye user requirements needs.

Huwa nashindwa kuelewa system kama za nacte unakuta watu wamejazana ofisini kusubiri huduma kama kweli "Online submission iko well functioning" hivyohivyo Tcu. Kuna matatizo makubwa katika usage of ICT systems watu wanapenda manual ili wapate rushwa hata kama ipo inabanduliwa hatua fulani ili mteja ukwame.

Hai make sense unakwenda Tanesco kuomba umeme wanakuambia kalete barua ya serikali ya mtaa wakati kuna Nida system ilitakiwa itoe taarifa zote kwa Tanesco mteja usisumbuliwe. Na bado utasikia kuna Head of ICT nonsense.
 
Hili suala nadhani ni vyema kuliangalia kwa pande zote mbili, kuna wakati inatokea pia sisi wenyewe tunaorudishiwa masahihisho tunashindwa kabisa kufanya marekebisho kama tulivyo elekezwa na badala yake tunaenda kuharibu zaidi kwenye mfumo.

On the other BRELA inahudumia Watanzania waliondani ya nchi na nje ya nchi, haina ubishi kuna wadau wanapewa huduma na kuridhika na kuna watu kwa namna moja au nyingine wanakutana na changamoto

Ni vyema tukawapongeza kwa nafasi ambayo wamefanya na kuwapa ari ya kuzifanyia kazi changamoto zao.

Hili suala nadhani ni vyema kuliangalia kwa pande zote mbili, kuna wakati inatokea pia sisi wenyewe tunaorudishiwa masahihisho tunashindwa kabisa kufanya marekebisho kama tulivyo elekezwa na badala yake tunaenda kuharibu zaidi kwenye mfumo.

On the other side BRELA inahudumia Watanzania waliondani ya nchi na nje ya nchi, haina ubishi kuna wadau wanapewa huduma na kuridhika na kuna watu kwa namna moja au nyingine wanakutana na changamoto....

Ni vyema tukawapongeza kwa nafasi ambayo wamefanya na kuwapa ari ya kuzifanyia kazi changamoto zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…